Wednesday, December 12, 2007

Mpenzi jini


Mohamed Ally huyu, ndio jina lake halisi lakini kwa kuwa siku hizi anaimba, anataka aitwe Z Anton, sijui kwa sababu gani, kikubwa ni kwamba ametoka na vibao vyakle viwili, kimoja kinaitwa Mpenzi jini, kingine Binti Kiziwi. Wadau wiki hii wameanza kumjia juu kwamba amewaibia, kutokana na ukweli kwamba theme za songi hizi zinafanana.
Mie simo zitafute uzisikilize...

Chai Hagwe!


Wakati huku baaraaa, tumesahau kabisa kama si kufogeti mambo ya Chai Hagwe a.k.a Chai Maharage, kule Zenji mambo bado kabisaaaaaaaaaa.
Msije mkasema nalonga sana, ...oneni wenyewe...

Pozi...


Mwanangu Man'dhari ya Uhuru Park ni kiboko, ilibidi nile pozi langu la kishamba hapa na kula upepo mwanana kabla ya kutimkia Mombasa na kisha Zanzibar...

Mnh...


Nilikula pozi hapa kidogo, kuangalia huku na huku, lile jengo la duara mnalijua? Linaitwaje mwanawane? Nitajie nikupe zawadi kutoka Nairobi...

Wikiendi Nairoberia...


Jamani samahani kwa kutokuwa hewani kwa muda, nilikuwa Nairobi kuangalia hili na lole, nilishangaa kweli, na cha kwanza ambacho nawaonesha ni suala la displini, wenzetu wanapanda mabasi kwa foleni, ulikuwa unaijua hii? ...chukua kama vipi!

Friday, December 7, 2007

Kesho katikati ya Mwananchi


Kila Jumamosi ndani ya Gazeti l Mwananchi kuna hiki kitu kinaitwa Starehe kinahusiana na burudani na mimi ndio mhariri na msanifu kurasa mkuu wa kijarida hiki. Hili ni jibu baada ya lile swali la wafanyaje Bongo?
AHSANTE

BoyFriend & Girlfriend

Kutambulishwa ukweli!
..unakuchukuliaje?

Ndugu zangu, tumshukuru Mungu kwa kukutana tena na kuweza kupeana hili au lile katika hizi makala zetu rza urafiki wa ujanani, ...yaani kijana wa kike na kiume, nashkuru sana kuwa na watu wanapoteza muda wao kabisa kunisoma, ujue ni baraka kwa kiasi flani? Mtu kupoteza muda wake kunisoma na pia kuniandikia katika hali ya kunishauri? ...nimeipenda hiyo.
Kwa wale waliokuwa wakinihimiza kuhusiana na blog yangu, nimeianza upya na ipo katika mtazamo mwingine sasa, itembeleeni mtakubali, inaitwa Henrymdimu. Blogspot.com, ...ina kila kitu ambacho unataka kujua cha kisasa, na mpaka mada hizi huwa naweka kwa hiyo mnaweza kuwaambia watu waliopo nje wasiyakose masomo haya ninayoyatoa.
Jamani, ..leo nina jipya na linahusiana na huku kutambulishana kwetu kwa ndugum jamaa na marafki na mara nyingine hata wazazi wa pande husika. EEti jamani hiki knaweza kuwa kigezo cha kukusababishia wewe kujisahau na kuhisi huna haja ya kuongeza chachu katika uhusiano wako. Au ni kigezo cha kukuhakikishia kwamba umefika mwisho wa safari yako ya uhusiano? Mi nahisi kama tunakosea hivi....
Maana nimekuwa nikipata malalamiko bwana, watu wanalalama, kwamba Ooh, ..mimi keshanitambulisha kwao, ..halafu anaanza kuniletea matatizo sasa itakuwaje? Au mwingine anakwambia sina wasiwasi, ..mpaka kwao najulikana. Kwani kutambulishwa ndio nini jamani, ...watu wamevalishwa pete kabisa na wakamwagwa sembuse wewe ndugu yangu na mie?
Ktambulishwa bwana msikuangalie hivi hivi mimi ndio nawaambia kama mlikuwa hamjui, kunaweza kuwa na picha nyingine kabisa katika uhusiano wenu, tena ikibidi watu wangekuwa wanakataa, maana bwana, ...twende kwenye vipengele uone mimi ninavyokuchukulia kwanza..

1. Inaweza kuwa danganya toto...
Hivi jamani, katika umri huu tulionao bado hatujashtukia kwamba binadamu, hasa kijana, akitaka lake anaweza kufanya lolote lile ili kuhakikisha kwamba lile ambalo analifikiria kichwani mwake linakamilika? Kama mlikuwa hamjui, sasa shtukieni jamani maana mimi ninayewaambia hivi nimeshuhudia mengi, ...Oohooooo!
Sasa kutambulishwa usije hata siku moja ukahisi kwamba unapendwa saaaaana, inaweza kuwa ni njia tu ya kukuweka sawa ili ujihisi kwamba uko nyumbani. Baada ya siku mbili tatu ndio utakuja kujua kwamba ulikuwa unatambulishwa katika minajili gani. Mtu anaweza kusema hata na ndugu zake kwamba kuna mtu nataka nimuingize mkenge, watu wakakubaliana kukuingiza kingi, ..yaani sanaa tu na mwenyewe kabaki unakenua tu kumbe unachorwa.
WEngine huomba kabisa kwamba mimi nataka kuwajua ndugu zako na familia yako, well ni nzuri kujua mwenzako anaishi katika mazingira gani, sisemi ni mbaya lakini mwisho wa siku, isije ikakusababishia wewe kuvimba kichwa kwamba Mimi mpaka kwao sijui, ...nimefika wananijua, wakikujua ndio nini, unataka kuangalia moyo wa mwenzio, unakuangaliaje? Mmenisoma, sona nia ya kuwavunja moyo, ..nina nia ya kuwaweka sawa nduugu zangu.

2. Usivimbe kichwa, ...jiangalie
Kuna watu bwana, ukimtambulisha tu kwao, kama mwanaume ndio anakuwa keshakuoa na kama mwanamke basi ujue baba huyo ndio mkeo. Basi kila kitu chako atajifanya ana haki nacho na ndio hapo hata tabia zake zilizokuwa pending ataanza kujzionesha, huku kichwani kwake akiwa keshajiaminisha kwamba yeye ndio mwenye mali. Unaona bwana?
tatizo letu sasa, kuna watu siku mbili tu baada ya uhusiano kuanza, watu wanapelekana nyumbani. Mtu masikini ya Mungu hujamjua yukoje kwa kuwa ni Handsome au labda ndio figa namba nane, unamkokota mpaka kwa wazazi wako. Na mwenyewe kwa kuwa ana lengo la kujifagilisha basi anakwakwatika na kuosha vyombo, mara kapika, ili mradi tu kuwateka akili wazee ambao hawakawii kukwambia baba, ...hapa umepata, baada ya mwezi sasa ndio unagundua kwamba umepatikana.
Sasa hapa ndio ukijidai kuwasomesha wazee kwamba nimegundua kwamba huyu hanifai, hawakuelewi, kwa sababu ujinga anaokufanyia wewe wao hawezi kuwafanyia.
Umeona? Ukizingatia pengine katika kumtambulisha kwako huyu mwenzio ili akubalike kirahisi inawezekana uliongeza chumvi na mbwembwe nyingine, ili mradi kumuweka kwenye matawi, kuiondoa sasa hii imani, ujue inakuwaga ngumu sana? Kama hujui waulize wenzako...

3. Wakati mwingine inaharibu tu...
Kama wewe ni msichana unayependa kutambulishwa, na wanaume wa siku hizi tulivyo unaweza kumaliza Dar nzima, Sitting room zote unaweza kuzikaa na mwishoni sasa, ..unaweza kujikuta unaanza kurudia nyingine, kwamba ulipita kwa mjomba mtu, sasa unakuja kwa binamu ama mdogo wake au kwa marafiki zao.
kwa nini haya mambo yetu tusiyaanze tu kimya kimya kisha mwisho wa siku tukaja kumaliza taratibu jamani? Maana unatambulishwa weeeeeeeeeee, mwisho wa siku unakutana na mtu ambaye ushatambulishwa kwake kama mara nne na marafiki wanne tofauti. Si unajua ilivyo?
Mwanzo ulikuwa Boyfrriend wa Jane ambaye ni rafiki wa Maria, ambaye ana rafiki yake anaitwa pendo, naye unaenda kutambulishwa kwake, ...hivyo hivyo na mwisho wa siku unakuta umemaliza kampani nzima!
Sijui kama nakosea lakini ukweli ni kwamba, hii bwana mwisho wa siku ina madhara sana mjue...
Naomba niishie hapa ndugu zangu

Watasha wa Yanga


Hawa mabwana ndio wanaoikochi Yanga kwa sasa, wabongo tumekuwa hodari kweli siku hizi wa kuleta makocha kutoka nje, ...hii ni baada ya Maximo kuleta mageuzi

Dada yetu...


Mwili wa dada yetu, Kanali Leticia Oswarl, aliyefariki kwa ajali ya Ndege ya KQ akitokea Ivory Coast umeshaingia nchini tayari kwa shughuli za mazishi, tumuombee astarehe katika amani...

Thursday, December 6, 2007

Lamar


Huyu jamaa anaitwa Lamar, ndio mtayarishaji mwenye umri mdogo kuliko wote ambaye anatisha kama njaa, anatokea 41records, kwa habari zaidi usikose kuangalia hapa kesho, ..kuna habari zake na pini ambazo amewahi kutengeneza...

Ze Family!


Mkunga mkuu wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk Nasawe akiwapa usia wamama watatu wambao familia zao jana zilikua ghafla, wakati Ashura Athumani(kulia) alipojifungua watoto wanne, na wenzake Asha Idd(Kushoto) na Stamili Ali walijipatia watoto watatu kila mmoja!
Familia zimekua kiukweli, ..na ukata huu wa Bongo, ..sijui...

shavu....


Kocha wa timu yetu ya Taifa itakayoshiriki mashindano ya Chalenji, Marcio Maximo akilonga na wanahabari, huku akishuhudiwa na mhamasishaji mkuu wa timu hiyo Mohamed dewji kuhusiana na shavu alilotoa mhamasishaji huyo ambalo ni dola 30,000, ...iwapo timu itashinda, ..haya jiueni wanawane

Pop Idol tena...


Lile shindano la kumtafuta kijana mdogo mwenye kipaji cha kuimba limerudishwa tena na Multichoice baada ya kutulia kwa miaka, ...safari hii liko bora zaidi, hapa muwakilishi wa Kampuni ya Multichoice, Lucy Kihwele akiongea na wanahabari huku mshindi wa shindano hilo kwa mara ya mwisho akichekelea kwa pembeni, anaitwa Banana Zorro samahani kwa msiomjua, nilikuwa nishasahau kumtambulisha

Wizi mpaka lini?


Kiongozi wa bendi ya muziki wa kizazi kipya inayokwenda kwa jina la The Atomic Band, Anoubakar Shaaban Katwila akilonga na wanahabari kuhusiana na makampuni ya nchini Kenya yalivyowaibia nyimbo zao na kuziuza kama milio ya simu bila taarifa.
Kushoto kwake ni Lumuliko Mengele, muwakilishi wa kampuni ya Push Mobile ambayo wameingia nayo mkataba kwa hapa Bongo na kushoto kwa Mengele ni Khaleed Mohamed, a.k.a TID

Utani mwingine bwana...


Watu wamemchora tena Hoyce bwana, eti karudia tena kulia baada ya Richa kushindwa, ...unadhani nani basi? SupaDeo huyo, mimi simo bwana...

Jamani Mkurugenzi!


Mkurugenzi kwa kampuni ya BenchMark Rita Paulsen akiwa anakatiza juu ya jukwaa la ulimbwende katika tramasha la kuchangia vituo vya watoto walioathirika na gonjwa ya Ukimwi mwishoni mwa wiki.
Hii safi sana, ..wakurugenzi walimbwende wakipatikana kumi kama hawa, ..shwaaaaari!

ShowLove


Siku hizi mambo ya Beef yamewekwa pembeni na watu wanafanya kazi kama inavyothibitika hapa mwanawane, ...Ambwene Yesaya a.k.a AY akila pozi na Chegge Chigunda mtoto wa Mama Said kutoka TMK Wanaume Family.
...hii inaitwa ShowLove bwana

Wednesday, December 5, 2007

Mgonjwa wetu, ..bado kidogo


Kila mtu amekuwa akiniuliza kuhusiana na Emanuel Didas, ambaye alipasuliwa Mguu badala ya kichwa na sasa yuko India kwa matibabu, hii ilikuwa mara yangu ya mwisho kumuona pale Muhimbili, ...tunasubiri majibu jamani kuweni na subra...

Singizi


Baada ya mihangaiko ya hapa na pale kijana kajisogeza pembeni ya gari na kuuchapa, unaijua kazi yake? Ni kukinga mkono tu na kujijazia vikoini vyetu!
...maisha bwana!

Tuesday, December 4, 2007

Barrick Gold Cup


Jamaa wa madini nao wamejitosa kudhamini michezo ambapo kuna mtanange utaanza karibuni na utakwenda kwa jina la Barrick Gold Cup, ...unaona bwana? Hapa ni Afisa wa Barrick Bwana Teweli akinadi zawadi kwa washindani, ..kazi kwenu warefu!

Mr Favor


Moja ya mambo yanayokwamisha usafiri kwa kiasi kikubwa jijini Dar es Salaam ni foleni, na kuna jamaa husimama kati kati ya barabara na kuzisimamisha kazi taa, na kutuongoza wenyewe ndio wanachelewesha zaidi ingawa wenyewe wanadai wanatusaidia...
Wanadai wanatufanyia Favor na mimi ndio nawaita hivyo hivyo, ..mabwana favor

PPF Towers


Haya akina Mwadawa na wenzako mliokuwa mnanibishia kuhusiana na urefu wa PPF Tower na hilo la hapo Khartoum naomba mliangalie hili kwa picha kisha muende tena pale Blue Pearl mkakae muanze ubishi, ...kitu gani bwana?

Kupima bwana...


Wanazi waliopo ughaibuni wameniuliza katika watu maarufu ni nani namjua kapima nikamuona? Jamani Mzee Kimei, ...Mkurugenzi wa CRDB Bank huyu hapa, ..semeni jingine!

Monday, December 3, 2007

Kinamama halooooo!


Twiga wetu wamewasili leo saa tatu asubuhi hii kutoka Asmara Eritrea ambako wamewatandika wenyeji wao Three Oclock!
Soka letu liko juu, ...we acha tu!

Mtu mzima mdogo


Huyu ndio mtu mzima mdogo, ...akiwa na lindo lake, hana wasiwasi, kalia wewe sasa uone mambo!

Tizi mwanawane!


Wadogo zetu The Kilimanjaro Stars wakiwa katika tizi, tayari kwa mambo yetu yale, hawa wako chini ya Tinocco, ..soka letu bwana siku hizi....
We acha tu!

Transpotesheni!


Hapa sio kijijini, ni Mbezi Dar Es Salaam, usafiri uko mgumu sana, watu wameamua kurudisha zile za kuleeeeeee...baiskeli mwanangu, hapa ndio zinasafirisha abiria na chini zimepaki na madereva wake zinasubiri abiria....
Kudadadeki!

Mambo bado...


Suala la usafiri kwa wanetu bado ni gumu ingawa tunaambiwa kila siku kwamba angalau sasa tuna maendeleo, bila kujali hatma ya Taifa hili la kesho.
Hapa kuna kusoma kwa umakini kweli baada ya kupigana vipushi kwa sana na makonda? Hebu nipeni maoni...

Sunday, December 2, 2007

Toleo la jana


Kuna mdau wa mtoni jana kaniuliza kama nimepigwa chini kuendesha pullout kama mwanablogu mmoja hivi maarufu sana ambaye alipewa ya kiinglish akashindwa? Nimemjibu No, na uthibitisho ni huu, kitu cha jana hiki, ....nimekidesign na kukiEdit pia, ...kudadadeki!
Kuna stori humu ndani bwana, kumbe lile songi la Pipi Kijiti linalofanana na la 50Cent kumbe sio mali ya Langa Kileo? Ni ya huyu dada anaitwa Nyangi...
Kamata Kopi kama uko Bongo!

Boyfriend & GirlFriend

Kuishi Pamoja!
...ni kweli kunapoteza nafasi ya ndoa?

Jamani Eeh, ....mwaka umeisha, na kama ulikuwa hujui kabisa, leo ni Desemba moja, ..unaona bwana? Siku ya Ukimwi duniani, hapa nilipo mwenzia nimepima tangu jumatano na niko pa, na miaka hii 32 sasa nahisi kama nioe hivi, ...au mnasemaje majamaa? Nshakuwa mtu mzima bwana ngoja niangalie kushoto na kulia kisha nikae upande wa pili wa mabachela niwe mpinzani wao. Nahisi italeta maana.
Tafakuri yetu ya leo jamani inatokana kama kawaida na ujumbe mwingi ambao huletwa na wasomaji wetu, ...kwa kawaida huwa naangalia wasomaji wengi wameongea kuhusiana na nini? Wengi wao wiki hii wamenogewa na penzi, wanataka kuhakia kwa wapenzi wao, wake kwa waume, tatizo liko kwa akinadada, wanahisi kama wakihamia tu, ndio kuolewa basi maana kutakuwa hamna jipya!
Mnanisoma?
Vijana kama vijana, wamekaa chini na kujadiliana jinsi hizi pesa za kwenda nyumba za wageni zinavyopukutika, au mara huyu kampa huyu hela ya kula wakati wangekuwa nyumba moja wangepika na kula kwa gharama nafuu na ule ukaribu tu wa kushauriana hili na lile ukiwepo pia ni sawa, maana kama kusomana tabia huu ndio muda wake? Lakini sasa, wakinadada wanadai kwambaaaaaa, ukishakaa na mtoto wa kiume, ...kuolewa sahai, anakuchezea kisha akuache. Hii ni kweli?
Au ndio twende kwenye mavipengele mwanawane? Haya twendeni tukaone kwa mtazamo wangu mimi ninavyoliangalia hili, huku nikiendelea kukusihi kwamba, si lazima uamini kila ninalosema mimi kwani na mimi jamani ni binadamu wa kawaida tu ambaye nina mapungufu yangu.
Chuja pumba, chukua nafaka, ...tumeelewana?

1. Kwa nia njema? ...mbona fresh tu!
Kuna kitu kimoja ambacho mimi nakiamini kila siku katika maisha yangu na nina imani kwamba hii ni moja ya imani ambazo nitazeeka nazo. Unanisoma? Penzi huleta mabadiliko makubwa katika maisha ya binadamu kama ulikuwa hujui sasa wewe una nia njema na mwenzako kwa nini uogope? Usafi wa nia huleta mabadiliko kama ulikuwa hujui...
Sasa hapa ujue kuna nini, mtu anaweza akawa kabisa ana nia ya kukuchezea, aishi na wewe kisha akuache lakini kuna moja lipo wazi sana. Mwanamke ukiamua kum'badilisha mwenzako mawazo mbona ni kazi ndogo tu? Huduma zile za baba mwenye nyumba kutoka kwa mama, zitamsahaulisha kila kitu na akitoka kwenye mtego huu huyo kashindikana,, usihangaike naye atakuua!
Anza asubuhi maji ya kuoga, atavaa nini, mchana asikose SMS za kumkumbusha kula kama anafanya kazi jioni akitoka kazini mambo yetu yale kama kawaida, ....nina uhakika, nia njema hujenga njia njema.

2. Hapa ndio penye ukweli...
Ujue bwana sisi vijana wa mjini tuna tabia moja ambayo watu wanahisi ni muhimu na ya kudumu lakini ni mbaya sana ya uongo. Mkianza mapenzi, kila mmoja atamdanganya mwenzako kuhusiana na jambo moja ama jingine si kwa nia mbaya, lakini mara nyingi huwa ni katika kuhakikisha kwamba uhusiano unakaa kwenye mstari, lakini mwisho wa siku, uongo ni m'baya!
Unaona bwana, sasa katika kuhakikisha kwamba mnaishi uhusiano salama, njia njema ya kuujua ukweli ni kuishi pamoja. Mnanisoma? Mkikaa pamoja lolote ulilodanganywa utalijua tu. Na mimi nahisi ni bora ukae miezi mitatu na kuujua ukweli ili kama unajitoa ujitoe kabla mambo hayajawa mabaya kuliko kukimbilia kufunga pingi za maisha halafu unakutana na mambo makubwa ukiwa ndani tayari. Ujue ni balaa?
Watu wakitaka yao huficha makucha bwana, hujifanya kuwa na tabia ambayo ni njema sana kwa sababu tu anataka lake, akishalipata anajisahau sasa, ndio unaanza kusema kabadilika, kumbe alibadilika wakati anakutaka, ...kwa sasa kwa kuwa kashakupata, tabia halisi kabisa ndio inakuja sasa.
Sasa kuliko mtu kukufanyia ujinga akiwa tayari keshakufunga pingu za maisha, ni bora ukazijua tabia zake za kweli ukiwa kama nje ya uwanja, ili ufanye maamuzi sahihi, kama utayavumilia haya, kama unahisi yatakushinda mwaya, ...ni bora ujiepushe mapemaaaaa...

3. Penzi la kweli halichuji!
Kama una penzi la kweli inakuwaje unachokwa? penzi la kweli halichokwi, na watu hawa kama wanajigundua kama wana mapungufu huamua kuambiana ukweli na kurekebishana na sio kuamua kuumizana na mwisho wa siku kuachana. Kwa hiyo kama una penzi la kweli kwa mwenzio ujue kuna uwezekano mkubwa sana wa kudumu.
Tabia hubadilishwa na penzi kaa ulikuwa hujui, nikupe njia, muonjeshe kwanza ule utamu wenyewe mwenzio. Ukiona karidhika sasa, mwambie hutaki hiki, na hiki na kile, ...umeona bwana, atabadilika mwenyewe na mtakuwa sawa.
Mi nakwambia, huna haja ya kuogopa kwamba nikikaa naye penzi litachujuka, kutakuwa hamna jipya, kwamba atakuchoka atakuacha. Wasiwasi wangu ni kwamba huenda akanogewa bwana, mambo yakawa mazuri kiasi mwenyewe ukafurahi.
Jamani, mimi mwenzenu naishia hapa, Krismas ndio inakuja jamani, kuna watu wanasema wao hawana simu kabisa lakini wanataka kuwasiliana na ukurasa huu basi anuani ya posta jamani.
Andika kwa :
Henry Mdimu
Boyfriend & Girlfriend
P.O BOX 19754
Dar es Salaam

Kwa Email ni:
Hmdimu@Mwananchi.co.tz

Kwa SMS
+255 787 000 880

Kitu kipya!


Wenzetu wa BongoStarSearch, watu wa BenchMark Productions wanazindua kagazeti kao nao kanaitwa BSS Mag, ..katakuwa mtaani kuanzia Jumanne hii, ...tuwaunge mkono, kanauzwa Tshs 1500.
Kwa nje ndivyo kanavyoonekana hv...

Tonite On BSS


Ile Top 40 ndio leo inaonekana luningani kupitia ITV kuanzia saa tatu na robo ambapo wanatarajia kupigwa msasa kabla ya kuongoa katika mchujo mwingine wa 20 Bora, ..msikose kuangalia wanangu, ..mtu si kwao jamani? Sasa nini?

Mchizi waaaangu!


Mchizi wangu Salama J, ni mmoja kati ya watu wanaonipa moyo sana wa kuendelea na maisha No Matter What, hapa tumekula pozi la KushowLOve baada ya Chit Chat na misele miwili mitatu ya weekend, tarajieni makubwa kutoka humu wazee!
....nimeamua!

Kwa wanazi!

Kuna matatizo yalinipata, ya kibinadamu, ya walimwengu nikaamua kunyamaza kwanza. Si ukweli kwamba sijaweza ku'run' Blog, naweza ila tatizo ni kwamba hawa hawa wanaoisoma wanatafuta kila njia kuniharibu na ndio maana kwa miezi miwili nikawa naangalia sasa nifanyeje?
Nimekuja na maamuzi, ...naendelea na nitafanikiwa, na matusi naendelea kupokea, ..Mungu mkubwa, atanisimamia!
Life is so sweet...
Henry

Tuesday, September 25, 2007

...Mudhihir...


...hatimaye Mudhihir anaonekana kama aliyemaliza tiba, hapa akitoka katika Hospitali ya Muhimbili ambako alilazwa kwa matibabu kwa siku kadhaa, tumuombee apone haraka, na kuendelea kulitumikia jimbo lake la Mchinga...

..keshawasili...


Mheshimiwa Juma Kapuya ambaye jana aliripotiwa kupata ajali huko Tabora ambapo watu watatu waliokuwamo kwenye gari lake walipoteza maisha, akishushwa kutoka kwenye Ndege baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam kwa matibabu zaidi, ambapo kwa sasa amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Sea Cliff...


Kuna mdau haamini kwamba Sea Cliff imefanza, kaniomba kuiona kutoka machoni pangu, naomba nichukue wasaa huu kumwambia, ni hivi...

Kapuya hoi!


Habari nilizonazo ni kwamba, profesa Juma kapuya amepata ajali akiwa katika msafara wake, na ameumia bega la kushoto na kifua, ....huyu ni kiongozi wa pili katika Serikali kupata ajali ndani ya wiki mbili, Mheshimiwa Mudhihir, Mbunge wa Mchinga, naye kakatwa mkono...

Monday, September 24, 2007

Dongo jingine kwa TID


Kufuatia kutangazwa rasmi kujitoa kwa Mwanamuziki Aboubakar Shaaban Katwila katika Bendi inayomilikiwa na Khaleed Mohamed, a.k.a Top In Dar, a.k.a TID, ...nimeruhusiwa kuwarushia wadau wa ughaibuni kipondo hiki ambacho kimechorwa na Msanii Supadeo
...enjoy..

Saturday, September 22, 2007

Mastaa wetu...


Mastaa kibao walikuwepo kwenye MTV Veejay Party, si unaona mwenyewe, Mtu mzima Fid, Mwana FA na wengine kibao walijivinjari, Bongo tamu kudadadeki...

MTV Veejay wa Bongo!


Shindano la MTV Veejay limefika ukingoni wanangu na huyu mdada kushoto anayeitwa Vanessa kutoka Arusha ndio kala shavu hilo, na ataaza kuonekana kwenye macho ya watu huko mbele kuanzia mwishoni mwa mwezi huu, tulikula raha kweli Club Maisha jana, ...nakuletea picha zaidi watu wazima tulivyojiachia Ki VIP...

Boyfriend & Girlfriend

Hivi, unajituma au unataka kutumikiwa?

Jamani imefika ile jumamosi ambayo kuna watu wengi wananiambia kwamba huwa wanaisubiri sana, eti waangalie nimesema nini leo? Jamani hivi mnajua kwamba sasa hivi nakuwa napata wakati mgumu sana ninapofikiria kufanya jambo? na hii ni kwa sababu kuna watu wengi makini wananisoma kwa sasa.
Shukrani za dhati kwa wasomaji wangu wa Arusha, ..tulikutana bwana tukajadili mengi tu na tulifurahi kwa kweli kuonana, wengi walishani watakutana na jibaaaaba hilo, kumbe kakijana tu lakini wengi wameniombea, kila mtu kwa imani yake kwamba Mungu anijaalie busara zaidi, maana ninayosema huwa hayalingani na umbo langu na miaka niliyonayo, eti wanadai naongea maneno ya kijana mwenye umri wa miaka 40, ...jamani!
Tuendelee na ya leo maana hizi sifa nikianza kuzielezea wala haziishi, ...kaka na dada zangu, nimesukumwa kuandika haya ninayoandika leo, kuna watu wananiandikia malalamiko kila kukicha. lawama kwa wapenzi wao wakidai kwamba hawaoni kama wanapendwa, yaani wenzi wao hao hawajitumi kabisa katika mapenzi, lakini kuna jibu nikawaandikia, ambalo liliwafanya wanyamaze, unajua niliwauliza nini?
Sawa hao wenzenu hawajitumi, na nyie wenyewe, mmeonesha jitihada gani kuwaweka karibu, ama mnataka kutumikiwa? Kwani jamani mapenzi ni kupenda ama kupendana? Maana wewe unasema huoni dalili kutoka kwa mwenzako, wewe zako ulionesha zikawekwa benchi? sasa kuna utaratibu wa kuangalia katika haya mapenzi, hasa kwa wale ambao walifuatwa, na sio wao kufuata, mnatakaiwa kujua mambo flani ambayo nitawawekea katika vipengele. Tupo p amoja jamani? ..me naanza:

1.Mapenzi na kuamua!
Hili ni jambo ambalo wengi wa vijana waliokuwemo katika uhusiano mlikuwa hamjalifahanu basi habari ndiyo hiyo. mapenzi ya kutegeana yamepitwa na wakati na ni kujidhulumu na mwisho wa siku utajikuta huridhiki na kila unayemuona maana utagundua kwamba labda hakuopendi kumbe wenyewe mnategeana na mwisho wa siku mnajikuta mnahisiana vibaya baada ya kila mtu kutegea kumuona mwenzake akiwa kajitoa kwa mwenzake.
Kama umeshaamua kwamba wewe uko na fulani haina kutegea kaka ama dada yangu. Umeamua kupenda, penda moja kwa moja, na hatua ya kwanza katika hili ni kufukia mashimo. Uliza kivipi? Unapoona anakosea rekebisha, unapohisi hupendi mambo fulani, ambayo mwenzako anayafanya, mwambie ukweli, na kwa kuwa yeye anakupenda anajirekebisha, wazungu wanasema, 'Love makes things happen', na mimi nawaunga mkono, nimeshuhudia watu wakiacha pombe, wakiacha sigara, wakiacha hata umbea kwa sababu ya mapenzi.
Lakini ukitega, kila mtu utamuona ana tabia mbaya, na kumbe tabia mbaya unayo wewe. na kibaya zaidi sasa, unajikuta umeachana na huyu, umeanza na huyu, ukaenda kwa huyu na huyu na yule na mwisho wa siku umefanya msuruuuru wa watu katika uhusiano wako wa kimapenzi. Na dunia si unaijua ilivyofunyangwa na teknolojia. Ndio yaleeee, unaingia mahala unakuta katika watu kumi, wanne umeshakaa nao mkao wa kimapenzi? Heshima ipo hao?
Unajinyima mwenyewe uhuru wa nafsi unakuwa, au nadanganya? ...semeni...

2. mapenzi huambatana na amani ya moyo?
Ndio maana hapo mwanzoni nikawaambia kwamba ukiamua kufanya uhusiano amua tu moja kwa moja maana uhusiano wa kuchungulia chungulia unakuwa kama hujiamini hivi, unakuwa na moyo wa kusita sita, kuliko kufanya hivi ni bora kuacha kaka au dada yangu maana hutafurahia, utakuwa kama unajinyima haki yako ya msingi.
Sasa mambo ya kukaa kama bosi na kusubiri mwenzako ahangaike ndio nini. Na yeye kwa kukuona hivyo unataka kusujudiwa unadhani atakubali kufanywa mjinga, na yeye huenda akawa na mtu anamnyenyekea, atahisi kwamba kwako hamna mapenzi. Kumbe yawezekana yamo, ila sasa tatizo ni kwamba, unasikilizia kwamba kama kweli lipo, ...ndio unakuta muda unakwenda, mmoja ataona anayeyushwa, mara uhusiano unabomoka, ...kila mtu kivyake!
Unatakiwa kabla ya kumwambia mtu I love you too, umehakikisha kabisa kutoka moyoni mwako kama umeamua na moyo ukiamua kupenda unakuwa na amani na ule uhusiano ambao unauanza. Unaona bwana na ukipata baraka kutoka moyoni mwako, penzi la namna hii hudumu asikudanganye mtu na ukihisi moyo unasita, achana na huo uhusiano, utakupotezea muda bila mwenyewe kujijua, na kama huniamini jaribu, ..haufiki popote uhusiano wa namna hii.

3.Nyie tu na mambo yenu
Kuna kosa kubwa ambalo vijana hulifanya pindi wanapokuwa katika husiano zao. Hupenda sana mambo mawili, moja ni kupenda sana kushirikisha rafiki zao katika husiano zao, yaani kuanzia kwenye maamuzi ama katika jambo ambalo wenyewe huliita ushauri kumbe wanakuwa wanauza silaha za maisha yao. Kikulacho ki nguoni mwako kama ulikuwa hujui, ..we una uhakika gani huyo unayemuomba ushauri anafurahia maisha yako na mpenzio?
Hili ni moja jingina bwana, ni lile la kulinganisha mambo, kwamba mbona flani anafanyiwa hiki mi sifanyiwi? Maisha ni kama vidole mikononi mwako, hayawezi kulingana, kuna aina ya maisha ambayo Mungu amekupangia, unatakiwa kukubali hali uliyonayo na kuirekebisha kwa zana ambazo ziko ndani ya uwezo wako, unaona bwana? ukilazimisha tu unakuwa umeharibu kila kitu.
Nomba niwashauri kitu kaka na dada zangu, rafiki yako mkubwa awe mpenzi wako, kama kweli unampenda, yeye ndio mshirikishe kwenye mambo yako na mwisho wa siku utakuja kuona, kila kitu kitanyooka, unajua hii itatoka wapi? ...katika kuhakikisha kwamba mnaridhiana.
Umri unaenda mbele ndugu zangu, hili nawaambia kila siku, mnafikiri bado tuna muda wa kupoteza vijana wenzangu? Mangapi yanatusubiri kwa ajili ya maisha yetu ya baadae?
Naomba niishie hapa kwa leo ndugu zangu, nina imani somo mmelipata na kama mna la zaidi la kuniambia, naomba mniandikie kule kwenye:
HMdimu@Mwananchi.co.tz
+255 787 000 880
Wiki ijayo, ...nipo hapa hapa, ..msikose.

Hili hapa...


Toleo la kijarida ambacho nakiendesha hapa Mwananchi wiki hii kiko hivi, kuna wadau wanafurahia kuona ukurasa wa mbele. Wiki hii tuna huyu kijana ambaye ana kasongi kake ka Mpenzi jini ambaye kwa mujibu wa wachambuaji wa mambo ya watu ni kwamba, ....kajamaa kanauza kweli!

Full kujiachia...


Weekend hii bwana., watu wanajiachia, hawa ni wadau wa muziki wa kizazi kipya bwana, watoto wa TNG, wakiwa na Joh Makini, kushoto kabisa. B12 wa nne kutoka kushoto, na kisha Lord Eyes wa nako2Nako na mwisho kabisa mtoto anaitwa Makamua, ana traki lake linaitwa Why kwa sasa amempa shavu mtu mzima ChidBeeeeenz!

Thursday, September 20, 2007

Watoto wa Msimbazi!


Ligi ya Vodaco iko karibu kutimua vumbi, hawa ni wana wa Msimbazi wanapasha mwanawane wanasubiri lapa la Jangwani wavaane nalo, sijui historia itakuwa kama kawaida?
...me sijasema!

Taifa Mademu


Ujue tumehamasika sana huku Bongo kuhusiana na suala la soka? Mademu zetu nao tunataka wafikie kiwango, unaona bwana, anza na kuwacheki kwa picha, kisha kwenye wanja tunamalizia, ..kudadadeki!

Wednesday, September 19, 2007

Hapo VP?


Wazee... hii mnafikiri ni nini? Kilimanjaro Kempiski bwana, sasa Ulaya nikafuate nini jamani kujiachia hapa kuna tofauti gani na London? Msinitanie bwana...

Life Oooh life...


Mnaona, ..kijana amekamatwa katikati ya Jiji la dar kwa kosa la kuuza kinywaji baridi, ikiwa ni sehemu ya kutafuta jinsi ya kujikimu na maisha, ...nina imani na wahujumu wa mali za sirikali nao siku moja watakamatwa kwa staili hii hii.
...tuombe Mungu!

Mjeda mpya!


Huyu ndio Mkuu mpya wa jeshi letu jamani anaitwa davis Mwamunyange, mlioko mtoni mmenisoma?

Waitara kaaga!


Jamani george Waitara kamaliza muda wake kwa wale waliokuwa hawajui siku hizi jeshini tua Mwamunyange? sawa? ...asenti!

Tuesday, September 18, 2007

Majibu kutoka kwa Dingi!


Bwana Wilbroad Slaa kutoka Chadema, ameshusha tuhuma nzito kuhusiana na viongozi a Serikali kuhujumu sirikali, Mzee Kingunge kafungua mdomo jana, kasema kwamba atalishughulikia hili, kwa mtindo gani? ....kaa tayari ntakuletea

Naota...


Mwanangu, ndio nimeshuka kwenye hiki Kitu, nikaomba nile snepu moja kwanza nione kama napendeza? Toeni maoni, nataka kumiliki kitu kama hiki ifikapo 2012, Mungu ajaliapo uhai...

Jobu kwa Ben


Si mlisikia kwamba kaka jakaya alimpa kazi ya ukuu wa chuo kaka Ben Mkapa? Kwa mtakaokuwa mnataka kujua mandhari ya kazini kwake, ndio hapa, ...mnakaribishwa kuja kupiga buku!