Thursday, June 11, 2009

Noma kweli, subiria kipindi chake...


Hivi hii mwaka gani unakumbuka? Mtu mzima nilitaka kujikakamua nikahisi mnhhhhhhh....
(M'jokin' was just testing the Mic, heee umetoa mimaaaacho mwenyewe!)

..dah shavu...


Watoto wa THT wamekula shavu kutoka Barrick,. kama M 35hv kwa ajili ya kuendeleza vipaji kikiwa ni kituo cha kwanza kupata msaada wa namna hii kutoka taasisi za nyumbani.
Hapo inathibitisha nini, si ndio kwamba wanaweza sana, au mnasemaje wadau?

Baba na Mwana


Jumapili ijayo ya tarehe 21 June ni siku ya wababa, ..eh bwana kizungu inaitwa Fathrrs Day, sasa ona huyu ni Maunda na huyu ni Mzee Zahir Zorro, katika ile ambayo mimi na washkaji zangu tumeipachika jina la Show Luv

Mzee wa Mashinoshino...


Kipindi hiki ndio wachumi huwa wanaumana sana kuhusiana na nini kiwe nini kisiwe katika Bajeti, hapa nimemnasa Cheyo nje ya ukumbi wa Bunge akijadili kitu na Karamagi..

Wednesday, June 10, 2009

Bata la Ushoto...


Kupanda milima ya Ushoto kazi jamani nilikwenda huku mimi na msh'kaji wangu Sarah ambaye ni Meneja wa bia ya Malta na Aaron.
Sarah ilibidi kutiumia fimbo kupanda, ...mcheki


...tukafika Mimi na Sarah


Tukafika hatimaye, Sarah Aron na mimi...

Tuesday, June 9, 2009

Je wajua?


1. Michoro ya kondom iligundulika katika mapango huko Marekani, michoro hiyo ilichorwa miaka 15,000 iliyopita.Hata hivyo haijulikani kondomu za wakati huo zilikuwa zikitengenezwa kwa 'material' gani.

2. Hapo mwanzo kondomu zilikuwa zikitolewa iwapo tu utakuwa umeandikiwa na daktari, wanaume walikuwa wakiandikiwa na daktari watumie kondomu kwa ajili ya kujikinga na magonjwa ya zinaa na wanawake walikuwa wakiandikiwa watumie kondomu ili wasipate ujauzito.

3. Kondomu ya kwanza ya mpira ilitengenezwa mwaka 1855. Zilitengenezwa maalumu kwaajili ya wanajeshi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Waingereza.

4. Wakati wa vita kuu ya kwanza ya dunia chama cha afya cha Marekani kilikuwa kikipinga matumizi ya kondomu kwa madai kuwa kama mtu ameamua kufanya mapenzi na mwanamke asiyemfahamu anastahili kupata magonjwa ya zinaa.

5. Wakati hapa kwetu ndo tumeingiza mashine za kuuzia kondomu huko mashariki ya mbali mashine hizi zimetimiza miaka 80 tangu zilipoanza kutumika.

6. Kaa tayari kwa kondomu za kupaka, yes unapaka kama mafuta then zinakauka na kuwa kama kondomu uzijiazo, Salama, Dume, Durex n.k. hivi sasa kondomu hizi zinafanyiwa majaribu ya mwisho mwisho kwa taarifa ni kwamba kondomu hizi ninakuwa kama jelly ambayo ukiipaka inapata joto na kukauka.

Mchongo uko hivi...


Mashosti, ...Enikah Bukuku na Carola Kinasha, wakijadili jinsi ya kulivaa jukwaa kabla ya uzinduzi wa albam mseto ya Wa Hapahapa Jumapili ya Juzi, lilikuwa poa sana tamasha...

ShoWluv


Unaambiwa ile kuangalia huku na huku, Abdul wa Maisha Plus si akaibuka? Tukala shot kimtindo...

Malta Guiness Street Dance Africa ya Tanga...


Tanga ilikuwa balaa tulikutana na vijana wanaojua kuzikata ngoma kwa kweli...


...cheki mwenyewe...


Na piaaaaa, ...matonya si alionesha staili mpya za steji shoo?


.....kwa Tanga hawa wanaitwa Faxers bwana walichukua ile kilo sita ya TBL kwa Tanga na wanatarajiwa kuja town mwezi ujaop kwa mashindano ya kimataifa

Wednesday, June 3, 2009

Wa Hapahapa...


Jumapili ya tarehe 7 mwezi huu pale Coco Beach kutakuwa na bonge moja ya Party la uzinduzi wa albam mseto ya Wa Hapahapa, ambapo wanamuziki lukuki wa nyumbani watashiriki, miongoni mwao ni hawa hapa waliokuwa wakiongea nasi hivi karibuni katika Hopteli ya Southern Sun, kutoka kushoto ni Enikah Bukuku, Paul Ndunguru, Frorah Mbasha na Banana Zorro, ...kiingilio ni bure...

Ngwasumaaaz...


FM Academia, wazee wa ngwasuma ndio bendi pekee ya muziki wa dansi ambayo imekula shoo nyingi sana msimu huu wa ulimbwende, hii ni kutokana na ukweli kwamba mshamini wao hana shobo, si unamjua?
Henekeeeeeene, ..kudadadeki!

Mlishtukia?


Amani alikuwepo this weekend ingawa watu walimuona sana Wahu, alikuwa katika Marketers Night ilikuwa poa sana, hivi mlishtukia?

Yalaaaah!


Richie jamani, ...kafa kiflamu? Hii ni katika muvi yake mpya itakayokuwa inajulikana kwa jina la Solemba, kaa mkao wa kuiona...

Tuesday, June 2, 2009

Unamjua fresh Che Guevara?


1. Pamoja na historia ya kuwa jamaa alikuwa akipigania uhuru wa Cuba, hakuwahi kuwa raia wa nchi hiyo, alizaliwa Argentina lakini pia hakuwa na asili ya nchi hiyo, Wazazi wake ni raia wa Ireland. So Che alikuwa Muairish.

2 Wakati huo mtu akiitwa 'Che Guevara' ilikuwa ikimaanisha kuwa mtu huyo anaweza kuwa mtu mzuri au mbaya, baadhi ya watu walikuwa wakimwita jina hilo wakimaanisha mpiganaji lakini wengine walimwita hivyo wakimaanisha muuaji.

3. Jina lake la utani lilikuwa Chacho ambalo kwa hapa bongo angeitwa nguruwe, Suala la kuoga kwa Che Guevara lilikuwa mtihani mkubwa. shati na suruali zake alivaa kwa wiki nzima.

4. Hakuwa akipigana kwa njaa na kukosa elimu, aligraduate masomo ya udaktari mwaka 1953. Alitokea katika familia ya kitajiri tofauti na wapiganaji wengi tunaowasoma leo katika historia.

5. Baada ya harakati alikuwa akiweka silaha chini na kutumia mikono hiyo kulea watoto wake, Che alikuwa baba wa watoto watano, mtoto wa kwanza alimzaa na mke wake wa kwanza Hilda Gadea na wengine aliwazaa na mwanamke mwanamapinduzi, Aleida March.

6. Bolivia wanamtukuza wakiamini kuwa Che ni nabii, huko Cuba sura yake ipo kwenye dola tatu na mashuleni kila siku asubuhi watoto hula kiapo wakisema "tunataka kuwa kama Che".

7.kubwa kuliko yote ni kwamba Che alikuwa akipendwa na watu wengi nchini cuba lakini idadi hiyo ililingana na ya watu wanaomchukia.

Mchagga kapata kazi BSS


Jamani, huyu si Master Jay? Haya kulikoni...