Friday, December 7, 2007

BoyFriend & Girlfriend

Kutambulishwa ukweli!
..unakuchukuliaje?

Ndugu zangu, tumshukuru Mungu kwa kukutana tena na kuweza kupeana hili au lile katika hizi makala zetu rza urafiki wa ujanani, ...yaani kijana wa kike na kiume, nashkuru sana kuwa na watu wanapoteza muda wao kabisa kunisoma, ujue ni baraka kwa kiasi flani? Mtu kupoteza muda wake kunisoma na pia kuniandikia katika hali ya kunishauri? ...nimeipenda hiyo.
Kwa wale waliokuwa wakinihimiza kuhusiana na blog yangu, nimeianza upya na ipo katika mtazamo mwingine sasa, itembeleeni mtakubali, inaitwa Henrymdimu. Blogspot.com, ...ina kila kitu ambacho unataka kujua cha kisasa, na mpaka mada hizi huwa naweka kwa hiyo mnaweza kuwaambia watu waliopo nje wasiyakose masomo haya ninayoyatoa.
Jamani, ..leo nina jipya na linahusiana na huku kutambulishana kwetu kwa ndugum jamaa na marafki na mara nyingine hata wazazi wa pande husika. EEti jamani hiki knaweza kuwa kigezo cha kukusababishia wewe kujisahau na kuhisi huna haja ya kuongeza chachu katika uhusiano wako. Au ni kigezo cha kukuhakikishia kwamba umefika mwisho wa safari yako ya uhusiano? Mi nahisi kama tunakosea hivi....
Maana nimekuwa nikipata malalamiko bwana, watu wanalalama, kwamba Ooh, ..mimi keshanitambulisha kwao, ..halafu anaanza kuniletea matatizo sasa itakuwaje? Au mwingine anakwambia sina wasiwasi, ..mpaka kwao najulikana. Kwani kutambulishwa ndio nini jamani, ...watu wamevalishwa pete kabisa na wakamwagwa sembuse wewe ndugu yangu na mie?
Ktambulishwa bwana msikuangalie hivi hivi mimi ndio nawaambia kama mlikuwa hamjui, kunaweza kuwa na picha nyingine kabisa katika uhusiano wenu, tena ikibidi watu wangekuwa wanakataa, maana bwana, ...twende kwenye vipengele uone mimi ninavyokuchukulia kwanza..

1. Inaweza kuwa danganya toto...
Hivi jamani, katika umri huu tulionao bado hatujashtukia kwamba binadamu, hasa kijana, akitaka lake anaweza kufanya lolote lile ili kuhakikisha kwamba lile ambalo analifikiria kichwani mwake linakamilika? Kama mlikuwa hamjui, sasa shtukieni jamani maana mimi ninayewaambia hivi nimeshuhudia mengi, ...Oohooooo!
Sasa kutambulishwa usije hata siku moja ukahisi kwamba unapendwa saaaaana, inaweza kuwa ni njia tu ya kukuweka sawa ili ujihisi kwamba uko nyumbani. Baada ya siku mbili tatu ndio utakuja kujua kwamba ulikuwa unatambulishwa katika minajili gani. Mtu anaweza kusema hata na ndugu zake kwamba kuna mtu nataka nimuingize mkenge, watu wakakubaliana kukuingiza kingi, ..yaani sanaa tu na mwenyewe kabaki unakenua tu kumbe unachorwa.
WEngine huomba kabisa kwamba mimi nataka kuwajua ndugu zako na familia yako, well ni nzuri kujua mwenzako anaishi katika mazingira gani, sisemi ni mbaya lakini mwisho wa siku, isije ikakusababishia wewe kuvimba kichwa kwamba Mimi mpaka kwao sijui, ...nimefika wananijua, wakikujua ndio nini, unataka kuangalia moyo wa mwenzio, unakuangaliaje? Mmenisoma, sona nia ya kuwavunja moyo, ..nina nia ya kuwaweka sawa nduugu zangu.

2. Usivimbe kichwa, ...jiangalie
Kuna watu bwana, ukimtambulisha tu kwao, kama mwanaume ndio anakuwa keshakuoa na kama mwanamke basi ujue baba huyo ndio mkeo. Basi kila kitu chako atajifanya ana haki nacho na ndio hapo hata tabia zake zilizokuwa pending ataanza kujzionesha, huku kichwani kwake akiwa keshajiaminisha kwamba yeye ndio mwenye mali. Unaona bwana?
tatizo letu sasa, kuna watu siku mbili tu baada ya uhusiano kuanza, watu wanapelekana nyumbani. Mtu masikini ya Mungu hujamjua yukoje kwa kuwa ni Handsome au labda ndio figa namba nane, unamkokota mpaka kwa wazazi wako. Na mwenyewe kwa kuwa ana lengo la kujifagilisha basi anakwakwatika na kuosha vyombo, mara kapika, ili mradi tu kuwateka akili wazee ambao hawakawii kukwambia baba, ...hapa umepata, baada ya mwezi sasa ndio unagundua kwamba umepatikana.
Sasa hapa ndio ukijidai kuwasomesha wazee kwamba nimegundua kwamba huyu hanifai, hawakuelewi, kwa sababu ujinga anaokufanyia wewe wao hawezi kuwafanyia.
Umeona? Ukizingatia pengine katika kumtambulisha kwako huyu mwenzio ili akubalike kirahisi inawezekana uliongeza chumvi na mbwembwe nyingine, ili mradi kumuweka kwenye matawi, kuiondoa sasa hii imani, ujue inakuwaga ngumu sana? Kama hujui waulize wenzako...

3. Wakati mwingine inaharibu tu...
Kama wewe ni msichana unayependa kutambulishwa, na wanaume wa siku hizi tulivyo unaweza kumaliza Dar nzima, Sitting room zote unaweza kuzikaa na mwishoni sasa, ..unaweza kujikuta unaanza kurudia nyingine, kwamba ulipita kwa mjomba mtu, sasa unakuja kwa binamu ama mdogo wake au kwa marafiki zao.
kwa nini haya mambo yetu tusiyaanze tu kimya kimya kisha mwisho wa siku tukaja kumaliza taratibu jamani? Maana unatambulishwa weeeeeeeeeee, mwisho wa siku unakutana na mtu ambaye ushatambulishwa kwake kama mara nne na marafiki wanne tofauti. Si unajua ilivyo?
Mwanzo ulikuwa Boyfrriend wa Jane ambaye ni rafiki wa Maria, ambaye ana rafiki yake anaitwa pendo, naye unaenda kutambulishwa kwake, ...hivyo hivyo na mwisho wa siku unakuta umemaliza kampani nzima!
Sijui kama nakosea lakini ukweli ni kwamba, hii bwana mwisho wa siku ina madhara sana mjue...
Naomba niishie hapa ndugu zangu

No comments: