Friday, May 29, 2009

Dah, noma kweli...


Jamaa walimkuta dukani kwa Mangi kajificha kwenye boksi ili mangi akifungaaaaa, achukueeeee, wakamaliza humo humo!

ShowLuv...


Kutoka Bagamoyo kwa mshindi wa BSS mwaka jana, Bi Misoji Nkwabi(shoto)kumekuja salamu bendi inafanya mazoezi na hivi karibuni kutakuwa na gig la maana kwa wapenda Sweet reggae, hapa ni shavu na mwanetu Caesar ambaye ni mtangazaji wa shindano hilo mwaka huu, ...asenti!

Thursday, May 28, 2009

UHUSIANO WA UJANANI


Ukipata ujauzito?
...nini kinafuata?

Kaka na dada zangu natumaini hamjambo na mnaendelea vema na shughuli za ujenzi wa Taifa, wasomaji mahiri kabisa wa ukurasa huu, ahsanteni kwa muda wenu, mimi mzima na maisha ni mafupi kusema ukweli, lakini nitakuwa nakosea nikiacha kuyapa sifa yake, ...matamu!
Shukrani kwa wasomaji wangu wa Zanzibar walioamua kushuka kwenye boti, na kuja moja kwa moja mpaka Tabata Relini kuja kumuona, huyu mwandishi wa makala wanazozipenda, zinazowagusa anafananaje? Walipoondoka kuna neno waliniambia likanifanya niwe mpole kidogo, unajua walisemaje? Hata siku moja, usithubutu kumkadiria mtu kwa kumtazama. Utakuwa umekosea sana!
Haya, tuachane na hizi kazi za Mungu, naomba leo tuangalie mambo makubwa yanayothusu sisi vijana wa kike na kiume wa kiAfrika, nazungumzia suala la ujauzito leo. Mmeamua kuwa mtu na mpenziwe, ikafikia hatua sijui ndio tuseme mlijisahau, au nini, ni kitu gani cha kwanza mtafikiria kufanya? Au huwa mnajihisii nini mkifikia hatua hili likatokea kaka na dada zangu?
Kusema ukweli jamani, mengi hufikiriwa hapa, kuna watu hufikia hatua ya kutoroka hata makwao, wakihofia ukali wa wazazi wao, au wakihofia aibu kwa umma, imani ni kwamba, mimba nje ya ndoa ni dhambi ya uzinzi, ambayo kiukweli jamii ikijua kwamba unaifanya bila haya haya, linaweza kuwa tatizo.
Mimi nina yangu ambayo nayafikiria katika hili, naomba nipewe wasaa nianze kumwaga vipengele vyangu. Si sawa jamani:

1. Sio ajabu, ..kawaida...
Ukweli uko hivi, kile kitendo tu cha kuwa wapenzi, kwa utamaduni yetu wa kiafrika, iko bayana kwamba uhusiano huu unahusisha pia tendo la ndoa, ambalo mwishilio wake ndio huu, hasa mkiwa sio watu wa kutumia kinga ya aina yeyote. Tunaelewana, kwa hiyo kwa kushiriki tendo la ndoa, suala la kupata ujauzito lina uwezekano mkubwa hapo jamani, nadanganya?
Sasa cha ajabu nini hapo? Umepanda mpunga, mchele ndio huo. Aibu inatoka wapi wakati ulikuwa pengine unafurahia, kinachofuata hapo ni jinsi ya kukabiliana na tatizo lenyewe, kama kweli wewe unaliona tatizo. Lakini kusema kwamba sijui hukutegemea, unajidanganya mwenyewe, kwa kuwa asilimia kubwa, ni watu wanaojua wanachokifanya. Na kama ulikuwa huutaki huu ujauzito, mbona hata tahadhari hukuchukua? Uliutaka bwana!
Atakayekucheka pia atakuwa mjinga, maana waliozaliwa nje ya ndoa siku hizi ni wengi kuliko hata waliozaliwa ndani ya ndoa, unatakiwa kujipanga hapa na jinsi ya kukabiliana na tatizo lenyyewe, ni lako na hutakuwa na pa kulikimbiza, ...unalo hilo!

2. Haichochei chochote!
Kuna akinadada bwaba huamini kwamba ukim'bebea mtu mimba basi kuna uwezekano mkubwa akawa ndio wako wa maisha. Naomba kuchukua wasaa huu kuwatahadharisha dada zangu kwamba hili si kweli kwamba kunibebea ujauzito, kunaweza kunihamasisha mimi kukuoa, au labda kuishi na wewe kama mtu na mwenzake,...kwa akili zetu vijana wa siku hizi, unaweza kuwa unanikimbiza. Tunaogopa majukumu kuliko tunavyoyaogopa magonjwa ya zinaa, ...mdio ukweli mdio ,maana sioni aibu kulisema hili kwa watu. Si tunajijua?
Nimelisema makusudi maana wanaolalamika mtaani wako wengi, ya kwamba wamekimbiwa, huamua tu kubeba mimba bila ya kuwaambia wenzao, kisha huwashtukiza. Jamaa sasa mara nyingi sijui ndio kusema hawajajiandaa na maisha ya malezi, hukataa, au kukimbia kabisa mji. Ukiangalia sio busara lakini sasa utafanyaje na ndio ushakimbiwa?
Tunabakia pale pale pa kukubali matokeo na kuangalia nini cha kufanya baada ya yote hayo.

3. Unaua? ...ni dhambi zaidi!
Hili ni kimbilio la wengi, kukimbilia kutoa akiamini kwamba amemaliza tatizo, kumbe ndio anajitengenezea matatizo zaidi maana duniani kama mlikuwa hamjui, ni Mungu ametuleta, amekupa uwezo wa kupata kiumbe, unakiua, unafikiri unamfurahisha? We ngoja matokeo yake, hukumu siku hizi iko hapa hapa duniani kama mikuwa hamjui.
Hii ni ya kiimani zaidi, fikiria umefanya dhambi ya uzinzi, hutosheki nayo unaenda kuua tena, halafu huyu Mungu unamuangaliaje? Baso utamtaka msaada? Bado utasema maisha yako yamekosa baraka na utakuwa unahisi kama unaonewa hivi, jibu mwenyewe kabla hatujafunga kurasa.
Kutoa mimba ni hatari kwa afya, na kwa kweli hata kiimani ni mbaya kwa hiyo ushauri wangu ni kwamba, kama unahisi kwamba huko tayari jamani kinga mbona zimejaa kibao? Shauriana na mwenzako au kama vipi acha kabisa haya mambo kama huko tayari nayo.
Mimi hapa kwa leo ndipo nahisi niishie, nataka kuwasiliana zaidi na watu wangu mniambie kuhusiana na hili mnaonaje? Niandikieni email:
Mdimu@hotmail.com
Simu:
+255 787 000 880

Kesho baba kesho....


Ndani ya Irish Pub kama kawaida Banana na Dingi yake Mzee Zahir Zorro, pamoja na B Band nzima, watakuwa wanapiga njaa mpaka jua litoke, kiingilio ni buku tatu tu.
....toleka!

Sinza, ...kumekucha!


Haya tena, watu na njaa zao, ule msimu wa Mamiss umefika na tayari mazoezi yameanza pale Vatican, waratibu ni wale wale, karibuni mjionee vimwana, maana shindano liko mbali, mpaka tarehe 18 bwana...

Njaa mbaya...


Uliza hapa tunapiga nini na wapi? Mbeya Mzee, tumegundua kumbe Kitimoto ina Supu?


Kila mtu alishughulika kudadadeki....

Peeeace...


Amani kwa wadau kutoka kwa Mchi'z wangu wa ukweli, ...Majani anawapa Hi wadau wote, tupo pamoko si ndio?

Wednesday, May 27, 2009

Mwana...


Wanangu hii ni Respect kwa mwanangu, Julieth Kulangwa, kichwa kingine ambacho hamjakishtukia, lakini kiko poa sana kwenye nafasi kama yangu na huwa anapiga mzigo na Project Maisha Plus, niko naye kwa ofisi, tulikuwa tunaenda lunch tukakutana na mchizi ana kamera tukaomba shot moja tuwape zawadi wadau..

Mambo yameiva...


Umeona bwana, Miss Tanga hii hapa, wiki ijayo inakuwa hewani, tarehe 6, mwezi ujao ndani ya uwanja wa Mkwakwani kutawaka Moto, kutakuwa na Matonya, Belle 9, ChidBenz, na msanii mojawapo wa kimataifa, unatakiwa kuwepo mzee, pichani ni Da' Asmah na Da'Sarah wakiwasilisha kwa wanahabari leo jijini.

Tanga, mpo ready???!!!


Kimbembe cha Malta Guinness Street Dance Africa wiki ijayo kinahamia Tanga, jamaa wameshaondoka kwa ajili ya kazi na sasa wako Tanga Hotel kwa ajili ya usaili, unakaribishwa kufanya usajili wa kundi lako ili mambo, ...yaendeleeeeeeee!

Roho 6...


Filamu mpya ya Roho Sita itaingia sokoni hivi punde ikiwa imesheheni visa na mikasa visivyofikirika katika fikra za kawaida. Mkurugenzi wa Filamu za Tollywood Movies, Hamie Rajab ameiambia Starehe kuwa roho Sita ni kati ya sinema nzuri zenye ubora wa Kimataifa ambayo inaweza kulitambulisha soko letu la filamu duniani. Muvi hiyo itaingia mitaani Juni 1, 2009.

usilolijua bwn...


1. Umeshawahi kujiuliza hivi nisipooga kwa siku kumi itakuwaje? Ndani kutakalika kweli? Halle Berry amewahi kuishi kwa siku kumi bila kuoga wala kupiga mswaki. Hii ilitokea alipokuwa akiigiza filamu ya Jungle Fever, ama kweli hakuna kazi rahisi anasema.

2.Kama kuna mtu duniani angetamani kumsaidia anasema angependa sana kumsaidia mwanamuziki mahiri wa pop, Britney Spears. Anasema anamwonea huruma sana hasa anapoandikwa kwasababu anayajua maumivu yasababishwayo na vyombo vya habari. "unakuwa umeumia tayari lakini vyombo vya habari vinakuongezea maumivu kwa kukuandika vibaya" anasema

3. Aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na JT( Justine Timberlake) baada tu ya kuachana na Erick Benet mwaka 2003. Hata hivyo uhusiano huo ulikuwa wa muda mfupi sana.

4. Ingawa ukimwangalia huwezi kufikiria kama mwanamke huyo anaweza kufanya upasuaji wa viungo lakini mwenyewe anasema Never say Never anafikiri ipo siku anaweza kufanya upasuaji.

5. Hasimu wake mkubwa ni Charlize Theron hata hivyo anasema hajali sana na huelekeza nguvu zake kwenye kazi na si kwenye mambo kama hayo.

Kutoka Zizzou Entertainment...


Kutoka kwa Zizzou Entertainment tunaambiwa kwamba, ..tarehe 3 Julai kutakuwa na Bonge la onesho la kimataifa la R&B, ambapo hawa watakuwepoooooooouuuum


...na hawa pia, watapiga showwwwwwwwwwwummmmmm!

JK wa misele?


Juu ya kuwa Rais wa kwanza wa Afrika kukutana na Rais Mteule wa Marekani, gazeti la The Economist la tarehe 7 Mei, limemchana rais Jakaya kwamba badala ya kutatua migigiri ya nchini mwake, yeye anapiga misele tu kuitangaza nchi.
Limehesabu katika habari yake hiyo yenye kichwa "Tanzania: Waiting for the great leap foward" kwamba hii ni mara ya sita kwa Jalaya kuingia Marekani tangu ashike madaraka.

Kama kawa kama dawa...


Ongeeeni eeeeh lakini wiki hii ndio wale watoto wa mikoani wanatua, na watakuwa Girrafe View Hotel ambapo watakuwa wanaanza ile kambi ya kitaifa ya Bongo Star Search, majaji wako fiti tayari kwa kazi ya kuhakikisha kwamba vipaji vinafikia hatua nyingine.
Ni hayo tu, ..asenti!

Tuesday, May 26, 2009

Enhe, ...tuendelee...


Niliahidi kuwaonesha mambo yalivyokuwa yakiendelea kwenye ile delectables ya Ally Remtullah, haya ndio mambo yenyewe.
...tujage mwanawani!


...dadadadeki umeona hiyo?


Pozi la ki nini hili, toa maoni!


..na pia, ..shaa alipiga shooooooo!


..heheheheheee, kisport mwanangu, very delectable!

Delectables...


Ebana dah, Jumamosi kulikuwa na ile show ya Ally Remtullah, hiki ni moja kati ya vivazi vingi vilivyoonesha, kwa mavitu zaidi, ingia humu baadae, nitakupa full mkanda mwanangu...

Wabongo tutatoka?


Jama, kuuza machungwa pia tunazuiwa, mazao yetu tukauze wapi wakati wateja mashambani hawaji, hivi, wafanyabiashara wakubwa walianzaje?

Street Dance Africa 2009


Wiki hii tulikuwa Mwwanza, katika hii Street Dance Africa ya Malta mwaka huu na hawa ndio walikuwa washindi lakini ngoma iliendaje?
...tujage mwanawani!


Ngosha The Don, ...alitumbuizaaaaa....


Mwasiti akavua pendo mbaya....


...New Edition walishindaje? Cheki...


...vijana walioneshana style mbaya katika kudance na hawa walijiita Nice boyz


...Street Kings...
Ngoma ilifanyika Villa Park

Monday, May 25, 2009

Ndio hivyo...


Shughuli imeisha waungwana, huyu Bibie kaibuka kidedea Busanda, ni mbunge wa jimbo hilo kihalali kabisa, ..anaitwaaa, Lolesia Bukwimbaaaaa.
Hamtaki?

Tuesday, May 19, 2009

Kitaani tena...


Baada ya mshike mshike kubwa ya mabomu na nini hatimaye wale waliokuwa na nyumba zenye afadhali kidogo baada ya kuathiriwa na mabomu wamerudishwa kitaani.
Pichani wakazi hao wakiwa wanashuka kutoka kwenye usafiri wa jeshiiiizzzzz...

Hehehehe, ...unaikumbuka hii?


Longtime ukiagwa darasa la saba lazima hii, kuimba shairi lazima, ambaye hakupitia hii aseme, kama huna aibu tuma maoni...

ShowLuv...


Mtoto Dully kwa shebendu mtamuweza? Hapa na Sarah wa Starehe na Bambataa ya Clouds wakishow Luv kwa mashabiki kabla ya kumalizana na kimoe Dodoma, juzi juzi hapa...

Dar Usiku


Dah, mwanangu Mwana FA kanipigia simu jana anataka kujua Dar usiku siku hizi kukoje? Nilikuwa nakatiza Kona Bar, nikatwanga pale pale bararabanyi, Oouph sore barabarani...
Ni hivi mwana!

Usafiri...


Wadau, haka ha kusafiri siku hizi kako juu sana mjue? Yaani kako sawa na gari kwa jinsi kanavyojitutumua, hebu cheki nako heti kamebeba usafiri.
...kichaa kweli kibajaji...

....wanaume kazini


Wanetu kutoka kiumeni wameanza tour ya kuizunguka Dar nzima kutangaza albam zao pamoja na ile ya mkubwa Fella ya mkubwa na wanawe, shoo inaitwa Mtaa kwa mtaa, kwa hiyo popote ulipo jijini dar es Salaam subiri...
Wanakuja!

Monday, May 18, 2009

Delectables...


Onesho kubwa la mavazi la tatu, kutoka kwa Ally Remtullah linakuja, baada ya ile Prism Break sasa anakuja na delectables, na hii ni sehemu ya usaili ya walimbwende ambao watashiriki katika kupamba onesho hili kwa kuonesha aina mmpya ya mavazi...

Mwasitiiii


Mshindi wa tuzo ya Kili ya singo bora ya R&B kwa mujibu wa tuzo za kili siku hizi anapatikana kama ukiangalia vema ratiba za Odama Band, kila ijumaa na jumamosi, huwa anapiga mahala, hebu jaribu kumfuatilia, mmoja kati ya wanadada ambao watakaa vema kwenye medani kwa kuweza kucheza vema na bendi

Friday, May 15, 2009

Aliyesema hapigi shoo nani?


Hivi, ..aliyesema Suma Leee hapigi shoo nani, si huyu? Ana ngoma mbili kachaa kitaani zinatesa, kile kitu cha reggae ya mapenzi na hiki kipya kinaitwa ndani ya wiki.
Semeni jingine!

Wednesday, May 13, 2009

Yes Massive!


Mwanetu Cosmo anafanya kumbukumbu ya kifo cha mtu mzima Bob Marley kesho pale Zhonghua Garden, atakuwepo Jhikoman na Afrikabisa Band, watakuwepo Bongo Massive na piaaaaaaa, ...Ngwair atawakilisha kizazi kipyaaaaaaaa.
Kiingilio buku nne baaab!

Tuesday, May 12, 2009

Mnamjua huyu?


Mfalme wa Moro akiwatambulisha wakazi wa Moro waliokuwepo katika ukumbi wa Mount Uluguru kwa B12, mtangazaji wa kipindi cha XXL cha Clouds FM ambaye alikuwa MC.
Ilikuwa poa sana wana...

Kaazi kweli kweli!


Ilikuwa kazi ngumu sana kumpata mshindi wa Malta Guiness Street Dance Africa wikiendi hii pale Mount Uluiguru Moro, lakini mwisho wa siku, hawa ndio waliibuka washindi.
..cheki makeke!

Ebana Dah!

Niko kitaani baada ya kupotea kwa muda wanangu, tegemeeni issues, laptop waliiba mwanawani!
Hehehehe..