Friday, January 8, 2010

Kesho, ...katikati ya gazeti la Mwananchi...


Kama uko bongo, isake nakala yako mwana...

Man X, ..huyu hapa!


Msanii mkongwe katika mziki wa kizazi kipya Alex Kushaba a.k.a Man X ameamua kujitosa rasmi katika kundi la TMK Majita original baada ya kufanya nao kazi kwa muda mrefu.
“Nimeona na vyema kujikita moja kwa moja na kundini kwani naamini kwa pamoja tutafika mbali”
Mpaka hivi sasa ameshafanya nyimbo mbili na kundi hilo na kuwa amejipanga vizuri zaidi kwa ajili ya kazi moja tu ya kutoa burudani kwa wapenzi wa muziki.
Kiongozi wa kundi hilo Eno K alisema kuwa wameamua kushirikiana na Man X kwa kuwa yeye ni mkali na ni mshikaji wao toka kitambo.
Kundi la TMK Majita Original llianzishwa miaka saba iliyopita maeneo ya keko mpaka sasa linamebaki na wasanii tofauti tofauti akiwemo Eno K, Fid, Soulder, Kindago, Jose, Kamoja, Dibwizzle pamija na Man x.

I Hate Playback, ..but...


Lawrence Malima a.k.a ‘Marlow’ kijana anayetamba na kibao kinachokwenda kwa jina la peep Peep, hatimaye ameibuka na kuutoa ukweli wake kuhusiana na sanaa anayoifanya na watu wake wa karibu ambao wanajulikana kwa jina la Mapromota.
Jamaa wanaua sanaa bwana kumbe, waziwazi kaumwaga ukweli wake bila kujali watamfanyaje baada ya makala hii kuchapishwa.
Unajua wanaiuaje sanaa?
Marlaw amesema ‘mapromota’ wanachangia kwa kiasi kikubwa kushamiri kwa PlayBack katika majukwaa ya muziki kutokana na kukwepa gharama.
Mapromota hawa, …ni mabingwa wa kukwepa gharama wanapenda kuandaa mambo kijuu juu kwa manufaa yao bila kujali aibu inayomkuta msanii.
Kwa kauli hii, Marlaw amewataja tena mapromota kuwa wanaodumaza wasanii hasa wanaopiga muziki wa Zouk, ambao mara nyingi huwa mzuri unapopigwa na vyombo jukwaani..
“Unajua Live ni gharama kubwa kuliko playback, sababu kama ni live utahitaji wapigaji na waitikiaji na vyombo. Hii imekuwa ngumu sana kwa wenzetu hawa ambao kwao, muziki ni biashara, na kikubwa anachoangalia yeye ni kufanya biashara na kupata faida. Tatizo linakuja sasa ukimwambia kuwa unataka kupiga live ukimtajia gharama anaruka viunzi, anataka ucheze playback” alisema Marlow.
Si unajua tena PlayBack? Ni wewe na CD yako na begi lako la nguo za kubadili , labda, …na mtu wa kukuitikia, kwa hiyo sana sana ni watu wawili tu.
Lakini tukianza kuongelea suala la live hapa, kuna wanamuziki ambao si chini ya kumi, kuna fundi mitambo labda, na kundi hili litahitaji kula na nini, sasa promota akiangalia umati huu anahisi hasara inakuja.
Matokeo yake sasa anaona bora uwe peke yako, lakini kwa aina hii ya muziki, tutazidi kila siku kuonekana hatufanyi muziki mzuri kama akina Mutukuzi ama Kidjo ama nani, kumbe hatujapewa ile nafasi ya kufanya muziki mzuri.
Na kwa mtindo huu ndio kila siku tutakuwa tunawasifu wanamuziki wengine wa kiafrika, kutokana na muziki wao mzuri na maendeleo waliyonayo, tukidhania kwamba hatujafikia kiwango chao, kumbe pengine tunaweza, tatizo liko kwetu wenyewe, hatulipani vizuri, hivyo thanabi ya sanaa yetu tunaidumaza wenyewe.
Marlow alisema kimsingi ni mbaya kwa wasanii wa aina kama yak wake, kuendelea kukumbatia staili hiyo ya kizamani kwani haiwezi kuwafikisha kwenye lengo wanalolitarajia. Ambapo kiukweli, kila mwanamuziki mdogo wa kitanzania kwa sasa ana ndoto ya kuwa mwanamuziki wa kimataifa.
“Mimi nachukia sana staili hiyo, inazidi kutudhalilisha sioni kama inatujenga kwani wakati sasa hauturuhusu sisi kuendelea kutumia staili hiyo” alisema Marlow.
Hata hivyo alisema haoni sababu za waandaaji hao au ‘mapromota’ kukwepa gharama kwani ndiyo wanawajenga wasanii kuweza kuashindana katika soko la kimataifa

Diamond...


Mdau kaomba nimwambia kijana mpya aliyeshine mwishoni mwa mwaka, me nimemtaja Diamond, ...kijana anatamba na kibao chake saaaafi, ...kinaitwa kamwambie, wadau wanajiuliza, ...ataweza kubaki?

Thursday, January 7, 2010

Jk, ..na Drogba


Umeuona Uzi?

...wanangu wa Taifa hawa, ndio jezi yetu...

Katutangaze...

Wednesday, January 6, 2010

Salam toka mjengoni...


Ni hivi, Clouds TV iko hewani na sura hizi zitashine mbaya hivi karibuni kutoka kushoto ni Sade, ..Sarah na Romeo...

VETO Kitaani...


Album ya mwana iko kitaani, ...buku tatu tu mkononi mwa wamachinga, ...usinunue zaidi ya buku tatu.
Ukiuziwa zaidi, piga namba...+255 716 627 344

Leo sijui imekuwaje?

Sijui hali ya hewa au nini? Lakini nimeshindwa kuupload wanangu, kila nikijaribu inachukua muda sana, net iko too slow, ...kesho jamani!

Tuesday, January 5, 2010

Kitu kipya, ..kutoka Tetemesha records...


Tetemesha Recordz inauanza mwaka 2010 kwa kumtambulisha artist wake mpya ambaye hajawahi kuskika. Anaitwa SAJNA, ni msanii mwenye miaka 18, anasoma form II hapa Mwanza. Kijana ana kipaji cha hali ya juu.
Ana wimbo, ..wimbo huu unaitwa NADHIFA, ni true story ambayo imemtokea yeye mwenyewe, kila alichokiimba katika wimbo huu ni cha kweli na kinamhusu yeye na familia yake.
Kwa ufupi amemuimba dada yake wa damu ambaye alitoweka nyumbani kwao bila taarifa miaka kadhaa iliyopita.
Wimbo umetengenezwa A2P RECORZ MWANZA, producer anaitwa SAM TIMBER.

Jacob Zuma amalizana na jiko la tano...

Mtu mzima hapa, ...inabidi aserebuke tu, ...mke wa tano sasa kudadadeki!

Bwana kakobe na harakati za kuzuia TANESCO...


Usishangae Mjomba, ...hizi ni harakati za Bwana Kakobe, katika kuhakikisha kwamba, ...hawa TANESCO, ..hawamzingui katika shughuli zake za kumtukuza bwana...

...inahuu?


...inahusu?

Monday, January 4, 2010

Jino kwa jino...


Hapa Didier Drogba, hapa Nadir Haroub, ...hii ya kimataifa sana mzee ingawa tulifungwa....

Saturday, January 2, 2010

KGT: 2010, ..ni kazi tu...


Kama haujawahi kukutana na KGT halafu ukakutana naye kwa mara ya kwanza, sidhani kama unaweza kuamini kuwa yeye ndo aliye’produce album bora ya mwaka katika tuzo za kill music awards, Cinderela ya Ali Kiba, ni kijana mwenye umbo dogo asiye na makuu.
Jina lake ni Omari Said Kombo maarufu kama KGT…. Usijiulize sana kirefu chake kwani yeye mwenyewe anasema KGT haina maana yoyote.
Ni audio producer kama walivyo kina Marco Chali, P Funk ns wengine, lakini pia wakati mwingine huikamata maiki, anamiliki nyimbo kadhaa nyumbani kwake.
Cha kushangaza nyimbo anazofanya yeye na kuimba yeye mwenyewe ‘hazipati air time’ ya kutosha lakini anazowafanyia watu ndugu yangu zinapata air time si kitoto kwakweli, baadhi ya nyimbo alizoimba ni ‘ One day’ na ‘something about you’.
Baadhi ya wasanii alipfanya nao kazi na anaoendelea kufanya nao kazi ni Ali Kiba, Pasha, Queen Darleen, Showdady, Manyota, Taqwa na Berry white ambao wengi wao amewafanyia albamu mzima.
Akizungumzia kazi anasema kuwa ni nzuri na inahitaji ‘concentration’ sana….. kuna baadhi ya wasanii ni wabishi hawataki kukubaliana na ukweli…. “ Ila nimejipanga vizuri kupambana kwenye hii ‘industry’ na naamini mwaka huu nitatoa albamu bora kama sio nyimbo bora.”

Bongo kuna wanamuziki?


MBUNGE wa jimbo la Mbinga na kiongozi wa bendi ya TOT, Kapteni John Komba amesema bongo hakuna wanamuziki bali kuna wasanii.
Anasema mwanamuziki anauwezo wa kuandika nyimbo na ikaimbwa na mwanamuziki yeyote duniani, lakini msanii ni mbabaishaji tu kama waliopo hapa bongo hawajui ‘notation’ nota za muziki.
Komba amesema mwanamuziki ni lazima ajue nota za muziki kama hajui ni msanii na kwa maana hiyo ni mbabaishaji na wanamuziki wengi wa bongo hawazijui.
“Mfano ninaweza kukwambia kuwa hule wimbo wa ‘We are the World’ uliandikwa na mwanamuziki ndiyo maana wanamuziki wengi namna hile waliimba bila kubabaika kwa sababu wanajua nota za muziki” anasema Komba.
Komba anasema anawaomba wasanii wa bongo waweze kuzisoma nota za muziki ili waweze kuwa wanamuziki wa ukweli.

Ali Kiba, kufanya kazi na Band!


NI wasanii wachache ambao wanamawazo ya kuendelea na kudumu katika fani zao au vipaji vyao katika muziki.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Ally Kiba amesema anatarajia kufungua studio pamoja na bendi yake mwaka huu wakati wowote.
Hali hiyo imekuja baada ya mwanamuziki huyo kufanya ziara za kimuziki Marekani na kujionea maendeleo ya wanamuziki na namna wanavyoishi maisha mazuri kwa kuwa na vitega uchumi vingi mbali na kutegemea muziki wao .
Akizungumza na Starehe, Ally Kiba anasema amejifunza mengi Marekani na sasa umefika wakati wa yeye kuanza kuimba nyimbo katika maonyesho live kwa kutumia bendi yake ambayo ataizindua muda si mrefu mwaka huu.
“Lengo langu nikutaka kuweza kumiliki bendi yangu lakini naona mipango yangu hiyo inakwenda vizuri na mwaka huu itaanza” anasema Kiba na kuongeza
“Mbali na bendi pia na studio ya kurekodia muziki nayo iko mbioni kukamilika, lengo ni kuweza kujiongezea kipato zaidi kwa kutumia vyanzo mbalimbali”.

Friday, January 1, 2010

Kesho katika Mwananchi...


Usikose kulitafuta mtaani kama uko Afrika ya Mashariki...

It's on...


Maisha Plus Season II iko hewani, ..watu wameingia kijijini jana, na hawa ni baadhi yao, ...stay tuned, ..only on TBC1

Kuna watu, ..na viatu


Unawachukuliaje watu? Nyota ndogo aliwahi kuimba kwamba suniani kuna watu, ...na viatu, mimi

nina mtazamo, some..

Kaka na dada zangu, siku imefika na mambo yanaendelea, tubadilishane mawazo kidogo, ...kuhusiana na maisha yetu ya kila siku.
Ahsanteni kwa maoni ya wiki iliyopita, nashkuru sana kuona kwamba kumbe mnanielewa zaidi, hii kwangu ni kama faraja na kiukweli, imenifurahisha sana. Iwe hivi basi ambapo pia nitakosea ili mwisho wa siku makala hii iwe na faida kwenu na jamii kwa ujumla, si ndio jamani?
Leo nataka kuongea na watu kuhusiana na watu.
Mnanielewa?
Kuhusiana na hawa wenzetu tunaoishi nao humu mitaani, majumbani, makazini humu tunao, ....watu jamani nyie mnawachukuliaje? Wana nafasi gani katika maisha yako?
Ungekuwa umeniuliza mimi ningekuwa na haya ya kusema:

Ni muhimu sana...
Fikiria dunia bila watu, ...ingekuwaje? We ungekuwa nani kwanza, bila shaka unajivunia utu wako, so ndio ndugu yangu? Na kwa kweli watu ndio wamesaidia wewe kuwepo hapo ulipo kwa sababu umelelewa na watu, kama unatembea na gari basi limebuniwa na watu, na kama unafanya kazi umeajiriwa na watu au mtu, yaani kila kitu ni watu, kwa hiyo kila itakavyokuwa katika haya maisha yetu ya kila siku, ..bila watu, ..dunia si kitu.
Unanielewa sasa.
Na labda nikuongezee kumbuka waalimu wako, kumbuka wazazi wako, ..kumbuka rafiki zako, kumbuka madaktari, kumbuka wanausalama, na kumbuka viongozi wa nchi.
Watu ni muhimu sana kiukweli katika maisha yetu ya kila siku, lakini...
Watu ndio chanzo cha kila tatizo lako!
Hili nalo pia tunapaswa kuliona, ukiona uzuri sio mbaya ukaona na ubaya wa kitu ili uweze kukabiliana nacho au kuishi katika hicho, kama tunaishi na watu basi watu ndio maisha yetu.
Kiukweli hatuwezi kuishi bila watu waliotuizunguka, si mnanielewa ninachokiongelea?
Lakini, hebu fikiria, uliyegombana naye juzi ni nani? Ni mtu, kibaka aliyekupora juzi ni mtu pia, na
aliyepeleka habari mbaya kwa wakuu wako wa kazi mpaka ukapewa onyo ni mtu na aliyekusema vibaya kiasi cha wewe kushuka heshima yako kwa jamii ni mtu pia, sijui jamani kama tunaenda pamoja?
Sasa hapa nilikuwa najaribu kukuelewesha kingine, hawa watu pia ni matatizo. Unanielewa bwana, hatuwezi kuishi bila watu lakini pia tunaweza kuwa na maangalizo, sasa maangalizo kama yapi?
...hebu tuendelee...

Usiwachukulie poa...
Nisikilize mimi, sio kila anayekuwa karibu yako anakupennda, kumkaribisha mtu karibu zaidi ndio kumjulisha silaha za kukuangamiza atakapoamua. kaka na dada zangu dunia imeharibika, kuaminiana, kupo lakini sio kwa asilimia kubwa, watu wamekuwa wabaya. Anayekusifia leo, kesho ndiye atakayekuwa mstari wa mbele kukuponda, kwa hiyo kuna kila sababu ya kuwa makini na watu.
Maadui zetu ni watu pia, kwa hiyo uangalifu hapa ndio jambo la msingi.
Kwangu mimi naona ni bora adui atakayekuja kugeuka na kuwa rafiki yangu kuliko rafiki atakayegeuka kuwa adui yangu.
...huyu ni hatari zaidi kwani anajua kabisa juu ya kuniangamiza, anajua pa kuanzia, na jinsi atakavyonimaliza.
Narudia tena kwa kumalizia kwamba watu, ...ni wa kuwaangalia sana kaka na dada zangu, ningeweza kuliongelea hili kwa upana zaidi lakini sina nafasi kubwa katika hili, naomba kuishia hapa ila mawasiliano si yapo?
...tutumiane ujumbe
Henry Mdimu ni mhariri wa burudani wa magazeti ya Mwananchi, anapatikana kwa simu:
+255 787 000 880
Na Barua Pepe:
Mdimu@hotmail.com

Zee la Nyeti wiki hii...


Acheni ukavu, ..toeni mashavu...

....dadadadeki..
Mwaka wa tabu uleeeee....
Big Up wanangu wote wa kitaa, tumesavaivu, ...ingawa mwaka dizaini kama ulikuwa sio hivi, watu walipigika ile ile, ..kila dili lilibuma mpaka ikafikia taimu watu wanaona, ...bore wakimbie mji, lakini mabontauni tukakomaa, mpaka mwaka umeisha na hakuna aliyeona diferensi, uongo mwanangu?
Big Up kwa wanangu wote waliokomaa kama mimi, kwenye Bata tulikuwemo, kwenye mitikasi kama kawa japo ilikuwa inabuma lakini hatukuwahi kuogopa ishu, ukija mchongo watu walikuwa wanapiga tu, matokeo mbele kwa mbele, ubume, uwe poa, ..kesho yake tu unakuta watu kitaani kama kawa, na Bata ni kuanzia Jumatatu mpaka Jumatatu.
Unabishaaa?
Haina kulaumu kudadadeki, kama uliharibu mwanzoni unafikiri ishu zitajimeki mwishoni kimiujiza? ..haina tangu mwanzo unatakiwa kujipanga fresh mwana, kweli mwaka ulizingua lakini mbona kuna ambao walikuwa poa tu? Nawashtua wana sasa, mwaka umeanza,..kama kkuna muda wa kujipanga ndio huu.
Usije kulaumu mida mida...
Mipango sio matumizi kajisemea mtu mzima Kingwendu Ngwendulile...
Si uliisikia ile ngoma yake kipindi kile, ...ilikuwa ina maana zake, na maana zenyewe ndio kama hizi.
Juzi nilikuwa na Deiwaka mwenzangu Sugu tunatathmini ishu mbiuili tatu za mwaka wa tabu tukashtukia kwamba wana wengi walibugi na waliokuwa kwenye chaneli hawakupiga ishu za maana kutokana na nini, waliokuwa wamewazunguka wengi kilikuwa hakijaeleweka, watu wakabaki kuonbeshana lav na nini, ..mambo ya msingi wakayapotezea.
Halafu dizaini, wana hawajashtuka hivi, wale waliokuwa kwenye chaneli bado wengine walikuwa wanammaindi kuwapa sapoti mademu zao, wanawaacha machizi wanapigika, wako kama hawajashtukia hivi kwamba ukiwezesha machizi, ni kama unaendeleza nchi hivi, machizi wanainvesti humu humu, mi leo ngoja kuna watu niwachane, wakimaindi kivyao au sio?
Mwaka huu japo ulikuwa wa tabu lakini, dizaini machizi tuliokuwa tunahangaika faa beki wote angalau watu wamepewa vioitengo nini, wanakamatia mfano mdogo mwanenu nimekabidhiwa kitengo cha Burudani na muziki hapa MCL, Ojuku Abraham, mhariri wa Bingwa, umeona? Mwanetu Jack Mbando katulia Tigo, Shyrose na Morris Njowoka wako NMB, Suka kala kitengo cha Muziki Clouds FM, na Seba Maganga ndio mkuu wa vipindi...
Kimsingi siwezi kuwattaja wote lakini dizaini mnaelewa kwamba wana, ambao tulikuwa tunakula Bata tangu enzi za pulsaidi, mpaka leo tunaegzisti, halafu tumekalia vitengo, unakubali?
Hii inatokana na ubishi na uwezo wa hivi vichwa, lakini tatizo liko moja, wanetu wa kitaa tunawasaidiaje? Watu tumekalia vitengo, halafu wana bado wanafanyishwa shoo za kilo tano, wakija wanaijeria tunawapa doola buku stini, ..haukamz?
Wana wanataka kutoka ikitaani wafanye mabiznes na nini, mnawapa shavu? Mikopo hii vipi akina Abdallah huko Stanbiki?
Siwachani kwamba muwapendelee wana kwa sababu ni wana, ila kiukweli, kitaa kuna vichwa ambavyo vikiwezeshwa hata sura na nchi itabadilika, utashangaa wana ndio wanakuwa mainvesta siku za mbeleni, unabisha?
Mashavu muhimu kupeana, kama uwezo upo, ila ndio hivyo, wana wanawaangalia watu wao, machizi wanaona poa kuwasapoti mademu zao hata kama hawana ishu za maana huku machizi wenye aidia za msingi wanapigika kitaani.
...sio mzuka wala nini....
Nimewamaindi!
Au dizaini mwana anataka umpige tafu unamwambia akupe mkwanja labda hivi, we mkwanja atakaokupa mwanao ambaye mnamingo wote kitaa utakusaidia nini? Mpe fadhila uone, ..samtaimz poa tu kupunguza hii mizinga ya buku tano tano, mpaka mwekundu hivi, tuwawezeshe wenzetu jama, au sio?
Najua hamjanimaindi.
Hepiniuyia....;

Heri ya mwaka mpya


Mimi na timu yangu nzima ya Starehe Magazine, tunawatakia wasomaji wetu heri ya mwaka mpya, ...kwa heri mwaka wa tabu...