Tuesday, September 25, 2007

...Mudhihir...


...hatimaye Mudhihir anaonekana kama aliyemaliza tiba, hapa akitoka katika Hospitali ya Muhimbili ambako alilazwa kwa matibabu kwa siku kadhaa, tumuombee apone haraka, na kuendelea kulitumikia jimbo lake la Mchinga...

..keshawasili...


Mheshimiwa Juma Kapuya ambaye jana aliripotiwa kupata ajali huko Tabora ambapo watu watatu waliokuwamo kwenye gari lake walipoteza maisha, akishushwa kutoka kwenye Ndege baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam kwa matibabu zaidi, ambapo kwa sasa amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Sea Cliff...


Kuna mdau haamini kwamba Sea Cliff imefanza, kaniomba kuiona kutoka machoni pangu, naomba nichukue wasaa huu kumwambia, ni hivi...

Kapuya hoi!


Habari nilizonazo ni kwamba, profesa Juma kapuya amepata ajali akiwa katika msafara wake, na ameumia bega la kushoto na kifua, ....huyu ni kiongozi wa pili katika Serikali kupata ajali ndani ya wiki mbili, Mheshimiwa Mudhihir, Mbunge wa Mchinga, naye kakatwa mkono...

Monday, September 24, 2007

Dongo jingine kwa TID


Kufuatia kutangazwa rasmi kujitoa kwa Mwanamuziki Aboubakar Shaaban Katwila katika Bendi inayomilikiwa na Khaleed Mohamed, a.k.a Top In Dar, a.k.a TID, ...nimeruhusiwa kuwarushia wadau wa ughaibuni kipondo hiki ambacho kimechorwa na Msanii Supadeo
...enjoy..

Saturday, September 22, 2007

Mastaa wetu...


Mastaa kibao walikuwepo kwenye MTV Veejay Party, si unaona mwenyewe, Mtu mzima Fid, Mwana FA na wengine kibao walijivinjari, Bongo tamu kudadadeki...

MTV Veejay wa Bongo!


Shindano la MTV Veejay limefika ukingoni wanangu na huyu mdada kushoto anayeitwa Vanessa kutoka Arusha ndio kala shavu hilo, na ataaza kuonekana kwenye macho ya watu huko mbele kuanzia mwishoni mwa mwezi huu, tulikula raha kweli Club Maisha jana, ...nakuletea picha zaidi watu wazima tulivyojiachia Ki VIP...

Boyfriend & Girlfriend

Hivi, unajituma au unataka kutumikiwa?

Jamani imefika ile jumamosi ambayo kuna watu wengi wananiambia kwamba huwa wanaisubiri sana, eti waangalie nimesema nini leo? Jamani hivi mnajua kwamba sasa hivi nakuwa napata wakati mgumu sana ninapofikiria kufanya jambo? na hii ni kwa sababu kuna watu wengi makini wananisoma kwa sasa.
Shukrani za dhati kwa wasomaji wangu wa Arusha, ..tulikutana bwana tukajadili mengi tu na tulifurahi kwa kweli kuonana, wengi walishani watakutana na jibaaaaba hilo, kumbe kakijana tu lakini wengi wameniombea, kila mtu kwa imani yake kwamba Mungu anijaalie busara zaidi, maana ninayosema huwa hayalingani na umbo langu na miaka niliyonayo, eti wanadai naongea maneno ya kijana mwenye umri wa miaka 40, ...jamani!
Tuendelee na ya leo maana hizi sifa nikianza kuzielezea wala haziishi, ...kaka na dada zangu, nimesukumwa kuandika haya ninayoandika leo, kuna watu wananiandikia malalamiko kila kukicha. lawama kwa wapenzi wao wakidai kwamba hawaoni kama wanapendwa, yaani wenzi wao hao hawajitumi kabisa katika mapenzi, lakini kuna jibu nikawaandikia, ambalo liliwafanya wanyamaze, unajua niliwauliza nini?
Sawa hao wenzenu hawajitumi, na nyie wenyewe, mmeonesha jitihada gani kuwaweka karibu, ama mnataka kutumikiwa? Kwani jamani mapenzi ni kupenda ama kupendana? Maana wewe unasema huoni dalili kutoka kwa mwenzako, wewe zako ulionesha zikawekwa benchi? sasa kuna utaratibu wa kuangalia katika haya mapenzi, hasa kwa wale ambao walifuatwa, na sio wao kufuata, mnatakaiwa kujua mambo flani ambayo nitawawekea katika vipengele. Tupo p amoja jamani? ..me naanza:

1.Mapenzi na kuamua!
Hili ni jambo ambalo wengi wa vijana waliokuwemo katika uhusiano mlikuwa hamjalifahanu basi habari ndiyo hiyo. mapenzi ya kutegeana yamepitwa na wakati na ni kujidhulumu na mwisho wa siku utajikuta huridhiki na kila unayemuona maana utagundua kwamba labda hakuopendi kumbe wenyewe mnategeana na mwisho wa siku mnajikuta mnahisiana vibaya baada ya kila mtu kutegea kumuona mwenzake akiwa kajitoa kwa mwenzake.
Kama umeshaamua kwamba wewe uko na fulani haina kutegea kaka ama dada yangu. Umeamua kupenda, penda moja kwa moja, na hatua ya kwanza katika hili ni kufukia mashimo. Uliza kivipi? Unapoona anakosea rekebisha, unapohisi hupendi mambo fulani, ambayo mwenzako anayafanya, mwambie ukweli, na kwa kuwa yeye anakupenda anajirekebisha, wazungu wanasema, 'Love makes things happen', na mimi nawaunga mkono, nimeshuhudia watu wakiacha pombe, wakiacha sigara, wakiacha hata umbea kwa sababu ya mapenzi.
Lakini ukitega, kila mtu utamuona ana tabia mbaya, na kumbe tabia mbaya unayo wewe. na kibaya zaidi sasa, unajikuta umeachana na huyu, umeanza na huyu, ukaenda kwa huyu na huyu na yule na mwisho wa siku umefanya msuruuuru wa watu katika uhusiano wako wa kimapenzi. Na dunia si unaijua ilivyofunyangwa na teknolojia. Ndio yaleeee, unaingia mahala unakuta katika watu kumi, wanne umeshakaa nao mkao wa kimapenzi? Heshima ipo hao?
Unajinyima mwenyewe uhuru wa nafsi unakuwa, au nadanganya? ...semeni...

2. mapenzi huambatana na amani ya moyo?
Ndio maana hapo mwanzoni nikawaambia kwamba ukiamua kufanya uhusiano amua tu moja kwa moja maana uhusiano wa kuchungulia chungulia unakuwa kama hujiamini hivi, unakuwa na moyo wa kusita sita, kuliko kufanya hivi ni bora kuacha kaka au dada yangu maana hutafurahia, utakuwa kama unajinyima haki yako ya msingi.
Sasa mambo ya kukaa kama bosi na kusubiri mwenzako ahangaike ndio nini. Na yeye kwa kukuona hivyo unataka kusujudiwa unadhani atakubali kufanywa mjinga, na yeye huenda akawa na mtu anamnyenyekea, atahisi kwamba kwako hamna mapenzi. Kumbe yawezekana yamo, ila sasa tatizo ni kwamba, unasikilizia kwamba kama kweli lipo, ...ndio unakuta muda unakwenda, mmoja ataona anayeyushwa, mara uhusiano unabomoka, ...kila mtu kivyake!
Unatakiwa kabla ya kumwambia mtu I love you too, umehakikisha kabisa kutoka moyoni mwako kama umeamua na moyo ukiamua kupenda unakuwa na amani na ule uhusiano ambao unauanza. Unaona bwana na ukipata baraka kutoka moyoni mwako, penzi la namna hii hudumu asikudanganye mtu na ukihisi moyo unasita, achana na huo uhusiano, utakupotezea muda bila mwenyewe kujijua, na kama huniamini jaribu, ..haufiki popote uhusiano wa namna hii.

3.Nyie tu na mambo yenu
Kuna kosa kubwa ambalo vijana hulifanya pindi wanapokuwa katika husiano zao. Hupenda sana mambo mawili, moja ni kupenda sana kushirikisha rafiki zao katika husiano zao, yaani kuanzia kwenye maamuzi ama katika jambo ambalo wenyewe huliita ushauri kumbe wanakuwa wanauza silaha za maisha yao. Kikulacho ki nguoni mwako kama ulikuwa hujui, ..we una uhakika gani huyo unayemuomba ushauri anafurahia maisha yako na mpenzio?
Hili ni moja jingina bwana, ni lile la kulinganisha mambo, kwamba mbona flani anafanyiwa hiki mi sifanyiwi? Maisha ni kama vidole mikononi mwako, hayawezi kulingana, kuna aina ya maisha ambayo Mungu amekupangia, unatakiwa kukubali hali uliyonayo na kuirekebisha kwa zana ambazo ziko ndani ya uwezo wako, unaona bwana? ukilazimisha tu unakuwa umeharibu kila kitu.
Nomba niwashauri kitu kaka na dada zangu, rafiki yako mkubwa awe mpenzi wako, kama kweli unampenda, yeye ndio mshirikishe kwenye mambo yako na mwisho wa siku utakuja kuona, kila kitu kitanyooka, unajua hii itatoka wapi? ...katika kuhakikisha kwamba mnaridhiana.
Umri unaenda mbele ndugu zangu, hili nawaambia kila siku, mnafikiri bado tuna muda wa kupoteza vijana wenzangu? Mangapi yanatusubiri kwa ajili ya maisha yetu ya baadae?
Naomba niishie hapa kwa leo ndugu zangu, nina imani somo mmelipata na kama mna la zaidi la kuniambia, naomba mniandikie kule kwenye:
HMdimu@Mwananchi.co.tz
+255 787 000 880
Wiki ijayo, ...nipo hapa hapa, ..msikose.

Hili hapa...


Toleo la kijarida ambacho nakiendesha hapa Mwananchi wiki hii kiko hivi, kuna wadau wanafurahia kuona ukurasa wa mbele. Wiki hii tuna huyu kijana ambaye ana kasongi kake ka Mpenzi jini ambaye kwa mujibu wa wachambuaji wa mambo ya watu ni kwamba, ....kajamaa kanauza kweli!

Full kujiachia...


Weekend hii bwana., watu wanajiachia, hawa ni wadau wa muziki wa kizazi kipya bwana, watoto wa TNG, wakiwa na Joh Makini, kushoto kabisa. B12 wa nne kutoka kushoto, na kisha Lord Eyes wa nako2Nako na mwisho kabisa mtoto anaitwa Makamua, ana traki lake linaitwa Why kwa sasa amempa shavu mtu mzima ChidBeeeeenz!

Thursday, September 20, 2007

Watoto wa Msimbazi!


Ligi ya Vodaco iko karibu kutimua vumbi, hawa ni wana wa Msimbazi wanapasha mwanawane wanasubiri lapa la Jangwani wavaane nalo, sijui historia itakuwa kama kawaida?
...me sijasema!

Taifa Mademu


Ujue tumehamasika sana huku Bongo kuhusiana na suala la soka? Mademu zetu nao tunataka wafikie kiwango, unaona bwana, anza na kuwacheki kwa picha, kisha kwenye wanja tunamalizia, ..kudadadeki!

Wednesday, September 19, 2007

Hapo VP?


Wazee... hii mnafikiri ni nini? Kilimanjaro Kempiski bwana, sasa Ulaya nikafuate nini jamani kujiachia hapa kuna tofauti gani na London? Msinitanie bwana...

Life Oooh life...


Mnaona, ..kijana amekamatwa katikati ya Jiji la dar kwa kosa la kuuza kinywaji baridi, ikiwa ni sehemu ya kutafuta jinsi ya kujikimu na maisha, ...nina imani na wahujumu wa mali za sirikali nao siku moja watakamatwa kwa staili hii hii.
...tuombe Mungu!

Mjeda mpya!


Huyu ndio Mkuu mpya wa jeshi letu jamani anaitwa davis Mwamunyange, mlioko mtoni mmenisoma?

Waitara kaaga!


Jamani george Waitara kamaliza muda wake kwa wale waliokuwa hawajui siku hizi jeshini tua Mwamunyange? sawa? ...asenti!

Tuesday, September 18, 2007

Majibu kutoka kwa Dingi!


Bwana Wilbroad Slaa kutoka Chadema, ameshusha tuhuma nzito kuhusiana na viongozi a Serikali kuhujumu sirikali, Mzee Kingunge kafungua mdomo jana, kasema kwamba atalishughulikia hili, kwa mtindo gani? ....kaa tayari ntakuletea

Naota...


Mwanangu, ndio nimeshuka kwenye hiki Kitu, nikaomba nile snepu moja kwanza nione kama napendeza? Toeni maoni, nataka kumiliki kitu kama hiki ifikapo 2012, Mungu ajaliapo uhai...

Jobu kwa Ben


Si mlisikia kwamba kaka jakaya alimpa kazi ya ukuu wa chuo kaka Ben Mkapa? Kwa mtakaokuwa mnataka kujua mandhari ya kazini kwake, ndio hapa, ...mnakaribishwa kuja kupiga buku!

Mafundi..


Watoto wa kibongo kwa machejo, ...nani anawaweza? Hapa wamenaswa wakikorokochoa mchuma wa mtu, unawatabirije miaka kumi ijayo?

Majaji...


hawa ndio majaji wa BSS, kutoka kushoto ni Mkurugenzi mwenyewe Ritha Paulsen, wa pili si mnamjua Bi Mkubwa? Salama Jabir na kulia kabisa ni bwana Joachim, wenyewe mnamjua kwa jina la Master Jay, hapa ndio wanaingia kazini jijini Arusha, mnanisoma?

Saturday, September 15, 2007

Boyfriend & Girlfriend

Penzi la kuibia tamu? Nani kakwambia?

Jamani, duniani kuna mambo, haya, na tuanze kwa kumshukuru Mungu kwa kuweza kuturuhusu tukutane tena Jumamosi hii na kuchukua muda wetu mchache kuongea angalau kwa uchache kuhusiana na suala zima la mahaba, mimi mzima, hofu na mashaka ni juu yenu nyie mlio mbali na upeo wa macho yangu. Ila nina imani mmesalimika!
Leo nina mada ambayo nilikuwa nimekaa kijiweni Ijumaa iliyopita, nikawakuta watu wazima na akili zao wanaijadili huku wakiipa sifa kweli hali ya penzi la kuibia, kwamba lina utamu uliopitiliza, nilipobisha, nikaambiwa usisikie, usiombe ukajaribu, unaweza ukagombea kuwa mwenyekiti wa chama cha wezi wa wake za watu!..nikaondokamahala pale maana nikahisi ningesikiliza sana ningeshawishika, ..mjue ni dhambi halafu madhara yako bayana,
Unaona bwana, sasa katika tafakuri yangu kuna mambonimeyagundua, kwa asiye naakili timamu anaweza akasema kwamba kuna faida nyingi atapata ambazo nitazisema kwa mafungu kama kawaida yangu na nitaongelea asthari katika kipengele cha mwisho kabisa.

1. Halina gharama!
Unaona bwana, watu wengi ambao ni wezi wa wake za watu hulifurahia penzi la wizi kwa kuwa hutunziwa hawa wanawake, yaani mwenye mke anapendezesha, amalisha na kila kitu, yeye kazi yake inakuwani kufurahia penzi tu ambalo halionei uchungu kwa hiyo yeye anakuwa anafaidi zaidi kuliko mwenye mali.
Kama anaingia gharama utakuta ni ya simu ya kumpigia, au kama wanakutana mahala mamb ya chakula na malazi kama wataamua kulala jambo ambalo ni sawa na hakuna kuliko ambavyo kama angekuwa na mtu ambaye labda angekuwa anamhudumia.
Hii ni mojawapo ya raha ambayo wezi wa wake za watu wanaifurahia na ni sababu ya msingi kiasi fulani inayopelekeawao kusema ni kwa nini penzi la kuiba ni tamu...

2. Penzi moto!
Kuna ujinga ambao naamini kabisa kuna wanandoampaka leo wanaufanya, nao ni kujifanya wana heshima saaaana baina yao, hata katika masuala ya mapenzi. Kifupi hawako wazi, wanakuwa wanakificha kile ambacho wanakipenda sana wanapokuwa mahabani, matokeo yake utakuta mtu tangu anaingia kwenye ndoa, mpaka anapata watoto, anakuwa hafurahii kabisa mahaba na mumewe.
Sasa ndio usiombe akaja akakutana na huyu mwizi ambaye atataka kuonesha maujuzi yake ili amteke mwenzako kiakili, ....utajuta!
Mara nyingi mapenzi ya namna hii ya kuiba watu huwa huru kufanyiana kila upuuzi unaohusianan a mapenzi, na hapa ndio utamu unapoanzia. Kingine penzi moto litakuja pale ambapo mtu anaudhiwa huko nyumbani, wanakuwa wanalala 'Mzungu wa nne', huyu ndio huko anakoiba ama kuibiwa anamalizia usongo wote!
....pata picha mwenyewe!

3. Haina kero..yaani shwari tu!
Unajua kuna jambo moja baina yetu wanadamu, mpaka watu mgombane, lazima mtakuwa kwa kiasi fulani mezoeana, sasa hawa wanaoibana mara nyingi huwa wanapatana sana maana muda wa kukaa na kuanza kusomana huwa hawana, hawa mara nyingi wakikutana wanakuwa na kazi moja tu, mahaba moto moto kisha wakimaliza kila mtu anaishia kivyake.
Tofauti na wenye husiano za kudumu, kunakuwa na migogoro iliyoongozana. Kila mara wanakuwa wanagombana na hii mara nyingi inakuwa ni kero baina yao. Na hii ni sababu mojawapo wezi wa mapenzi wanakuwa wanaamini kwamba ni bora penzi la kuibia, kuliko kuwa na uhusiano na mtu.
Maana kingine ni kwamba si unajijua ni mwizi? Kwa hiyo hata kuchunga sana unakuwa huna haja, mwenye mke si atakuwa analindakwa niaba? Sasa wewe presha za nini?
Mimi kwa leo naona niishie hapa, wiki ijayo ndio nitakupa madhara ya kuibia penzi, lakini kama una maoni tuma ujumbe kwenye namba +255 787 000 880 uniambie au kwa email:
Mdimu@hotmail.com

ShowLove!


Huyu Binti alikuwa kama shabiki wa Kala Jewremiah wakati anafanya ubishi ndani ya BongoStarSearch ya mwaka jana, tumekutana naye mitaa ya sokoni akaomba snepu nz kijana, ..sasa tumnyimie nini?

Kala amekula!


Unamkumbuka huyu jamaa? Anaitwa Kala Jeremiah, alikuwammoja kati ya washirikiwa Bongo Star Search mwaka jana,akashika nafasi kama ya nne hv, ..mwaka huu amek\kula shavu lautangazaji kwenye hiiTour ya kusaka vipaji ambayo wiki iliyopita ilikuwa Zanzibar, na leo mambo yanaendelea pale Blue Tripple A, ...kuna nyomi...

Safari imeanza!


Kazi ya kumsaka Staa mwingine wa kuimba bongo imeanza, imepachikwa jina la Bongo Star Search, hii ni Arusha jamani ndani ya ukumbi wa Blue Tripple A leo asubuhi, kazi ya kuwaangalia hawa vijana inaendelea mpaka kesho...

Monday, September 3, 2007

..tutafanyaje sasa?


..imebidi kuingia gharama za ziada kukarabati, ..roho inauma anyway, na Jumamosi tunapandisha bei, kudadadeki!

jamani!


Huu ndio wema wa wabongo baada ya kutengenezewa bonge la wanja, ...wameuharibu bwana, si unauona ule mstari usio na viti, mstari wa tatu kuanzia kushoto viti vya buluu, ...wamekwiba!

Sunday, September 2, 2007

Jamani Doooooktaaaa!


hahahaaaa, jamani sasa, ...umefika muda na sisi tuoe, si mnamjua Dokta Cheni wa Kaole? Jamaa kach'kua mzigo bwana. Kwanza alianza kama anaigiza naye muvi halafu akachukua jumla. kuna jingine? Kama mnabisha si huyu?

Anashika hapa kudadadeki...heeeehe!


Umeona jinsi tulivyowatawala kisoka mpaka wanashika? Si unawaona? basi mimi baada ya hapa nilitoka nikaenda Miss Tanzania, bao lilifungwa Abdi Kassim, bora tumeubikiri wenyewe uwanja, ...wangetufunga ingekuwa aibu!

Saturday, September 1, 2007

Kosi letu


Hili ndio kosi letu ambalo jana lilimchapa Cranes kimoja tu, ...sio sana hicho tu

Kama Wembley kudadadeki!


Unacheki wanja lilivyokuwa limetulia, kuna tofauti gani na mawanja ya mamtoni sasa? Tuache tu tubaki hapa Bongo!

Mapemaaaaaaa


Unafikiri tulitaka makuu, mechi ilianza saa moja, na hivi wanja lenyewe jipya, ..tukaamua kujitoma mapemaaaaaa

Mbwembwe!


Jana tulikipiga na Uganda, uzalendo ulianzia mchana, mambo yalikuwa hivi mtaani...

Balozi wa Redds


dada yetu Victoria Martin kala shavu la Balozi wa redds, kama ulikuwa hujui huyu ndio Miss Tanga ambaye pia ana taji la kanda ya Kaskazini. Mrithi wa Jokate bwana...

Shavu


Hapa Miss wetu anakula shavu na Miss World wa miaka ileee, ambaye alikuwa jaji, si mnamkumbuka Agbani Darego? sasa nini mnataka kutajiwa na miaka na nini...snepu hilo kama vipi ch'kueni

Na huyu ndio....


Richa Adhia, aliyewahi kutuwakilisha kwenye Miss Earth kipindi flani kala shavu jingine, ..ndio Miss Tanzania wetu, hata kama mlisema mdosi kudadadeki, watu wameamua!

Mzee Kawawa ndani!


Tulikuwa na Simba wa vita leaders Club ambaye aliona bolu sio issue, tukajimiksi naye kwenye Miss Tanzania akiwa na Mai wafu wake!
..si umecheki pozi?

Majaji


hawa ndio walioifanya kazi ya kuwachuja mabinti waliongozwa na Agbani Darego kushoto kabisa, hawa wengine si mnawajua jamani? Taabu za nini sasa?

Top Five


Hawa ndio waliikamata ile tano bora mwanangu, kilikuwa kimbembe mwaka huu, ...we acha tu!

Miss Tanzania


Jana ilikuwa kazi hapa kumtamuta kimwana wa Tanzania, na hawa ndio washiriki walipendeza, ...tujage tuone tukio lilivyokuwa