Friday, August 13, 2010

Nimefufuka!

Baada ya zain kuleta mfumo mpya nimepata unafuu jamani, haya niko heani tena!

Monday, March 1, 2010

Kamuzi la Bi Kidude Travertine jana...


"Sasa ndio mtaona tofauti ya taarab, na mipasho..."

Acha masikhara wewe, ...twende kazini...

Mfalme na Malkia, wakatambulishana jukwaani!

...likafuata kamuzi la maana, mijihela si unaiona?

Wednesday, February 24, 2010

Dah Manara...


Bado ngoma ngumu kwa aliyekuwa Katibu mwenezi wa Chama cha Mapinduzi, Haji Manara, baada ya kufanikiwa kupata dhamana jana, akakamatwa tena pale pale, ..hivi karudi tena rumande.
...kaaazi kweli kweli

Yanauzwa wapi na mi nikauze, nshachoka mie!


Kila nnayemuona town kabeba hili zigo mgongoni, wapi mnauza?

Tuesday, February 23, 2010

Isha mashauzi alivyozindua...


Nyomi hili bila shaka litakuthibitishia kwamba uzinduzi wa albam ya Mwanadada Aisha Ramadhani, a.k.k.k.k.a Isha Mashauzi, a.k.a Mamaa Mashetani inayokwenda kwa jina la Mama na Mwana ulifana, kundi zima la Jahazi lilimsindikiza, kama unataka kuziona kashda zaidi, ...shula ujionee, mimi nilikuwepo...

..shughuli muongozaji babu, ..aku!

..mashauzi yalitawala kama jina la mwimbaji mwenyewe...

Sanduku lilitangulia, mwenyewe je? ...tujage...

Full kjishaua mabegani, mwanamke hulka babu...

Mnh, ..hapa sijui alizimia?

..alipoibuka chacha, ..weweeeee!

Mfalme mwenyewe alikuwepo kusapoti mzigo...

Thursday, February 18, 2010

It's Kili time...


george Kavishe ambaye ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro na Katibnu mkuu wa Baraza la sanaa wakizindua rasmi tuzo za Kili Msimu huu wa 2009/2010. Mengi yameongelewa na kuna ahadi ya kwamba tuzo za mwaka huu zitaboreshwa zaidi...
...tungoje tuone

AY akimnong'oneza kitu, mkuu mpya wa Baraza la sanaa, Gonche Materego

George Kavishe akishikana mkono na Lady Jay Dee, kama ishara ya muungano mpya kati ya wasanii na Kilimanjaro Music Awards

George Kavighe, AY, Nyoshi na Mzee Yusuph wakishow luv mbele ya nembo ya tuzo ya Kili kwa mwaka huu...

TID na Dada jide ndio walitoka kistaa zaidi...

Friday, February 12, 2010

Fresh Jumbe nae...



Kiupi mambo yameanza cha kushangaza ndugu zatu akina ChidBenz, na Tundaman ambao kwenye matangazo ya awali tuliwaona, hawamo kwenye ratiba, ni kweli wamekimbia live perfomance?

Da'Kidude bado Fit


Weweiyaaaa, hapa ndio ile, ..Aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!

Tangu jana mtiti umeanza na Bi Kidude kama kawaida, ...akakamua!

Thursday, February 11, 2010

Busara 2010, pamoja tunasababisha...


Yusuph Mahmoud Director wa Busara Promotions akizindua rasmi ndani ya Ngome Kongwe...

Mbwembwe za uzinduzi mtaani zikawa hivi!

Ebwana daaaaah....

...hizi ni utangulizi tu, za usiku wa leo, angalia asubuhi na mapema, ...ntakuwa hewani!

Papic...


Mtu mzima Clinton, leo kawasilisha vielelezo vya kuwania u'Maximo

Friday, January 8, 2010

Kesho, ...katikati ya gazeti la Mwananchi...


Kama uko bongo, isake nakala yako mwana...

Man X, ..huyu hapa!


Msanii mkongwe katika mziki wa kizazi kipya Alex Kushaba a.k.a Man X ameamua kujitosa rasmi katika kundi la TMK Majita original baada ya kufanya nao kazi kwa muda mrefu.
“Nimeona na vyema kujikita moja kwa moja na kundini kwani naamini kwa pamoja tutafika mbali”
Mpaka hivi sasa ameshafanya nyimbo mbili na kundi hilo na kuwa amejipanga vizuri zaidi kwa ajili ya kazi moja tu ya kutoa burudani kwa wapenzi wa muziki.
Kiongozi wa kundi hilo Eno K alisema kuwa wameamua kushirikiana na Man X kwa kuwa yeye ni mkali na ni mshikaji wao toka kitambo.
Kundi la TMK Majita Original llianzishwa miaka saba iliyopita maeneo ya keko mpaka sasa linamebaki na wasanii tofauti tofauti akiwemo Eno K, Fid, Soulder, Kindago, Jose, Kamoja, Dibwizzle pamija na Man x.

I Hate Playback, ..but...


Lawrence Malima a.k.a ‘Marlow’ kijana anayetamba na kibao kinachokwenda kwa jina la peep Peep, hatimaye ameibuka na kuutoa ukweli wake kuhusiana na sanaa anayoifanya na watu wake wa karibu ambao wanajulikana kwa jina la Mapromota.
Jamaa wanaua sanaa bwana kumbe, waziwazi kaumwaga ukweli wake bila kujali watamfanyaje baada ya makala hii kuchapishwa.
Unajua wanaiuaje sanaa?
Marlaw amesema ‘mapromota’ wanachangia kwa kiasi kikubwa kushamiri kwa PlayBack katika majukwaa ya muziki kutokana na kukwepa gharama.
Mapromota hawa, …ni mabingwa wa kukwepa gharama wanapenda kuandaa mambo kijuu juu kwa manufaa yao bila kujali aibu inayomkuta msanii.
Kwa kauli hii, Marlaw amewataja tena mapromota kuwa wanaodumaza wasanii hasa wanaopiga muziki wa Zouk, ambao mara nyingi huwa mzuri unapopigwa na vyombo jukwaani..
“Unajua Live ni gharama kubwa kuliko playback, sababu kama ni live utahitaji wapigaji na waitikiaji na vyombo. Hii imekuwa ngumu sana kwa wenzetu hawa ambao kwao, muziki ni biashara, na kikubwa anachoangalia yeye ni kufanya biashara na kupata faida. Tatizo linakuja sasa ukimwambia kuwa unataka kupiga live ukimtajia gharama anaruka viunzi, anataka ucheze playback” alisema Marlow.
Si unajua tena PlayBack? Ni wewe na CD yako na begi lako la nguo za kubadili , labda, …na mtu wa kukuitikia, kwa hiyo sana sana ni watu wawili tu.
Lakini tukianza kuongelea suala la live hapa, kuna wanamuziki ambao si chini ya kumi, kuna fundi mitambo labda, na kundi hili litahitaji kula na nini, sasa promota akiangalia umati huu anahisi hasara inakuja.
Matokeo yake sasa anaona bora uwe peke yako, lakini kwa aina hii ya muziki, tutazidi kila siku kuonekana hatufanyi muziki mzuri kama akina Mutukuzi ama Kidjo ama nani, kumbe hatujapewa ile nafasi ya kufanya muziki mzuri.
Na kwa mtindo huu ndio kila siku tutakuwa tunawasifu wanamuziki wengine wa kiafrika, kutokana na muziki wao mzuri na maendeleo waliyonayo, tukidhania kwamba hatujafikia kiwango chao, kumbe pengine tunaweza, tatizo liko kwetu wenyewe, hatulipani vizuri, hivyo thanabi ya sanaa yetu tunaidumaza wenyewe.
Marlow alisema kimsingi ni mbaya kwa wasanii wa aina kama yak wake, kuendelea kukumbatia staili hiyo ya kizamani kwani haiwezi kuwafikisha kwenye lengo wanalolitarajia. Ambapo kiukweli, kila mwanamuziki mdogo wa kitanzania kwa sasa ana ndoto ya kuwa mwanamuziki wa kimataifa.
“Mimi nachukia sana staili hiyo, inazidi kutudhalilisha sioni kama inatujenga kwani wakati sasa hauturuhusu sisi kuendelea kutumia staili hiyo” alisema Marlow.
Hata hivyo alisema haoni sababu za waandaaji hao au ‘mapromota’ kukwepa gharama kwani ndiyo wanawajenga wasanii kuweza kuashindana katika soko la kimataifa

Diamond...


Mdau kaomba nimwambia kijana mpya aliyeshine mwishoni mwa mwaka, me nimemtaja Diamond, ...kijana anatamba na kibao chake saaaafi, ...kinaitwa kamwambie, wadau wanajiuliza, ...ataweza kubaki?

Thursday, January 7, 2010

Jk, ..na Drogba


Umeuona Uzi?

...wanangu wa Taifa hawa, ndio jezi yetu...

Katutangaze...

Wednesday, January 6, 2010

Salam toka mjengoni...


Ni hivi, Clouds TV iko hewani na sura hizi zitashine mbaya hivi karibuni kutoka kushoto ni Sade, ..Sarah na Romeo...

VETO Kitaani...


Album ya mwana iko kitaani, ...buku tatu tu mkononi mwa wamachinga, ...usinunue zaidi ya buku tatu.
Ukiuziwa zaidi, piga namba...+255 716 627 344

Leo sijui imekuwaje?

Sijui hali ya hewa au nini? Lakini nimeshindwa kuupload wanangu, kila nikijaribu inachukua muda sana, net iko too slow, ...kesho jamani!

Tuesday, January 5, 2010

Kitu kipya, ..kutoka Tetemesha records...


Tetemesha Recordz inauanza mwaka 2010 kwa kumtambulisha artist wake mpya ambaye hajawahi kuskika. Anaitwa SAJNA, ni msanii mwenye miaka 18, anasoma form II hapa Mwanza. Kijana ana kipaji cha hali ya juu.
Ana wimbo, ..wimbo huu unaitwa NADHIFA, ni true story ambayo imemtokea yeye mwenyewe, kila alichokiimba katika wimbo huu ni cha kweli na kinamhusu yeye na familia yake.
Kwa ufupi amemuimba dada yake wa damu ambaye alitoweka nyumbani kwao bila taarifa miaka kadhaa iliyopita.
Wimbo umetengenezwa A2P RECORZ MWANZA, producer anaitwa SAM TIMBER.

Jacob Zuma amalizana na jiko la tano...

Mtu mzima hapa, ...inabidi aserebuke tu, ...mke wa tano sasa kudadadeki!