Tuesday, August 21, 2007

Boyfriend & Girlfriend

...mpenzi asiyekuwa hivi...

HAKUFAI!

Makala nyingine ninayoendesha kwelye gazeti la Mwananchi Jumamosi hii hapa, kuna mdau kaomba niiweke aisome akiwa ughaibuni.
Mwezi agosti umeisha, ..unaweza kuamini? Siku zinapotea jamani, mwaka uko kama unaisha hivi na usipoangalia unaweza ukajikuta kwamba malengo yanashindwa kabisa kutimia, madai yako yanaweza kabisa kuwa yanasubiri kesho, ...nikwambie kitu? Tommorow never comes, usiisubiri jamani tuendelee kuhangaika.
Nashkuru kwa maoni ya Starehe lililoboreshwa, mwisho wa siku, tunataka mfurahi kaka na dada zetu kwamba mnapata kitu ambacho mwisho wa siku kkinawaridhisha na kwa kweli karibuni tutakuwa tunakaa pamoja katika Club 32, ni mpya kabisa ya watu wa miaka 20 mpaka 35, ambao mimi nawaita vijana, itakuwa ya kisasa na maendeleo kidogo itakayoweza kukupa jinsi ya kuishi mjini, watu wanatapeliwa vipi, wanaume uongo wao uko wapi na wasichana warukaji wakoje na kila kitu. Kuweka na kukopa, yaani itakuwa ni ya aina yake, kaeni tayari, ...inakuja.
Leo jamani nataka kuangalia rafiki ambaye hakufai, sio katika maisha ya kawaida bali katika maisha ya mahusiano ya kimapenzi na hii ni kutokana na kusumbuliwa sana na akina dada na kaka zangu ambao wanaamini kwamba labda, ...mimi najua sana kuliko wao kumbe hamna bwana, wanaweza kuwa wao wanajua zaidi. Kilichopo, ni kwamba mimi ninao uwanja wa kusemea, lakini naamini kabisa, kuna watu wapo huko mtaani, wakipewa nafasi kama hii, wanaweza kuandika na kushauri zaidi yangu, ...namaanisha. Wapo watu wanaojua zaidi.
Najaribu kuwaangalizia visifa ambavyo, muangalie wakati mnawasoma watu tabia, kabla hamjaamua ni nini cha kufanya, mnatakiwa kujua mambo manne muhimu...
Muonekano unatengenezeka, asili ni ngumu!
Hili ni gumu sana, kuna watu mpaka leo wanahisi kwamba anaweza kabisa kuibadili tabia ya mtu, naomba niwahakikishie, kwamba kiasili kukibadilisha, unatakiwa kuwa na kipaji cha ziada lakini katka hali ya kawaida hizi ni imani ambazo haziwezekani.
Mwanamke au mwanamke, kujipenda ni tabia ambazo zipo, katika hali ya kawaida ni lazima kila kijana kujipenda, teknolojia inaruhusu, lakini kuna mambo ya ndani kabisa ambayo unatakiwa kuangalia, kwa mwanaume, mwangalie mwanamke ambaye anaweza kuishi maisha ya kawaida, kila msichana ujue ni mama wa kesho, sasa angalia...

Anajali?
Muangalie, anza na hata hizi za kutoka out moja moja hivi, ..muangalie kinapoletwa chakula chako na chake, anakiangalia,au anafakamia tu cha kwake na kuagiza kinyaji na kusukumia? Hii ni ya kwanza kabisa na kabla ya hii labda mkikutana muangalia kama anaangalia shati au gauni lako, umependeza? Liko safi?
Maana kuna wengine hajali mnapoenda kama mtatiana aibu au vipi. Mtu muwazi ni mwema sana, tusidanganyane kwa kuambiana sijui tunaoneana aibu, ni uongo, kwa mpenzi wako ni lazima mtu uwe wazi ilimsiaibishane, au lisitokee lolote kusababisha hatari katika uhusiano wenu.
Mwanamke au mwanaume wa maisha utamjua tu, ukianzia kwenye vitu vidoko kama hivi. Kuna suala la malipo kwenye gharama zenu za kawaida, je mwenzako zinamuuma, au mkiambiwa toeni kiasi hiki hata kama ni nyingi mwenzako haulizi kwa nini inakuwa hivi?
Wanaume wengi wanadhani mwanamke anayelipa gharama ndio mzuri, kulipa sio tatizo, tatizo ni kuangalia hali ya maisha na matumizi yake, kama anagharimika kupita kiasi, kumbuka hizo gharama siku moja zitakuangukia, sasa jiulize utaziweza? Umeona?
Hata kama mna pesa sana. lakini kuwe na sababu ya msingi basi ya kutumia kiasi kingi ya kile mlichonacho na sio kutumia tu kwa sababu mnacho, kuna leo na kesho.

Mrekebishaji...
ogopa katika maisha yako, mtu ambaye analiona kosa leo, anakuja kulisema mnapogombana, na hapo usikute anakuwa na mengiiii ambayo ameyakusanya. Jiulize ni kwa nini kayaweka? Na kuyaweka kwake hakuwezi kusababisha yakawa mengi ikawa sababu ya nyie wawili kuachana? sasa huyo wa nini? ...siwachonganishi lakini mdomo unajenga na msisahau, ...kuna kipindi unapoza, hili mnapaswa kulijua mapema msije mkalaumu baadae.
Kama mtu ana nia na mwenzake, linapotokea jambo, hanyamazi, lazima aliseme ili kama huyu mwenzake atajieleza, ama kujirekebisha ni vema kwa manufaa ya mahusiano yako ya baadae.
Unapoweka kitu moyoni, hata mapenzi yanapungua kwa kuwa unakuwa hujui kile kitu ni kweli au sio? Anaendelea ama kaacha, unajikuta tu umeshammchukia mtu ambaye pengine hata kosa hana. Au kama kweli analo si anakuwa ana hisia kwamba hujajua, si anaendelea? Kama unampenda unamshtua mapema kwa kumwambia hivi sivyo mpenzi wangu, kuwa hivi, na kama ana sababu ya kufanya atakwambia, pengine umesababisha mwenyewe, na kama hana kama anakupenda ataacha ila kama anazuga, ndio utakapouona ukweli sasa!
Jamani sina lengo la kukosanisha watu, ..hizi ni hisia zangu kama Mdimu tu.

Anakusikiliza?
Hauna kitu chema katika maisha ya kila siku kwa fammilia inayotaka kujijenga kama kusikilizana. Kuna ubishi ambao kwa kweli nauona katika husiano zilizo karibu na mimi ambazo nahisi kwamba hauna msingi, watu ili mradi wanaishi lakini ukiangalia maisha yao, unawaonea huruma, maisha ni mashaka matupu!
Kupenda wakati mwingine ni kama ujinga, kwa hiyo unapoamua kwamba unampenda fulani, jitahidi kuhakikisha kwamba unampenda na unamsikiliza. Ukimpenda mtu, una haki ya kujua ni nini anapenda na nini hapendi, angalia mnapotoofautiana na ukipajua, hakikisha kwamba unakaa naye chini, mnaelezeana jinsi ya kuparekebisha ili muwe sawa.
Kubishiana sio kipimo kwamba wewe ndio una msimamo na kukubaliana sio kipimo ya kwamba mnapendana lakini inasaidia pia katika kuondoa misononeko midogo midogo. Mnanielewa?
Msikilize anachosema, kama una sababu za msingi za kumkatalia, sawa kama huna sababu, huna haja ya kuonesha ubabe usiokuwa na msingi eti kwa sababu tu wewe ni mwanaume, kiongozi wa familia, wenzako wapo wanaolegeza masharti kila kukicha wanaweza kukuzidi ufundi ikakosa la kufanya, ..mnanielewa jamani?
Aceni nisiseme sana kwa leo lakini, nina uhakika picha mmeipata, iwapo mna maoni kuhusiana na hizi makala zangu, niandikieni kwa:
Mdimu@hotmail.com
Au SMS
+255 787 000 880
Ahsanteni, wiki ijayo msikose kusoma Starehe, ...ni kila jumamosi!

2 comments:

Ndesanjo Macha said...

Asante na endelea kutuwekea makala zako hapa ili tulio nje tuzisome.

mzee wa mshitu said...

Karibu kaka unatisha nimesoma news zako mwana wane moto wa kuotea mbali, nakuomba kitu kimoja usitutelekeze tupachikie kila ukipatacho, karibu saana kijijini kwetu.