Tuesday, August 28, 2007

Zee la Nyeti wiki hii!

Blaza, mkwanja si wako? Mbona unakutesa?

Wanangu wa Arusha mambo VP? Hope mko poa, nataka niwashtue wana kama mlikuwa hamjashtukia, Zee la Nyeti niko jijini mwenu, jana nilikuwa nakamua ndani ya Full Shangwe za Fiesta na sasa najiandaa kuondoka kuelekea Tanga ndugu zangu, ..kwa hiyo mkiniona nakatiza mitaani msiwe na shaka ni mambo madogo tu ya mihangaiko ya kimaisha si mnaelewa?
Last wik nimepata meseji kibao kutoka kwa washkaji zangu walioko mtoni wanauliza kama kweli Zee limerudi. Nimewahakikishia, niko mtamboni na kwa wale walioko mamtoni mnaweza kunikamata kwa kupitia Henrymdimu.Blogspot.com, ..napatikana mule wanangu msiwe na shaka. waambieni na washkaji wengine mnaowajua ambao walikuwa wakilimaindi Zee tangu enzi zile, su sio wana, ...pamoja.
Mwanangu umeona jinsi watoto wa kibongo walivyofunika kwenye Boda la Kinondoni, ..ilikuwa balaa mwanangu. Mtu mzima ChidBeeeenz na Mwana FA si uliona walivyokonga. FM Academia a.k.a wazee wa Ngwasuma walimfunika Koffi, hii mkubali ama mkatae ndio ukweli, ..Ngwasuma liko juu bwana, alaa, mnataka kuniambia nini mimi mtu mzima wa zamani? Ndio nshasema sasa Ngwasuma ni kiboko yao, asiyetaka basi!
Basi unajua mzee nilitinga mida gani pale, kama moja moja hivi kimvua kama kinaangka halafu kibaya zaidi si nilikuwa aloni? Basi nikawa nimesimama plesi flani hivi karibu kabisa na basi la matangazo la Clouds FM, wenyewe wanaliita Handsome, Basi katika kusimama kwangu mara akaja mshkaji mmoja hivi kajiwasha ile mbaya na Mi'bling Bling na mi nini, nikajua mambo ya vjijana tu, nikatulia nikawa nacheki shoo zinavyoenda. Unajua yuko nani jukwaani hapo? Yuko Mwanangu mwenyewe Z Antoni anakamua na jini lake!
Basi bwana, mara wakapita mademu flani hivi wakawa kama wanaocheza cheza hivi, si unajua sasa vivazi vya binti zetu, wakawa wametinga kama Pamba flani za kichangu halafu figa zikawa zinalipa, jamaa si akadata? Akawaita, kwani na wenyewe wanajivunga? ..wakaja!
Jamaa likaangalia huku na huku, kuona watu wanamuangalia, akatia mkono mfukoni unaambiwa, ile akaibua fuba lina Msimbazi tupu kudadadeki, ...nikamuangaliaaaaaaa. wale mademu kwa kipindi chote niliwaona walikuwa wanakunywa maji, kwa nini wasiyatupe chini. MMoja akamkalia kushoto mwingine akawakalia kulia, jamaa likahisi limeopoa..
Likawauliza wanachokunya, unaambiwa mademu wakaanza kumtajia vinywaji ghali tu, wa kwanza heinneken, wa pili akataka Red Bull, akawapa kila mtu Msimbazi wake, mademu wakatambaa!
Zee kama Zee nikawa interested kujua jamaa ataishia wapi? Basi tukawa kama tuko pamoja tunasubiri wale watoto wardi. Kumbuka Fiesta ilifanyika Kinondoni, kitovuni kabisa kwa watoto wa mjini kudadadeki. Jamaa kasubiri mpaka kangoja, baada ya kama saa zima hivi wale mademu wakaibuka. Unajua walimpa zipi jamaa?
Eti walikutana na baba yao mdogo kwa hiyo wakajificha kwanza, lakini hata hivyo wakampoza na ile twente aliyowapa ya kinywaji, kwa hiyo pale walipo walikuwa wanasikia kiu kama nini, ...jamaa likajifanya halijamaindi, likakata twente nyingine, mademu wakajikata! ..sijui unaipata fresh picha yenyewe...
Safari hii wakarudi na misosi wakakaa chini wakaanza kujisevia, jamaa likawa kama linataka kuwaambia kitu lakini linashindwa, nilichomgundua mchizi alikuwa kama anatamani mademu wengine, lakini sasa hapa si keshainvesti, akawa kama anasubiri lakini kimtindo akawa kama kashtuka hivi kwwamba kuna kamchezo, ..atoke vipi? Ndio likawa tatizo pale, sijui unaipata picha kamili?
Basi mademu wenyewe bwana walikuwa wale dizaini machale flani, kila anayepita wanamsalimia, wanamkumbatia, mara kaja huyu, jamaa linaonekana hivi hivi linakereka lakini lifanyeje? Zishamtoka Fote, halafu hata ailavyu hajasema, hata kiuno hajashika kudadadeki, nikawa namhisi anatamani kulia ila sasa amlilie nani, kwani alilazimishwa?
Mademu unaambiwa wakamtoa tena teni, mmoja alijifanya hajashiba, akaenda hakurudi, demu mwingine akajifanya anamfuata, ...nduki!
Jamaa likawa limemegwa Fifte bila lenyewe kutegemea, mademu wala hakupata gudtaim nao, matatizo matupu. Nikawa sasa najifikiria kama mkwanja kama ule mtu kama mimi hapa mjini pangekuwaje jamani, ..semeni wenyewe maana kabila langu ni M'zigua nimechanganya na M'bondei!
Sasa wabondei wana Mbwembwe, Wazigua wana Ngebe, ukichanganya vyote hivi unapata kitu kinaitwa Machejo! ...wangekimbia mjini hapa, ningetembea kifua mbele utadhani nimepigwa ngumi ya mgongo kudadadeki.
Nimeamini wanangu, mkwanja sio ishu, ishu u'bontauni kaka!
Big Up wanangu wenyewe Njenje Prodaksheni, akina Kittime, Waziri na Babu Njenje mwenyewe, washkaji zangu wa Mererani VP? Nipo Arusha mjue? Mnakumbuka enzi zile za Kasheshe nilitimba huko tukawa na Gudtaim ile mbaya. Wanangu wa maulaya msisahau napatikana kwa; Henrymdimu.Blogspot.com
ze Komedi, mwanangu Seki, masanja, Mpoki, Wakuvwanga, MC Regan a.k.a Mjeshi, Vengu inakuwaje? Mko poa? Nawaaminia sana wanangu, keep it up!
Wanangu eeh, ..jumamosi ijayo hapahapa kama kawa basi...

No comments: