Sunday, August 19, 2007

Stori za Zee la nyeti!

Dogo unaremba? ..wenzako wanaperemba!

Wana, ..mko poa? Naona kama kawaida mmetimba kwenye kurasa tata, tunamuvuziosha tu hapa mwanawane hatuangalii figa kudadadeki, ..watake wasitake mwisho wa siku watajiunga na bendi tu, si unajua tena mambo ya Muziki mnene? Watabanaaaaaaaa, mwisho wa siku watajikuta tu wanakubali kwamba flagi liko juu, ....uongo wana? Tunakamua!
Ebana kwanza nianze kwa kushukuru kwa mishavu ambayo wana wameanza kuimimina, ..si kitoto nimeshtukia kwamba watu walikuwa wamelimisi sana Zee lakini ndio ilikuwa walipate wapi? Lilikuwa limewakosesha watu testi flani ambazo kwa sasa zinasababisha watu washindwe kuacha kununua Mwananchi Jumamosi, ..sasa hivi balaa kweli mtaani kila mtu anafagilia, si ndio kuna mambo ya ukweli? sasa nini tena?
Wanangu wa Dom nawashkuru sana, kwa mapokezi mliyonipa, ntakuja tena kufanya mambo kwenye Fiesta ya huko, si mnashtukia kwenye BongoFleva ni mmoja wa wadau? sasa nini tena? sasa n'na moja hii niliikuta Dom inabidi niwape mwanangu kwa faida ya wengine, si mnajua mwisho wa siku tunataka tunyooshane?
Basi mwanangu ile kutua Dom si ikabidi nianze kwenda spidi na wana ambao ni wenyeji? Nikawa nazuga striti pengine nitakutana nao, ..kweli bwana, nikakutana na mchizi flani ambaye alikuwa mitaa ya Samora kipindi flani anauza fremu, nikawa simuoni tena kumbe mwana kahamishia goli Dom kuwabana wahishimiwa, dah, ..nikawa nimepata kampani flani ambayo nikajua ningejimiksi nayo kwa siku tatu ambazo nilikuwepo hapo.
Bsi bwana, baada ya kugawana kontakti na nini, ...ikabidi mimi nimuache mchizi kijiweni kwake, niende nikalikite kwenye Gesti yangu ya buku mbili mia tano niliyofikia, ili mida mida mshkaji akishafunga Biznes, tukutane tuanze misele, ...unanisoma lakini?
Mida ilipofika, mchizi ikaja, akaniambia kwanza kabla hatujajimiksi viwanja, twende mtaani kwa demu wake tukaangalie kama tunaweza kupata kampani. Dah, ..mi mwenyewe nikaimaindi hiyo aidia, kidogo nimuulize umejuaje kama na mimi namaindi totoz? Ila nikaona sio ishu, ..nikachuna, nikakubali twen'zetu.
Dah, ..mwanangu kufika huko mwenyewe nilidata!
Acha Bunge liendelee kuwa Dom, kuna totoz hizo mwanangu sijawahi kukutana nazo. Utafikiri zina ujamaa na Mungu? Manake unaweza kujenga picha kwamba binti kaumbwa huku anajiangalia halafu anatoa maelekezo, kwamba. "...mjomba mbona unaniumba vibaya? Niongeze huku basi", anaongezwa, uumbaji ukiisha, utafikiri kashushwa!
Watoto wamefungasha kudadadeki utafikiri wanahama, mzee fasta, ...nikapointi kicheche flani cha kirangi kilikuwa pembeni, jamani akaniambia nimuachie kila kitu, atamaliza. mzee pia nikahisi nacheleweshwa nikahisi kama akinitafunia anaweza akanimalizia testi, nikamwambia we mwambie namuita, mi si mjanja? Inakuaje sasa hata Praiveti ishu nafanyiwa, ..kicheche kikaitwa!
Unafikiri kilipewa maneno mengi basi? Kiliambiwa tu kwamba mtu mzima nimemaindi mzigo, twenzetu tukajiachie siku ziende, kicheche chenyewe kikaona Yeees, huyu kichaa, hamna cha Ooh, ailavyu so machi, sijui nikujengee nyumba, Ooh nikuoe, hizo mbona wenyewe madem wenyewe washazisgtukia? Binti kama jiksi jiksi hivi akajiunga na bendi bwaba, si unaniona nilivyo balaa?
Sasa kumbe kuna mshkaji, longtaim anagharimika kweli kwa demu, naye alikuwa anammaindi ila alikuwa hajamwambia. Unaona bwana, ye mtu wa kumtoa malanchi, sijui mara kampeleka muvi, mara mnadani lakini kumwambia kwamba mambo flani anamaindi akawa anaogopa kutoswa, na yeye akawepo anga zile zile.
Alipoona mchmba kashikwa kiuno mchizi ndio naling'oa goma si ndio akaanza kuleta zake? Nikamuuliza demu inakuwaje?
Unajua demu akanipa zipi? Tumuite!
Tukamuita mshkaji tukamuulize vipi mzee? Mbona kama umemaindi hivi? Akajibu kwamba demu anavyomfanyia sivyo, siku zote wapo wote, inakuwaje anakuja mtu tu kwa sababu anatoka dar, anam'beba?
demu kwanza akamtolea kile kicheko cha kimbea,. chenye Haloooooooooooo... kwa mbele. Akamuuliza kwani wewe ulikuwa unatakaje? Mwenzako kaniambia kwamba anamaindi kuwa na mimi, lakini wewe ulikuwa unapenda kula na mimi, kuninunulia nguo na kunitilia vocha, jamaa kamaindi mpaka kupiga mbonji!
Mchizi akadai na yeye alikuwa anataka hivyo hivyo, demu akamwambia imposibo, nishamkubalia huyu, kama ulikuwa unataka si ungesema? Jamaa likaanza kumwaga michozi bwana, mi nikachukua kitu, nikatambaa!
Dah, ila kufika mbele mbele nikakumbuka washkaji wenye tabia hii, ujue kuna watu wanaremba sana matokeo yanakuwa kupigwa bao? We ushamaindi kitu, kwa nini usishughulikie mapema, unaanza kuremba, unadhani unakiona peke yako? Unataka kulaumu watu bila sababu za msingi?
sasa wewe remba mwanangu, ..wenzako wanaperemba kudadadeki..
Ebwana mi ngoja leo niwaachie hapa ila Big Up kwa wote wanaonipa Big Up, washkaji wote ambao wanataka kuchangia, No sweti, anuani pepe ni HMdimu@Mwananchi.co.tz na simu ni 0787 000 880
Msilete mambo ya kifala lakini, kuna watu huwa wanapiga kutaka kuzinguana na mimi, simaindi, tuonane wiki ijayo wanangu, na jioni kwenye Fiesta si kama kawa? Tupeane hai tukionana...

2 comments:

Pereira said...

You guys having Blogg in Bongo you one serious problem, it is typographical error, we don't like to see typo error everyday in every Bloog. I specifically talking about yours Zee la Nyeti, please check words in Swahili our native language!! Also where caps lock apply I find a small one, watch out one day if you write my name pereira instead of Pereira I will shoot you.

Otherwise Bravo Kaka, you are great and you are on top kaka, we say what we say but we need to give you credits you deserve. Big Up to you brother and all the stuffs you are trying to put is fine and tunafagilia mno. Soon it will get better and best, rectofy these small small things kaka.

Bring many stories, put some nice pics and great events, you are the best so we expect the best things here.

Pereira said...

You guys having Blogg in Bongo you one serious problem, it is typographical error, we don't like to see typo error everyday in every Bloog. I specifically talking about yours Zee la Nyeti, please check words in Swahili our native language!! Also where caps lock apply I find a small one, watch out one day if you write my name pereira instead of Pereira I will shoot you.

Otherwise Bravo Kaka, you are great and you are on top kaka, we say what we say but we need to give you credits you deserve. Big Up to you brother and all the stuffs you are trying to put is fine and tunafagilia mno. Soon it will get better and best, rectofy these small small things kaka.

Bring many stories, put some nice pics and great events, you are the best so we expect the best things here.