Friday, August 31, 2007
Kesho!
Wadau wanataka kujua jarida ninalofanyia kazi kwa sasa, hili ndio goma lenyewe, na hili ni toleo la kesho, nakahariri haka ka pullout kanakotoka kila Jumamosi na gazeti la Mwananchi.
...nako kanaongoza Tanzania kwa burudani!
Tembele!
Banana Zorro
Kesho kuna kazi!
Sitaki Rasta!
Mzee wa kulialia..
Sekioni
Kuna mdau kaniuliza hivi yule muigizaji Seki wa mambo hayo yuko wapi? Nimemuwekea hii makusudi ajue kwamba kijana siku hizi yuko Juu, ni mtangazaji wa kipindi cha City Sound, kiko kila Jumatatu na ni maarufu sana hapa Bongo na pia ni mtayarishaji wa kipindi cha Ze Comedy ambacho kina chati kuliko Big Brother ya mwaka huu!
Maigizo aliacha zamaaaani, na hapo ni moja ya matukio katika kipindi chake cha City Sound...
Jokate
Kulia kabisa jamani anaitwa Jokate, huyu dada ni Miss Tanzania namba 2 ambaye ametunza heshima yake vilivyo, kesho anakabidhi taji la balozi wa Redds ambalo ameliwakilisha vema kwa mwaka mzima, shughuli ya kutafuta mrithi wake anaiendesha mwenyewe, hapa akishirikiana na wadau wa Sophia Records, Matukuta, wa pili kutoka kulia na Claud kushoto kabisa, huyu mwingine sijui anaitwaje vile...
Tuesday, August 28, 2007
Kingwendu Ngwendulile
Zee la Nyeti wiki hii!
Blaza, mkwanja si wako? Mbona unakutesa?
Wanangu wa Arusha mambo VP? Hope mko poa, nataka niwashtue wana kama mlikuwa hamjashtukia, Zee la Nyeti niko jijini mwenu, jana nilikuwa nakamua ndani ya Full Shangwe za Fiesta na sasa najiandaa kuondoka kuelekea Tanga ndugu zangu, ..kwa hiyo mkiniona nakatiza mitaani msiwe na shaka ni mambo madogo tu ya mihangaiko ya kimaisha si mnaelewa?
Last wik nimepata meseji kibao kutoka kwa washkaji zangu walioko mtoni wanauliza kama kweli Zee limerudi. Nimewahakikishia, niko mtamboni na kwa wale walioko mamtoni mnaweza kunikamata kwa kupitia Henrymdimu.Blogspot.com, ..napatikana mule wanangu msiwe na shaka. waambieni na washkaji wengine mnaowajua ambao walikuwa wakilimaindi Zee tangu enzi zile, su sio wana, ...pamoja.
Mwanangu umeona jinsi watoto wa kibongo walivyofunika kwenye Boda la Kinondoni, ..ilikuwa balaa mwanangu. Mtu mzima ChidBeeeenz na Mwana FA si uliona walivyokonga. FM Academia a.k.a wazee wa Ngwasuma walimfunika Koffi, hii mkubali ama mkatae ndio ukweli, ..Ngwasuma liko juu bwana, alaa, mnataka kuniambia nini mimi mtu mzima wa zamani? Ndio nshasema sasa Ngwasuma ni kiboko yao, asiyetaka basi!
Basi unajua mzee nilitinga mida gani pale, kama moja moja hivi kimvua kama kinaangka halafu kibaya zaidi si nilikuwa aloni? Basi nikawa nimesimama plesi flani hivi karibu kabisa na basi la matangazo la Clouds FM, wenyewe wanaliita Handsome, Basi katika kusimama kwangu mara akaja mshkaji mmoja hivi kajiwasha ile mbaya na Mi'bling Bling na mi nini, nikajua mambo ya vjijana tu, nikatulia nikawa nacheki shoo zinavyoenda. Unajua yuko nani jukwaani hapo? Yuko Mwanangu mwenyewe Z Antoni anakamua na jini lake!
Basi bwana, mara wakapita mademu flani hivi wakawa kama wanaocheza cheza hivi, si unajua sasa vivazi vya binti zetu, wakawa wametinga kama Pamba flani za kichangu halafu figa zikawa zinalipa, jamaa si akadata? Akawaita, kwani na wenyewe wanajivunga? ..wakaja!
Jamaa likaangalia huku na huku, kuona watu wanamuangalia, akatia mkono mfukoni unaambiwa, ile akaibua fuba lina Msimbazi tupu kudadadeki, ...nikamuangaliaaaaaaa. wale mademu kwa kipindi chote niliwaona walikuwa wanakunywa maji, kwa nini wasiyatupe chini. MMoja akamkalia kushoto mwingine akawakalia kulia, jamaa likahisi limeopoa..
Likawauliza wanachokunya, unaambiwa mademu wakaanza kumtajia vinywaji ghali tu, wa kwanza heinneken, wa pili akataka Red Bull, akawapa kila mtu Msimbazi wake, mademu wakatambaa!
Zee kama Zee nikawa interested kujua jamaa ataishia wapi? Basi tukawa kama tuko pamoja tunasubiri wale watoto wardi. Kumbuka Fiesta ilifanyika Kinondoni, kitovuni kabisa kwa watoto wa mjini kudadadeki. Jamaa kasubiri mpaka kangoja, baada ya kama saa zima hivi wale mademu wakaibuka. Unajua walimpa zipi jamaa?
Eti walikutana na baba yao mdogo kwa hiyo wakajificha kwanza, lakini hata hivyo wakampoza na ile twente aliyowapa ya kinywaji, kwa hiyo pale walipo walikuwa wanasikia kiu kama nini, ...jamaa likajifanya halijamaindi, likakata twente nyingine, mademu wakajikata! ..sijui unaipata fresh picha yenyewe...
Safari hii wakarudi na misosi wakakaa chini wakaanza kujisevia, jamaa likawa kama linataka kuwaambia kitu lakini linashindwa, nilichomgundua mchizi alikuwa kama anatamani mademu wengine, lakini sasa hapa si keshainvesti, akawa kama anasubiri lakini kimtindo akawa kama kashtuka hivi kwwamba kuna kamchezo, ..atoke vipi? Ndio likawa tatizo pale, sijui unaipata picha kamili?
Basi mademu wenyewe bwana walikuwa wale dizaini machale flani, kila anayepita wanamsalimia, wanamkumbatia, mara kaja huyu, jamaa linaonekana hivi hivi linakereka lakini lifanyeje? Zishamtoka Fote, halafu hata ailavyu hajasema, hata kiuno hajashika kudadadeki, nikawa namhisi anatamani kulia ila sasa amlilie nani, kwani alilazimishwa?
Mademu unaambiwa wakamtoa tena teni, mmoja alijifanya hajashiba, akaenda hakurudi, demu mwingine akajifanya anamfuata, ...nduki!
Jamaa likawa limemegwa Fifte bila lenyewe kutegemea, mademu wala hakupata gudtaim nao, matatizo matupu. Nikawa sasa najifikiria kama mkwanja kama ule mtu kama mimi hapa mjini pangekuwaje jamani, ..semeni wenyewe maana kabila langu ni M'zigua nimechanganya na M'bondei!
Sasa wabondei wana Mbwembwe, Wazigua wana Ngebe, ukichanganya vyote hivi unapata kitu kinaitwa Machejo! ...wangekimbia mjini hapa, ningetembea kifua mbele utadhani nimepigwa ngumi ya mgongo kudadadeki.
Nimeamini wanangu, mkwanja sio ishu, ishu u'bontauni kaka!
Big Up wanangu wenyewe Njenje Prodaksheni, akina Kittime, Waziri na Babu Njenje mwenyewe, washkaji zangu wa Mererani VP? Nipo Arusha mjue? Mnakumbuka enzi zile za Kasheshe nilitimba huko tukawa na Gudtaim ile mbaya. Wanangu wa maulaya msisahau napatikana kwa; Henrymdimu.Blogspot.com
ze Komedi, mwanangu Seki, masanja, Mpoki, Wakuvwanga, MC Regan a.k.a Mjeshi, Vengu inakuwaje? Mko poa? Nawaaminia sana wanangu, keep it up!
Wanangu eeh, ..jumamosi ijayo hapahapa kama kawa basi...

Saturday, August 25, 2007
Besta!
Jamani, ..huyu mtoto anaitwa Besta, juzi juzi hapa ndio kajitambulisha kwamba ni mtanzania lakini hapo awali alikuwa akifanya muziki wake uganda. Toto la kihaya hili tukitaka kujipa matumaini ya kumuona Beyonce huwa tunachukua kasi kwa huyu, ...jana Arusha, ilikuwa soo jama, mtoto sijui anajijua huyu kama nanihii....?
Wednesday, August 22, 2007
Kijivua
Yalaaaa!
mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania akitangaza jinsi ya kuingia katika kinyang'anyiro ya huyo mlimbwende, kwa mwaka huu ambacho kitafanyika kwenye viwanja vya Leaders Club.
Kiingilio ni Tshs 75,000 za kitanzania bwana, halafu kuna udaku kwamba, onesho limeuzwa kwa Vodacom, kwa hiyo wapenda raha za bure a.k.a Complimentaries, mtafuteni Mafuru kama mnamjua!
Ze Machozi Band!
Kila iJumaa wenyewe tunakuwa na dada Jide katika kaukumbi kamja hivi, kako nyuma ya mgahawa wa best Bite uko Namanga jijini Dar es Salaam. Ka'Club kanaitwa Ruaha.
Ni Machozi Band hapo kila Ijumaa, kwa masongi ya nyumbani na ya nje na ya Jide mwenyewe, Jiunge ne bendi yetu, ..Machozi bila kulia, ...kudadadeki!
Hawa VP?
Punda Racers!
...mnh, haya!
Chikondi
Tuesday, August 21, 2007
Boyfriend & Girlfriend
...mpenzi asiyekuwa hivi...
HAKUFAI!
Makala nyingine ninayoendesha kwelye gazeti la Mwananchi Jumamosi hii hapa, kuna mdau kaomba niiweke aisome akiwa ughaibuni.
Mwezi agosti umeisha, ..unaweza kuamini? Siku zinapotea jamani, mwaka uko kama unaisha hivi na usipoangalia unaweza ukajikuta kwamba malengo yanashindwa kabisa kutimia, madai yako yanaweza kabisa kuwa yanasubiri kesho, ...nikwambie kitu? Tommorow never comes, usiisubiri jamani tuendelee kuhangaika.
Nashkuru kwa maoni ya Starehe lililoboreshwa, mwisho wa siku, tunataka mfurahi kaka na dada zetu kwamba mnapata kitu ambacho mwisho wa siku kkinawaridhisha na kwa kweli karibuni tutakuwa tunakaa pamoja katika Club 32, ni mpya kabisa ya watu wa miaka 20 mpaka 35, ambao mimi nawaita vijana, itakuwa ya kisasa na maendeleo kidogo itakayoweza kukupa jinsi ya kuishi mjini, watu wanatapeliwa vipi, wanaume uongo wao uko wapi na wasichana warukaji wakoje na kila kitu. Kuweka na kukopa, yaani itakuwa ni ya aina yake, kaeni tayari, ...inakuja.
Leo jamani nataka kuangalia rafiki ambaye hakufai, sio katika maisha ya kawaida bali katika maisha ya mahusiano ya kimapenzi na hii ni kutokana na kusumbuliwa sana na akina dada na kaka zangu ambao wanaamini kwamba labda, ...mimi najua sana kuliko wao kumbe hamna bwana, wanaweza kuwa wao wanajua zaidi. Kilichopo, ni kwamba mimi ninao uwanja wa kusemea, lakini naamini kabisa, kuna watu wapo huko mtaani, wakipewa nafasi kama hii, wanaweza kuandika na kushauri zaidi yangu, ...namaanisha. Wapo watu wanaojua zaidi.
Najaribu kuwaangalizia visifa ambavyo, muangalie wakati mnawasoma watu tabia, kabla hamjaamua ni nini cha kufanya, mnatakiwa kujua mambo manne muhimu...
Muonekano unatengenezeka, asili ni ngumu!
Hili ni gumu sana, kuna watu mpaka leo wanahisi kwamba anaweza kabisa kuibadili tabia ya mtu, naomba niwahakikishie, kwamba kiasili kukibadilisha, unatakiwa kuwa na kipaji cha ziada lakini katka hali ya kawaida hizi ni imani ambazo haziwezekani.
Mwanamke au mwanamke, kujipenda ni tabia ambazo zipo, katika hali ya kawaida ni lazima kila kijana kujipenda, teknolojia inaruhusu, lakini kuna mambo ya ndani kabisa ambayo unatakiwa kuangalia, kwa mwanaume, mwangalie mwanamke ambaye anaweza kuishi maisha ya kawaida, kila msichana ujue ni mama wa kesho, sasa angalia...
Anajali?
Muangalie, anza na hata hizi za kutoka out moja moja hivi, ..muangalie kinapoletwa chakula chako na chake, anakiangalia,au anafakamia tu cha kwake na kuagiza kinyaji na kusukumia? Hii ni ya kwanza kabisa na kabla ya hii labda mkikutana muangalia kama anaangalia shati au gauni lako, umependeza? Liko safi?
Maana kuna wengine hajali mnapoenda kama mtatiana aibu au vipi. Mtu muwazi ni mwema sana, tusidanganyane kwa kuambiana sijui tunaoneana aibu, ni uongo, kwa mpenzi wako ni lazima mtu uwe wazi ilimsiaibishane, au lisitokee lolote kusababisha hatari katika uhusiano wenu.
Mwanamke au mwanaume wa maisha utamjua tu, ukianzia kwenye vitu vidoko kama hivi. Kuna suala la malipo kwenye gharama zenu za kawaida, je mwenzako zinamuuma, au mkiambiwa toeni kiasi hiki hata kama ni nyingi mwenzako haulizi kwa nini inakuwa hivi?
Wanaume wengi wanadhani mwanamke anayelipa gharama ndio mzuri, kulipa sio tatizo, tatizo ni kuangalia hali ya maisha na matumizi yake, kama anagharimika kupita kiasi, kumbuka hizo gharama siku moja zitakuangukia, sasa jiulize utaziweza? Umeona?
Hata kama mna pesa sana. lakini kuwe na sababu ya msingi basi ya kutumia kiasi kingi ya kile mlichonacho na sio kutumia tu kwa sababu mnacho, kuna leo na kesho.
Mrekebishaji...
ogopa katika maisha yako, mtu ambaye analiona kosa leo, anakuja kulisema mnapogombana, na hapo usikute anakuwa na mengiiii ambayo ameyakusanya. Jiulize ni kwa nini kayaweka? Na kuyaweka kwake hakuwezi kusababisha yakawa mengi ikawa sababu ya nyie wawili kuachana? sasa huyo wa nini? ...siwachonganishi lakini mdomo unajenga na msisahau, ...kuna kipindi unapoza, hili mnapaswa kulijua mapema msije mkalaumu baadae.
Kama mtu ana nia na mwenzake, linapotokea jambo, hanyamazi, lazima aliseme ili kama huyu mwenzake atajieleza, ama kujirekebisha ni vema kwa manufaa ya mahusiano yako ya baadae.
Unapoweka kitu moyoni, hata mapenzi yanapungua kwa kuwa unakuwa hujui kile kitu ni kweli au sio? Anaendelea ama kaacha, unajikuta tu umeshammchukia mtu ambaye pengine hata kosa hana. Au kama kweli analo si anakuwa ana hisia kwamba hujajua, si anaendelea? Kama unampenda unamshtua mapema kwa kumwambia hivi sivyo mpenzi wangu, kuwa hivi, na kama ana sababu ya kufanya atakwambia, pengine umesababisha mwenyewe, na kama hana kama anakupenda ataacha ila kama anazuga, ndio utakapouona ukweli sasa!
Jamani sina lengo la kukosanisha watu, ..hizi ni hisia zangu kama Mdimu tu.
Anakusikiliza?
Hauna kitu chema katika maisha ya kila siku kwa fammilia inayotaka kujijenga kama kusikilizana. Kuna ubishi ambao kwa kweli nauona katika husiano zilizo karibu na mimi ambazo nahisi kwamba hauna msingi, watu ili mradi wanaishi lakini ukiangalia maisha yao, unawaonea huruma, maisha ni mashaka matupu!
Kupenda wakati mwingine ni kama ujinga, kwa hiyo unapoamua kwamba unampenda fulani, jitahidi kuhakikisha kwamba unampenda na unamsikiliza. Ukimpenda mtu, una haki ya kujua ni nini anapenda na nini hapendi, angalia mnapotoofautiana na ukipajua, hakikisha kwamba unakaa naye chini, mnaelezeana jinsi ya kuparekebisha ili muwe sawa.
Kubishiana sio kipimo kwamba wewe ndio una msimamo na kukubaliana sio kipimo ya kwamba mnapendana lakini inasaidia pia katika kuondoa misononeko midogo midogo. Mnanielewa?
Msikilize anachosema, kama una sababu za msingi za kumkatalia, sawa kama huna sababu, huna haja ya kuonesha ubabe usiokuwa na msingi eti kwa sababu tu wewe ni mwanaume, kiongozi wa familia, wenzako wapo wanaolegeza masharti kila kukicha wanaweza kukuzidi ufundi ikakosa la kufanya, ..mnanielewa jamani?
Aceni nisiseme sana kwa leo lakini, nina uhakika picha mmeipata, iwapo mna maoni kuhusiana na hizi makala zangu, niandikieni kwa:
Mdimu@hotmail.com
Au SMS
+255 787 000 880
Ahsanteni, wiki ijayo msikose kusoma Starehe, ...ni kila jumamosi!

Kalinyekalinye baaaaab!
Mtachonga sana juu yake!
mama mtoto!
Bye AC
Hitma ya Amina tayari, hapa wasichana wenzake wa mjini walikuwa wakimlia ubwabwa nyumbani kwao Mikocheni kumaliza kilio, kutoka kulia walioweka mkono kwenye sahani ni Maimartha wa EATV na Sauda wa Star TV, huyu mwingine sijui nani...
Mungu ailze roho ya Marehemu Amina Chifupa wa Mpakanjia mahala pema peponi, ..Amen
mwasiti!
Fake Pastors!
Monday, August 20, 2007
I'm so Sorry....
Ndugu zangu, mtanisamehe kwa matatizo yoyote mtakayoyaona, sijaweza bado kupost lakini kuanzia kesho nadhani mabadiliko mtayaona, leo nilikuwa na haraka kidogo..
Wa kisauzi
Pamoja Maaaan!
Arusha MTV Base VJ Finalists
Dar MVT VJ Finalists
Mlimani City
Sunday, August 19, 2007
Wazee wa Mujini!
Si unajua kwamba hawa vijana, wanaitwa AY na FA, wamejitoa juzi juzi hapa katika kundi la East Coast Team? Wanatoka kivyao sasa leo wameachia 'shughuli' yao inaitwa Asubuhi, ..wamemshirikisha Q Chief, ...ni balaa, we sikiliza redio utaipata habari yake!
Ibasemekana ni sehemu ya albam yao mpya itakayoitwa habari ndio hiyo...
Stori za Zee la nyeti!
Dogo unaremba? ..wenzako wanaperemba!
Wana, ..mko poa? Naona kama kawaida mmetimba kwenye kurasa tata, tunamuvuziosha tu hapa mwanawane hatuangalii figa kudadadeki, ..watake wasitake mwisho wa siku watajiunga na bendi tu, si unajua tena mambo ya Muziki mnene? Watabanaaaaaaaa, mwisho wa siku watajikuta tu wanakubali kwamba flagi liko juu, ....uongo wana? Tunakamua!
Ebana kwanza nianze kwa kushukuru kwa mishavu ambayo wana wameanza kuimimina, ..si kitoto nimeshtukia kwamba watu walikuwa wamelimisi sana Zee lakini ndio ilikuwa walipate wapi? Lilikuwa limewakosesha watu testi flani ambazo kwa sasa zinasababisha watu washindwe kuacha kununua Mwananchi Jumamosi, ..sasa hivi balaa kweli mtaani kila mtu anafagilia, si ndio kuna mambo ya ukweli? sasa nini tena?
Wanangu wa Dom nawashkuru sana, kwa mapokezi mliyonipa, ntakuja tena kufanya mambo kwenye Fiesta ya huko, si mnashtukia kwenye BongoFleva ni mmoja wa wadau? sasa nini tena? sasa n'na moja hii niliikuta Dom inabidi niwape mwanangu kwa faida ya wengine, si mnajua mwisho wa siku tunataka tunyooshane?
Basi mwanangu ile kutua Dom si ikabidi nianze kwenda spidi na wana ambao ni wenyeji? Nikawa nazuga striti pengine nitakutana nao, ..kweli bwana, nikakutana na mchizi flani ambaye alikuwa mitaa ya Samora kipindi flani anauza fremu, nikawa simuoni tena kumbe mwana kahamishia goli Dom kuwabana wahishimiwa, dah, ..nikawa nimepata kampani flani ambayo nikajua ningejimiksi nayo kwa siku tatu ambazo nilikuwepo hapo.
Bsi bwana, baada ya kugawana kontakti na nini, ...ikabidi mimi nimuache mchizi kijiweni kwake, niende nikalikite kwenye Gesti yangu ya buku mbili mia tano niliyofikia, ili mida mida mshkaji akishafunga Biznes, tukutane tuanze misele, ...unanisoma lakini?
Mida ilipofika, mchizi ikaja, akaniambia kwanza kabla hatujajimiksi viwanja, twende mtaani kwa demu wake tukaangalie kama tunaweza kupata kampani. Dah, ..mi mwenyewe nikaimaindi hiyo aidia, kidogo nimuulize umejuaje kama na mimi namaindi totoz? Ila nikaona sio ishu, ..nikachuna, nikakubali twen'zetu.
Dah, ..mwanangu kufika huko mwenyewe nilidata!
Acha Bunge liendelee kuwa Dom, kuna totoz hizo mwanangu sijawahi kukutana nazo. Utafikiri zina ujamaa na Mungu? Manake unaweza kujenga picha kwamba binti kaumbwa huku anajiangalia halafu anatoa maelekezo, kwamba. "...mjomba mbona unaniumba vibaya? Niongeze huku basi", anaongezwa, uumbaji ukiisha, utafikiri kashushwa!
Watoto wamefungasha kudadadeki utafikiri wanahama, mzee fasta, ...nikapointi kicheche flani cha kirangi kilikuwa pembeni, jamani akaniambia nimuachie kila kitu, atamaliza. mzee pia nikahisi nacheleweshwa nikahisi kama akinitafunia anaweza akanimalizia testi, nikamwambia we mwambie namuita, mi si mjanja? Inakuaje sasa hata Praiveti ishu nafanyiwa, ..kicheche kikaitwa!
Unafikiri kilipewa maneno mengi basi? Kiliambiwa tu kwamba mtu mzima nimemaindi mzigo, twenzetu tukajiachie siku ziende, kicheche chenyewe kikaona Yeees, huyu kichaa, hamna cha Ooh, ailavyu so machi, sijui nikujengee nyumba, Ooh nikuoe, hizo mbona wenyewe madem wenyewe washazisgtukia? Binti kama jiksi jiksi hivi akajiunga na bendi bwaba, si unaniona nilivyo balaa?
Sasa kumbe kuna mshkaji, longtaim anagharimika kweli kwa demu, naye alikuwa anammaindi ila alikuwa hajamwambia. Unaona bwana, ye mtu wa kumtoa malanchi, sijui mara kampeleka muvi, mara mnadani lakini kumwambia kwamba mambo flani anamaindi akawa anaogopa kutoswa, na yeye akawepo anga zile zile.
Alipoona mchmba kashikwa kiuno mchizi ndio naling'oa goma si ndio akaanza kuleta zake? Nikamuuliza demu inakuwaje?
Unajua demu akanipa zipi? Tumuite!
Tukamuita mshkaji tukamuulize vipi mzee? Mbona kama umemaindi hivi? Akajibu kwamba demu anavyomfanyia sivyo, siku zote wapo wote, inakuwaje anakuja mtu tu kwa sababu anatoka dar, anam'beba?
demu kwanza akamtolea kile kicheko cha kimbea,. chenye Haloooooooooooo... kwa mbele. Akamuuliza kwani wewe ulikuwa unatakaje? Mwenzako kaniambia kwamba anamaindi kuwa na mimi, lakini wewe ulikuwa unapenda kula na mimi, kuninunulia nguo na kunitilia vocha, jamaa kamaindi mpaka kupiga mbonji!
Mchizi akadai na yeye alikuwa anataka hivyo hivyo, demu akamwambia imposibo, nishamkubalia huyu, kama ulikuwa unataka si ungesema? Jamaa likaanza kumwaga michozi bwana, mi nikachukua kitu, nikatambaa!
Dah, ila kufika mbele mbele nikakumbuka washkaji wenye tabia hii, ujue kuna watu wanaremba sana matokeo yanakuwa kupigwa bao? We ushamaindi kitu, kwa nini usishughulikie mapema, unaanza kuremba, unadhani unakiona peke yako? Unataka kulaumu watu bila sababu za msingi?
sasa wewe remba mwanangu, ..wenzako wanaperemba kudadadeki..
Ebwana mi ngoja leo niwaachie hapa ila Big Up kwa wote wanaonipa Big Up, washkaji wote ambao wanataka kuchangia, No sweti, anuani pepe ni HMdimu@Mwananchi.co.tz na simu ni 0787 000 880
Msilete mambo ya kifala lakini, kuna watu huwa wanapiga kutaka kuzinguana na mimi, simaindi, tuonane wiki ijayo wanangu, na jioni kwenye Fiesta si kama kawa? Tupeane hai tukionana...

Totoooooz
Power Breakfast
Kazi imeanza kudadadeki, mwenyewe kwanza!
Subscribe to:
Posts (Atom)