Friday, January 1, 2010

Kuna watu, ..na viatu


Unawachukuliaje watu? Nyota ndogo aliwahi kuimba kwamba suniani kuna watu, ...na viatu, mimi

nina mtazamo, some..

Kaka na dada zangu, siku imefika na mambo yanaendelea, tubadilishane mawazo kidogo, ...kuhusiana na maisha yetu ya kila siku.
Ahsanteni kwa maoni ya wiki iliyopita, nashkuru sana kuona kwamba kumbe mnanielewa zaidi, hii kwangu ni kama faraja na kiukweli, imenifurahisha sana. Iwe hivi basi ambapo pia nitakosea ili mwisho wa siku makala hii iwe na faida kwenu na jamii kwa ujumla, si ndio jamani?
Leo nataka kuongea na watu kuhusiana na watu.
Mnanielewa?
Kuhusiana na hawa wenzetu tunaoishi nao humu mitaani, majumbani, makazini humu tunao, ....watu jamani nyie mnawachukuliaje? Wana nafasi gani katika maisha yako?
Ungekuwa umeniuliza mimi ningekuwa na haya ya kusema:

Ni muhimu sana...
Fikiria dunia bila watu, ...ingekuwaje? We ungekuwa nani kwanza, bila shaka unajivunia utu wako, so ndio ndugu yangu? Na kwa kweli watu ndio wamesaidia wewe kuwepo hapo ulipo kwa sababu umelelewa na watu, kama unatembea na gari basi limebuniwa na watu, na kama unafanya kazi umeajiriwa na watu au mtu, yaani kila kitu ni watu, kwa hiyo kila itakavyokuwa katika haya maisha yetu ya kila siku, ..bila watu, ..dunia si kitu.
Unanielewa sasa.
Na labda nikuongezee kumbuka waalimu wako, kumbuka wazazi wako, ..kumbuka rafiki zako, kumbuka madaktari, kumbuka wanausalama, na kumbuka viongozi wa nchi.
Watu ni muhimu sana kiukweli katika maisha yetu ya kila siku, lakini...
Watu ndio chanzo cha kila tatizo lako!
Hili nalo pia tunapaswa kuliona, ukiona uzuri sio mbaya ukaona na ubaya wa kitu ili uweze kukabiliana nacho au kuishi katika hicho, kama tunaishi na watu basi watu ndio maisha yetu.
Kiukweli hatuwezi kuishi bila watu waliotuizunguka, si mnanielewa ninachokiongelea?
Lakini, hebu fikiria, uliyegombana naye juzi ni nani? Ni mtu, kibaka aliyekupora juzi ni mtu pia, na
aliyepeleka habari mbaya kwa wakuu wako wa kazi mpaka ukapewa onyo ni mtu na aliyekusema vibaya kiasi cha wewe kushuka heshima yako kwa jamii ni mtu pia, sijui jamani kama tunaenda pamoja?
Sasa hapa nilikuwa najaribu kukuelewesha kingine, hawa watu pia ni matatizo. Unanielewa bwana, hatuwezi kuishi bila watu lakini pia tunaweza kuwa na maangalizo, sasa maangalizo kama yapi?
...hebu tuendelee...

Usiwachukulie poa...
Nisikilize mimi, sio kila anayekuwa karibu yako anakupennda, kumkaribisha mtu karibu zaidi ndio kumjulisha silaha za kukuangamiza atakapoamua. kaka na dada zangu dunia imeharibika, kuaminiana, kupo lakini sio kwa asilimia kubwa, watu wamekuwa wabaya. Anayekusifia leo, kesho ndiye atakayekuwa mstari wa mbele kukuponda, kwa hiyo kuna kila sababu ya kuwa makini na watu.
Maadui zetu ni watu pia, kwa hiyo uangalifu hapa ndio jambo la msingi.
Kwangu mimi naona ni bora adui atakayekuja kugeuka na kuwa rafiki yangu kuliko rafiki atakayegeuka kuwa adui yangu.
...huyu ni hatari zaidi kwani anajua kabisa juu ya kuniangamiza, anajua pa kuanzia, na jinsi atakavyonimaliza.
Narudia tena kwa kumalizia kwamba watu, ...ni wa kuwaangalia sana kaka na dada zangu, ningeweza kuliongelea hili kwa upana zaidi lakini sina nafasi kubwa katika hili, naomba kuishia hapa ila mawasiliano si yapo?
...tutumiane ujumbe
Henry Mdimu ni mhariri wa burudani wa magazeti ya Mwananchi, anapatikana kwa simu:
+255 787 000 880
Na Barua Pepe:
Mdimu@hotmail.com

No comments: