Saturday, January 2, 2010

Ali Kiba, kufanya kazi na Band!


NI wasanii wachache ambao wanamawazo ya kuendelea na kudumu katika fani zao au vipaji vyao katika muziki.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Ally Kiba amesema anatarajia kufungua studio pamoja na bendi yake mwaka huu wakati wowote.
Hali hiyo imekuja baada ya mwanamuziki huyo kufanya ziara za kimuziki Marekani na kujionea maendeleo ya wanamuziki na namna wanavyoishi maisha mazuri kwa kuwa na vitega uchumi vingi mbali na kutegemea muziki wao .
Akizungumza na Starehe, Ally Kiba anasema amejifunza mengi Marekani na sasa umefika wakati wa yeye kuanza kuimba nyimbo katika maonyesho live kwa kutumia bendi yake ambayo ataizindua muda si mrefu mwaka huu.
“Lengo langu nikutaka kuweza kumiliki bendi yangu lakini naona mipango yangu hiyo inakwenda vizuri na mwaka huu itaanza” anasema Kiba na kuongeza
“Mbali na bendi pia na studio ya kurekodia muziki nayo iko mbioni kukamilika, lengo ni kuweza kujiongezea kipato zaidi kwa kutumia vyanzo mbalimbali”.

No comments: