Friday, January 8, 2010

I Hate Playback, ..but...


Lawrence Malima a.k.a ‘Marlow’ kijana anayetamba na kibao kinachokwenda kwa jina la peep Peep, hatimaye ameibuka na kuutoa ukweli wake kuhusiana na sanaa anayoifanya na watu wake wa karibu ambao wanajulikana kwa jina la Mapromota.
Jamaa wanaua sanaa bwana kumbe, waziwazi kaumwaga ukweli wake bila kujali watamfanyaje baada ya makala hii kuchapishwa.
Unajua wanaiuaje sanaa?
Marlaw amesema ‘mapromota’ wanachangia kwa kiasi kikubwa kushamiri kwa PlayBack katika majukwaa ya muziki kutokana na kukwepa gharama.
Mapromota hawa, …ni mabingwa wa kukwepa gharama wanapenda kuandaa mambo kijuu juu kwa manufaa yao bila kujali aibu inayomkuta msanii.
Kwa kauli hii, Marlaw amewataja tena mapromota kuwa wanaodumaza wasanii hasa wanaopiga muziki wa Zouk, ambao mara nyingi huwa mzuri unapopigwa na vyombo jukwaani..
“Unajua Live ni gharama kubwa kuliko playback, sababu kama ni live utahitaji wapigaji na waitikiaji na vyombo. Hii imekuwa ngumu sana kwa wenzetu hawa ambao kwao, muziki ni biashara, na kikubwa anachoangalia yeye ni kufanya biashara na kupata faida. Tatizo linakuja sasa ukimwambia kuwa unataka kupiga live ukimtajia gharama anaruka viunzi, anataka ucheze playback” alisema Marlow.
Si unajua tena PlayBack? Ni wewe na CD yako na begi lako la nguo za kubadili , labda, …na mtu wa kukuitikia, kwa hiyo sana sana ni watu wawili tu.
Lakini tukianza kuongelea suala la live hapa, kuna wanamuziki ambao si chini ya kumi, kuna fundi mitambo labda, na kundi hili litahitaji kula na nini, sasa promota akiangalia umati huu anahisi hasara inakuja.
Matokeo yake sasa anaona bora uwe peke yako, lakini kwa aina hii ya muziki, tutazidi kila siku kuonekana hatufanyi muziki mzuri kama akina Mutukuzi ama Kidjo ama nani, kumbe hatujapewa ile nafasi ya kufanya muziki mzuri.
Na kwa mtindo huu ndio kila siku tutakuwa tunawasifu wanamuziki wengine wa kiafrika, kutokana na muziki wao mzuri na maendeleo waliyonayo, tukidhania kwamba hatujafikia kiwango chao, kumbe pengine tunaweza, tatizo liko kwetu wenyewe, hatulipani vizuri, hivyo thanabi ya sanaa yetu tunaidumaza wenyewe.
Marlow alisema kimsingi ni mbaya kwa wasanii wa aina kama yak wake, kuendelea kukumbatia staili hiyo ya kizamani kwani haiwezi kuwafikisha kwenye lengo wanalolitarajia. Ambapo kiukweli, kila mwanamuziki mdogo wa kitanzania kwa sasa ana ndoto ya kuwa mwanamuziki wa kimataifa.
“Mimi nachukia sana staili hiyo, inazidi kutudhalilisha sioni kama inatujenga kwani wakati sasa hauturuhusu sisi kuendelea kutumia staili hiyo” alisema Marlow.
Hata hivyo alisema haoni sababu za waandaaji hao au ‘mapromota’ kukwepa gharama kwani ndiyo wanawajenga wasanii kuweza kuashindana katika soko la kimataifa

No comments: