Tuesday, January 5, 2010

Bwana kakobe na harakati za kuzuia TANESCO...


Usishangae Mjomba, ...hizi ni harakati za Bwana Kakobe, katika kuhakikisha kwamba, ...hawa TANESCO, ..hawamzingui katika shughuli zake za kumtukuza bwana...

...inahuu?


...inahusu?

Monday, January 4, 2010

Jino kwa jino...


Hapa Didier Drogba, hapa Nadir Haroub, ...hii ya kimataifa sana mzee ingawa tulifungwa....

Saturday, January 2, 2010

KGT: 2010, ..ni kazi tu...


Kama haujawahi kukutana na KGT halafu ukakutana naye kwa mara ya kwanza, sidhani kama unaweza kuamini kuwa yeye ndo aliye’produce album bora ya mwaka katika tuzo za kill music awards, Cinderela ya Ali Kiba, ni kijana mwenye umbo dogo asiye na makuu.
Jina lake ni Omari Said Kombo maarufu kama KGT…. Usijiulize sana kirefu chake kwani yeye mwenyewe anasema KGT haina maana yoyote.
Ni audio producer kama walivyo kina Marco Chali, P Funk ns wengine, lakini pia wakati mwingine huikamata maiki, anamiliki nyimbo kadhaa nyumbani kwake.
Cha kushangaza nyimbo anazofanya yeye na kuimba yeye mwenyewe ‘hazipati air time’ ya kutosha lakini anazowafanyia watu ndugu yangu zinapata air time si kitoto kwakweli, baadhi ya nyimbo alizoimba ni ‘ One day’ na ‘something about you’.
Baadhi ya wasanii alipfanya nao kazi na anaoendelea kufanya nao kazi ni Ali Kiba, Pasha, Queen Darleen, Showdady, Manyota, Taqwa na Berry white ambao wengi wao amewafanyia albamu mzima.
Akizungumzia kazi anasema kuwa ni nzuri na inahitaji ‘concentration’ sana….. kuna baadhi ya wasanii ni wabishi hawataki kukubaliana na ukweli…. “ Ila nimejipanga vizuri kupambana kwenye hii ‘industry’ na naamini mwaka huu nitatoa albamu bora kama sio nyimbo bora.”

Bongo kuna wanamuziki?


MBUNGE wa jimbo la Mbinga na kiongozi wa bendi ya TOT, Kapteni John Komba amesema bongo hakuna wanamuziki bali kuna wasanii.
Anasema mwanamuziki anauwezo wa kuandika nyimbo na ikaimbwa na mwanamuziki yeyote duniani, lakini msanii ni mbabaishaji tu kama waliopo hapa bongo hawajui ‘notation’ nota za muziki.
Komba amesema mwanamuziki ni lazima ajue nota za muziki kama hajui ni msanii na kwa maana hiyo ni mbabaishaji na wanamuziki wengi wa bongo hawazijui.
“Mfano ninaweza kukwambia kuwa hule wimbo wa ‘We are the World’ uliandikwa na mwanamuziki ndiyo maana wanamuziki wengi namna hile waliimba bila kubabaika kwa sababu wanajua nota za muziki” anasema Komba.
Komba anasema anawaomba wasanii wa bongo waweze kuzisoma nota za muziki ili waweze kuwa wanamuziki wa ukweli.

Ali Kiba, kufanya kazi na Band!


NI wasanii wachache ambao wanamawazo ya kuendelea na kudumu katika fani zao au vipaji vyao katika muziki.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Ally Kiba amesema anatarajia kufungua studio pamoja na bendi yake mwaka huu wakati wowote.
Hali hiyo imekuja baada ya mwanamuziki huyo kufanya ziara za kimuziki Marekani na kujionea maendeleo ya wanamuziki na namna wanavyoishi maisha mazuri kwa kuwa na vitega uchumi vingi mbali na kutegemea muziki wao .
Akizungumza na Starehe, Ally Kiba anasema amejifunza mengi Marekani na sasa umefika wakati wa yeye kuanza kuimba nyimbo katika maonyesho live kwa kutumia bendi yake ambayo ataizindua muda si mrefu mwaka huu.
“Lengo langu nikutaka kuweza kumiliki bendi yangu lakini naona mipango yangu hiyo inakwenda vizuri na mwaka huu itaanza” anasema Kiba na kuongeza
“Mbali na bendi pia na studio ya kurekodia muziki nayo iko mbioni kukamilika, lengo ni kuweza kujiongezea kipato zaidi kwa kutumia vyanzo mbalimbali”.

Friday, January 1, 2010

Kesho katika Mwananchi...


Usikose kulitafuta mtaani kama uko Afrika ya Mashariki...

It's on...


Maisha Plus Season II iko hewani, ..watu wameingia kijijini jana, na hawa ni baadhi yao, ...stay tuned, ..only on TBC1

Kuna watu, ..na viatu


Unawachukuliaje watu? Nyota ndogo aliwahi kuimba kwamba suniani kuna watu, ...na viatu, mimi

nina mtazamo, some..

Kaka na dada zangu, siku imefika na mambo yanaendelea, tubadilishane mawazo kidogo, ...kuhusiana na maisha yetu ya kila siku.
Ahsanteni kwa maoni ya wiki iliyopita, nashkuru sana kuona kwamba kumbe mnanielewa zaidi, hii kwangu ni kama faraja na kiukweli, imenifurahisha sana. Iwe hivi basi ambapo pia nitakosea ili mwisho wa siku makala hii iwe na faida kwenu na jamii kwa ujumla, si ndio jamani?
Leo nataka kuongea na watu kuhusiana na watu.
Mnanielewa?
Kuhusiana na hawa wenzetu tunaoishi nao humu mitaani, majumbani, makazini humu tunao, ....watu jamani nyie mnawachukuliaje? Wana nafasi gani katika maisha yako?
Ungekuwa umeniuliza mimi ningekuwa na haya ya kusema:

Ni muhimu sana...
Fikiria dunia bila watu, ...ingekuwaje? We ungekuwa nani kwanza, bila shaka unajivunia utu wako, so ndio ndugu yangu? Na kwa kweli watu ndio wamesaidia wewe kuwepo hapo ulipo kwa sababu umelelewa na watu, kama unatembea na gari basi limebuniwa na watu, na kama unafanya kazi umeajiriwa na watu au mtu, yaani kila kitu ni watu, kwa hiyo kila itakavyokuwa katika haya maisha yetu ya kila siku, ..bila watu, ..dunia si kitu.
Unanielewa sasa.
Na labda nikuongezee kumbuka waalimu wako, kumbuka wazazi wako, ..kumbuka rafiki zako, kumbuka madaktari, kumbuka wanausalama, na kumbuka viongozi wa nchi.
Watu ni muhimu sana kiukweli katika maisha yetu ya kila siku, lakini...
Watu ndio chanzo cha kila tatizo lako!
Hili nalo pia tunapaswa kuliona, ukiona uzuri sio mbaya ukaona na ubaya wa kitu ili uweze kukabiliana nacho au kuishi katika hicho, kama tunaishi na watu basi watu ndio maisha yetu.
Kiukweli hatuwezi kuishi bila watu waliotuizunguka, si mnanielewa ninachokiongelea?
Lakini, hebu fikiria, uliyegombana naye juzi ni nani? Ni mtu, kibaka aliyekupora juzi ni mtu pia, na
aliyepeleka habari mbaya kwa wakuu wako wa kazi mpaka ukapewa onyo ni mtu na aliyekusema vibaya kiasi cha wewe kushuka heshima yako kwa jamii ni mtu pia, sijui jamani kama tunaenda pamoja?
Sasa hapa nilikuwa najaribu kukuelewesha kingine, hawa watu pia ni matatizo. Unanielewa bwana, hatuwezi kuishi bila watu lakini pia tunaweza kuwa na maangalizo, sasa maangalizo kama yapi?
...hebu tuendelee...

Usiwachukulie poa...
Nisikilize mimi, sio kila anayekuwa karibu yako anakupennda, kumkaribisha mtu karibu zaidi ndio kumjulisha silaha za kukuangamiza atakapoamua. kaka na dada zangu dunia imeharibika, kuaminiana, kupo lakini sio kwa asilimia kubwa, watu wamekuwa wabaya. Anayekusifia leo, kesho ndiye atakayekuwa mstari wa mbele kukuponda, kwa hiyo kuna kila sababu ya kuwa makini na watu.
Maadui zetu ni watu pia, kwa hiyo uangalifu hapa ndio jambo la msingi.
Kwangu mimi naona ni bora adui atakayekuja kugeuka na kuwa rafiki yangu kuliko rafiki atakayegeuka kuwa adui yangu.
...huyu ni hatari zaidi kwani anajua kabisa juu ya kuniangamiza, anajua pa kuanzia, na jinsi atakavyonimaliza.
Narudia tena kwa kumalizia kwamba watu, ...ni wa kuwaangalia sana kaka na dada zangu, ningeweza kuliongelea hili kwa upana zaidi lakini sina nafasi kubwa katika hili, naomba kuishia hapa ila mawasiliano si yapo?
...tutumiane ujumbe
Henry Mdimu ni mhariri wa burudani wa magazeti ya Mwananchi, anapatikana kwa simu:
+255 787 000 880
Na Barua Pepe:
Mdimu@hotmail.com

Zee la Nyeti wiki hii...


Acheni ukavu, ..toeni mashavu...

....dadadadeki..
Mwaka wa tabu uleeeee....
Big Up wanangu wote wa kitaa, tumesavaivu, ...ingawa mwaka dizaini kama ulikuwa sio hivi, watu walipigika ile ile, ..kila dili lilibuma mpaka ikafikia taimu watu wanaona, ...bore wakimbie mji, lakini mabontauni tukakomaa, mpaka mwaka umeisha na hakuna aliyeona diferensi, uongo mwanangu?
Big Up kwa wanangu wote waliokomaa kama mimi, kwenye Bata tulikuwemo, kwenye mitikasi kama kawa japo ilikuwa inabuma lakini hatukuwahi kuogopa ishu, ukija mchongo watu walikuwa wanapiga tu, matokeo mbele kwa mbele, ubume, uwe poa, ..kesho yake tu unakuta watu kitaani kama kawa, na Bata ni kuanzia Jumatatu mpaka Jumatatu.
Unabishaaa?
Haina kulaumu kudadadeki, kama uliharibu mwanzoni unafikiri ishu zitajimeki mwishoni kimiujiza? ..haina tangu mwanzo unatakiwa kujipanga fresh mwana, kweli mwaka ulizingua lakini mbona kuna ambao walikuwa poa tu? Nawashtua wana sasa, mwaka umeanza,..kama kkuna muda wa kujipanga ndio huu.
Usije kulaumu mida mida...
Mipango sio matumizi kajisemea mtu mzima Kingwendu Ngwendulile...
Si uliisikia ile ngoma yake kipindi kile, ...ilikuwa ina maana zake, na maana zenyewe ndio kama hizi.
Juzi nilikuwa na Deiwaka mwenzangu Sugu tunatathmini ishu mbiuili tatu za mwaka wa tabu tukashtukia kwamba wana wengi walibugi na waliokuwa kwenye chaneli hawakupiga ishu za maana kutokana na nini, waliokuwa wamewazunguka wengi kilikuwa hakijaeleweka, watu wakabaki kuonbeshana lav na nini, ..mambo ya msingi wakayapotezea.
Halafu dizaini, wana hawajashtuka hivi, wale waliokuwa kwenye chaneli bado wengine walikuwa wanammaindi kuwapa sapoti mademu zao, wanawaacha machizi wanapigika, wako kama hawajashtukia hivi kwamba ukiwezesha machizi, ni kama unaendeleza nchi hivi, machizi wanainvesti humu humu, mi leo ngoja kuna watu niwachane, wakimaindi kivyao au sio?
Mwaka huu japo ulikuwa wa tabu lakini, dizaini machizi tuliokuwa tunahangaika faa beki wote angalau watu wamepewa vioitengo nini, wanakamatia mfano mdogo mwanenu nimekabidhiwa kitengo cha Burudani na muziki hapa MCL, Ojuku Abraham, mhariri wa Bingwa, umeona? Mwanetu Jack Mbando katulia Tigo, Shyrose na Morris Njowoka wako NMB, Suka kala kitengo cha Muziki Clouds FM, na Seba Maganga ndio mkuu wa vipindi...
Kimsingi siwezi kuwattaja wote lakini dizaini mnaelewa kwamba wana, ambao tulikuwa tunakula Bata tangu enzi za pulsaidi, mpaka leo tunaegzisti, halafu tumekalia vitengo, unakubali?
Hii inatokana na ubishi na uwezo wa hivi vichwa, lakini tatizo liko moja, wanetu wa kitaa tunawasaidiaje? Watu tumekalia vitengo, halafu wana bado wanafanyishwa shoo za kilo tano, wakija wanaijeria tunawapa doola buku stini, ..haukamz?
Wana wanataka kutoka ikitaani wafanye mabiznes na nini, mnawapa shavu? Mikopo hii vipi akina Abdallah huko Stanbiki?
Siwachani kwamba muwapendelee wana kwa sababu ni wana, ila kiukweli, kitaa kuna vichwa ambavyo vikiwezeshwa hata sura na nchi itabadilika, utashangaa wana ndio wanakuwa mainvesta siku za mbeleni, unabisha?
Mashavu muhimu kupeana, kama uwezo upo, ila ndio hivyo, wana wanawaangalia watu wao, machizi wanaona poa kuwasapoti mademu zao hata kama hawana ishu za maana huku machizi wenye aidia za msingi wanapigika kitaani.
...sio mzuka wala nini....
Nimewamaindi!
Au dizaini mwana anataka umpige tafu unamwambia akupe mkwanja labda hivi, we mkwanja atakaokupa mwanao ambaye mnamingo wote kitaa utakusaidia nini? Mpe fadhila uone, ..samtaimz poa tu kupunguza hii mizinga ya buku tano tano, mpaka mwekundu hivi, tuwawezeshe wenzetu jama, au sio?
Najua hamjanimaindi.
Hepiniuyia....;

Heri ya mwaka mpya


Mimi na timu yangu nzima ya Starehe Magazine, tunawatakia wasomaji wetu heri ya mwaka mpya, ...kwa heri mwaka wa tabu...

Tuesday, September 8, 2009

BSS walivyoleta 'njaa' kwa mashabiki


Mwishoni mwa wiki kulikuwa na kazi temeke, baada ya kwenda Mlimani na Coco Beach kwa washua, watoto wa BSS walijaiachia TCC Chang'ombe na shoo ikawa kama hivi.
Huyo ni Beatrice

Sarafina naye alikuwepo...

Paschal naye kazini...

George aliwakilisha kihivi...

..Mwapwwani na mambo yake yaleeee...

Mtu mzima Msechu naye kazini...

Kisha kwa pamoja wakangia uwanjani...

..na Nyomi lilikuwa kihivi baaab!

Watoto wa Ilala


Mabinti kutoka Ilala wakijinadi kuliwakilisha vilivyo jiji la Dar es salaam katika kambi ya Miss Tanzania ambayo imeanza leo katika Hotel ya Girrafe View Hotel
Kambi ilianza rasmi jana

Yu wapi?


Tangu tusikie amekula shavu la Sony Music amekuwa kimya sana, washakunaku, wakunwaji wa masuala ya muziki na mashabiki wake, kwa pamoja wanaungana na kuuliza, yuko wapi?
Mwenye jibu alete

Sunday, September 6, 2009

BBR Dinner Party, kula haikuwa rahhisi kiviiiile...


Dada Furaha wa Multichoice bwana, leo aliwaambia watu hakuna kula mpaka mmalize kazi, watu ikabidi waingie mzigoni, hii ilikuwa meza yangu, kamanda wetu alikuwa Ambwene Yesaya

Jipangeni wanangu, sio ishu wala nini, kamanda Ambwene akiweka sawa wanawe!

..hatimaye watu wakafanikiwa...

The Revolution 2009


Big Brother nyingine inaanza leo vijana wanaingia kambini kuanzia saa 12 za jioni, tukae tayari...

...na humu, ..ndimo watakamojidai...

He, ..kawa mtangazaji?


Jamani, huyu si yule Charls wa Maisha Plus jama? ..haya nasikia kala shavu Clods TV, ..kaaazi kweli kweli..
Na tuisubiri

Umasaini...


...baada ya kuwapima pima sana warembo, majaji waliokuwa wakipiga misele ya kumtafuta kisura wa Tanzania mwaka huu, misele ambayo imedhaminiwa na Vita Matl Plus wakaamua kuweka pozi, kushoto ni Emmy Melau, Ally Remtullah a.k.a Superstar, na Nashino...
Kazi inaendelea

Mama Sambona


Misoji Nkwabi mshindi wa shindano la Bongo Star Search mwaka jana amemaliza kurekodi tamthilia inayoitwa Mama sambona nchini Ujerumani, kaa tayari kuiona, hapa ni wakati akiwa katika kuitengeneza

Saturday, September 5, 2009

Kwa hisani yenu...


Jamaa anatia huruma jama na tuzo anahitaji, ili kumfanikisha andika neno BHH AY kwenda 0789 777 333
Utakuwa umemsaidia sana