Penzi la kuibia tamu? Nani kakwambia?
Jamani, duniani kuna mambo, haya, na tuanze kwa kumshukuru Mungu kwa kuweza kuturuhusu tukutane tena Jumamosi hii na kuchukua muda wetu mchache kuongea angalau kwa uchache kuhusiana na suala zima la mahaba, mimi mzima, hofu na mashaka ni juu yenu nyie mlio mbali na upeo wa macho yangu. Ila nina imani mmesalimika!
Leo nina mada ambayo nilikuwa nimekaa kijiweni Ijumaa iliyopita, nikawakuta watu wazima na akili zao wanaijadili huku wakiipa sifa kweli hali ya penzi la kuibia, kwamba lina utamu uliopitiliza, nilipobisha, nikaambiwa usisikie, usiombe ukajaribu, unaweza ukagombea kuwa mwenyekiti wa chama cha wezi wa wake za watu!..nikaondokamahala pale maana nikahisi ningesikiliza sana ningeshawishika, ..mjue ni dhambi halafu madhara yako bayana,
Unaona bwana, sasa katika tafakuri yangu kuna mambonimeyagundua, kwa asiye naakili timamu anaweza akasema kwamba kuna faida nyingi atapata ambazo nitazisema kwa mafungu kama kawaida yangu na nitaongelea asthari katika kipengele cha mwisho kabisa.
1. Halina gharama!
Unaona bwana, watu wengi ambao ni wezi wa wake za watu hulifurahia penzi la wizi kwa kuwa hutunziwa hawa wanawake, yaani mwenye mke anapendezesha, amalisha na kila kitu, yeye kazi yake inakuwani kufurahia penzi tu ambalo halionei uchungu kwa hiyo yeye anakuwa anafaidi zaidi kuliko mwenye mali.
Kama anaingia gharama utakuta ni ya simu ya kumpigia, au kama wanakutana mahala mamb ya chakula na malazi kama wataamua kulala jambo ambalo ni sawa na hakuna kuliko ambavyo kama angekuwa na mtu ambaye labda angekuwa anamhudumia.
Hii ni mojawapo ya raha ambayo wezi wa wake za watu wanaifurahia na ni sababu ya msingi kiasi fulani inayopelekeawao kusema ni kwa nini penzi la kuiba ni tamu...
2. Penzi moto!
Kuna ujinga ambao naamini kabisa kuna wanandoampaka leo wanaufanya, nao ni kujifanya wana heshima saaaana baina yao, hata katika masuala ya mapenzi. Kifupi hawako wazi, wanakuwa wanakificha kile ambacho wanakipenda sana wanapokuwa mahabani, matokeo yake utakuta mtu tangu anaingia kwenye ndoa, mpaka anapata watoto, anakuwa hafurahii kabisa mahaba na mumewe.
Sasa ndio usiombe akaja akakutana na huyu mwizi ambaye atataka kuonesha maujuzi yake ili amteke mwenzako kiakili, ....utajuta!
Mara nyingi mapenzi ya namna hii ya kuiba watu huwa huru kufanyiana kila upuuzi unaohusianan a mapenzi, na hapa ndio utamu unapoanzia. Kingine penzi moto litakuja pale ambapo mtu anaudhiwa huko nyumbani, wanakuwa wanalala 'Mzungu wa nne', huyu ndio huko anakoiba ama kuibiwa anamalizia usongo wote!
....pata picha mwenyewe!
3. Haina kero..yaani shwari tu!
Unajua kuna jambo moja baina yetu wanadamu, mpaka watu mgombane, lazima mtakuwa kwa kiasi fulani mezoeana, sasa hawa wanaoibana mara nyingi huwa wanapatana sana maana muda wa kukaa na kuanza kusomana huwa hawana, hawa mara nyingi wakikutana wanakuwa na kazi moja tu, mahaba moto moto kisha wakimaliza kila mtu anaishia kivyake.
Tofauti na wenye husiano za kudumu, kunakuwa na migogoro iliyoongozana. Kila mara wanakuwa wanagombana na hii mara nyingi inakuwa ni kero baina yao. Na hii ni sababu mojawapo wezi wa mapenzi wanakuwa wanaamini kwamba ni bora penzi la kuibia, kuliko kuwa na uhusiano na mtu.
Maana kingine ni kwamba si unajijua ni mwizi? Kwa hiyo hata kuchunga sana unakuwa huna haja, mwenye mke si atakuwa analindakwa niaba? Sasa wewe presha za nini?
Mimi kwa leo naona niishie hapa, wiki ijayo ndio nitakupa madhara ya kuibia penzi, lakini kama una maoni tuma ujumbe kwenye namba +255 787 000 880 uniambie au kwa email:
Mdimu@hotmail.com
No comments:
Post a Comment