Tuesday, June 2, 2009

Unamjua fresh Che Guevara?


1. Pamoja na historia ya kuwa jamaa alikuwa akipigania uhuru wa Cuba, hakuwahi kuwa raia wa nchi hiyo, alizaliwa Argentina lakini pia hakuwa na asili ya nchi hiyo, Wazazi wake ni raia wa Ireland. So Che alikuwa Muairish.

2 Wakati huo mtu akiitwa 'Che Guevara' ilikuwa ikimaanisha kuwa mtu huyo anaweza kuwa mtu mzuri au mbaya, baadhi ya watu walikuwa wakimwita jina hilo wakimaanisha mpiganaji lakini wengine walimwita hivyo wakimaanisha muuaji.

3. Jina lake la utani lilikuwa Chacho ambalo kwa hapa bongo angeitwa nguruwe, Suala la kuoga kwa Che Guevara lilikuwa mtihani mkubwa. shati na suruali zake alivaa kwa wiki nzima.

4. Hakuwa akipigana kwa njaa na kukosa elimu, aligraduate masomo ya udaktari mwaka 1953. Alitokea katika familia ya kitajiri tofauti na wapiganaji wengi tunaowasoma leo katika historia.

5. Baada ya harakati alikuwa akiweka silaha chini na kutumia mikono hiyo kulea watoto wake, Che alikuwa baba wa watoto watano, mtoto wa kwanza alimzaa na mke wake wa kwanza Hilda Gadea na wengine aliwazaa na mwanamke mwanamapinduzi, Aleida March.

6. Bolivia wanamtukuza wakiamini kuwa Che ni nabii, huko Cuba sura yake ipo kwenye dola tatu na mashuleni kila siku asubuhi watoto hula kiapo wakisema "tunataka kuwa kama Che".

7.kubwa kuliko yote ni kwamba Che alikuwa akipendwa na watu wengi nchini cuba lakini idadi hiyo ililingana na ya watu wanaomchukia.

No comments: