Tuesday, June 9, 2009

Je wajua?


1. Michoro ya kondom iligundulika katika mapango huko Marekani, michoro hiyo ilichorwa miaka 15,000 iliyopita.Hata hivyo haijulikani kondomu za wakati huo zilikuwa zikitengenezwa kwa 'material' gani.

2. Hapo mwanzo kondomu zilikuwa zikitolewa iwapo tu utakuwa umeandikiwa na daktari, wanaume walikuwa wakiandikiwa na daktari watumie kondomu kwa ajili ya kujikinga na magonjwa ya zinaa na wanawake walikuwa wakiandikiwa watumie kondomu ili wasipate ujauzito.

3. Kondomu ya kwanza ya mpira ilitengenezwa mwaka 1855. Zilitengenezwa maalumu kwaajili ya wanajeshi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Waingereza.

4. Wakati wa vita kuu ya kwanza ya dunia chama cha afya cha Marekani kilikuwa kikipinga matumizi ya kondomu kwa madai kuwa kama mtu ameamua kufanya mapenzi na mwanamke asiyemfahamu anastahili kupata magonjwa ya zinaa.

5. Wakati hapa kwetu ndo tumeingiza mashine za kuuzia kondomu huko mashariki ya mbali mashine hizi zimetimiza miaka 80 tangu zilipoanza kutumika.

6. Kaa tayari kwa kondomu za kupaka, yes unapaka kama mafuta then zinakauka na kuwa kama kondomu uzijiazo, Salama, Dume, Durex n.k. hivi sasa kondomu hizi zinafanyiwa majaribu ya mwisho mwisho kwa taarifa ni kwamba kondomu hizi ninakuwa kama jelly ambayo ukiipaka inapata joto na kukauka.

1 comment:

Anonymous said...

hizo condom za kupaka zinafanyiwa utafiti wapi ndugu yangu? mbona leo ndo mara yangu ya kwanza kusikia, au na wewe unaleta nyepesi nyepesi